24-1013 Ono La Patimo

UJUMBE: 60-1204E Ono La Patimo

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno Mkamilifu, 

Ni kitu gani kinachotukia ndani ya Bibi-arusi kote ulimwenguni? Tunaingia katika Roho, tukiinuka na kupaza sauti, “Utukufu! Haleluya! Bwana asifiwe!” Mungu anatusafirisha na kulifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake.

Mambo ambayo tumeyasoma na kuyasikia maisha yetu yote sasa yanadhihirika. Uhuishaji mkuu unatendeka. Tumeangaziwa na Neno kuliko wakati wowote. 

Tunalihisi ndani kabisa ya nafsi zetu. Kuna kitu fulani cha tofauti, kuna kitu kinatendeka. Tunamhisi Roho Mtakatifu akitutia mafuta, akiijaza mioyo na akili zetu kwa Neno Lake. 

Tunaweza kumsikia Yeye akisema nasi: Najua adui anapigana nanyi kuliko hapo awali, lakini msiogope enyi watoto wadogo, NINYI NI WANGU. Ninawapa upendo Wangu, ujasiri na uwezo. Mnene tu Neno, nami nitalitimiza. Mimi ni pamoja nanyi siku zote.

Katika somo letu kuu la Ufunuo wa Yesu Kristo, tuko chini ya matazamio makubwa kila wiki nini kifuatacho Atakachotufunulia. Neno lake ndilo kimbilio letu pekee, amani na faraja yetu. Tunasikiliza kwa makini tena na tena na tena. Kila aya ndogo tunayosoma, tunataka kupiga kelele na kupaza sauti wakati Neno linapofunuliwa mbele ya macho yetu. Imani ya Kunyakuliwa inakuja juu ya Bibi-arusi, ikizijaza nafsi zetu.

Hebu wazia, hakuna mahali pengine ulimwenguni unapoweza kwenda, ila papo hapo kwenye vidole vyako, kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nawe na kulifunua Neno Lake. 

Jinsi ambavyo Mungu alivyoliondoa lile pazia, akalivuta, na kumruhusu Yohana atazame ndani na kuona kile ambacho kila wakati wa kanisa ungefanya, na kuyaandika katika Kitabu na kututumia sisi. Ndipo, wakati utimilifu wa wakati ulipotimia, Mungu alitutumia sisi malaika Wake wa saba mwenye nguvu kukinena, na kufunua yote Ilichomaanisha. 

Yohana aliandika kile alichokiona, lakini hakujua maana yake. Yesu hata hakulijua hilo wakati alipokuwa hapa duniani. Hakuna mtu katika nyakati zote aliyejua, mpaka siku hii, wakati huu, watu hawa, SISI, Bibi-arusi Wake.

Jinsi ambavyo ametufunulia kwamba hizo taa saba zilikuwa zikifyonza uhai na nuru kutoka kwenye hazina ya hilo bakuli kuu. Alitueleza jinsi ambavyo kila mmoja walivyokuwa wametumbikiza tambi zao mle. Kila mjumbe wa wakati wa kanisa alikuwa amewashwa moto na Roho Mtakatifu na utambi wake ukiwa umetumbukizwa ndani ya Kristo, akifyonza uzima halisi wa Kristo na kuitoa Nuru hiyo kwa kanisa. Na sasa, mjumbe wetu wa siku ya mwisho, aliye mkuu kuliko wajumbe wote, alikuwa na maisha yale yale na Nuru ile ile iliyodhihirishwa na maisha yaliyofichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Kisha malaika wetu mwenye nguvu anatuambia kuwa si tu kwamba kila mjumbe alionyeshwa hapo, BALI KILA MMOJA WETU NASI PIA, waamini wa kweli wa Mungu. Kila mmoja wetu pia anawakilishwa wazi wazi hapo. Kila mmoja wetu anafyonza kutoka kwenye chemchemi ile ile kama wale wajumbe. Sote tumetumbukizwa kwenye bakuli lile lile. Tumekufa kwa nafsi zetu na maisha YETU yamefichwa pamoja na, na ndani ya, Kristo Yesu Bwana wetu. 

Jinsi Yeye anavyotutia moyo kwa kusema hakuna mtu anayeweza kututoa sisi kutoka katika Mkono wa Mungu. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Maisha yetu yanayoonekana yanawaka moto na kuangaza, yakitoa nuru na madhihirisho ya Roho Mtakatifu. Maisha yetu ya ndani, yasiyoonekana yamefichwa ndani ya Mungu na kulishwa kwa Neno la Bwana. 

Vita ni vikali. Adui anashambulia kwa hasira kuliko hapo awali, akijaribu awezavyo kutuvunja moyo, kutupiga kabisa, lakini hawezi kulifanya hilo.  Mungu Mwenyewe ananena nasi kupitia midomo ya mwanadamu naye anatuambia, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE, ALIYEMCHAGUA, na hilo linamshinda shetani KILA WAKATI. 

Bwana wetu Mkamilifu, akinena Neno Lake Kamilifu, akitoa Amani Kamilifu, kwa Bibi-arusi Wake Mkamilifu.

Kama kawaida, tunaualika ulimwengu mzima uje kuchovya utambi wao ndani ya BAKULI KUU, Ujumbe huu, ambao umehifadhiwa na kutunzwa kwa ajili ya Bibi-arusi. Tutakuwa tukipiga mayowe na kupaza sauti saa 6:00 Sita MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 Moja JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikinena na kufunua yaliyotukia katika: Ono la Patimo 60-1204E.

Ndugu. Joseph Branham