24-0915 Chujio La Mtu Mwenye Busara

UJUMBE: 65-0822E Chujio La Mtu Mwenye Busara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bi. Yesu Kristo,

Roho wa Mungu aliye hai, tupulizie. Hebu tuchukue Chujio lako nasi tuishi chini ya Hilo, Bwana. Tupulizie hewa safi ya Roho Mtakatifu ndani ya mapafu yetu na ndani ya nafsi zetu kila siku. Tunaweza tu kuishi kwa Neno Lako; kila Neno litokalo katika kinywa Chako kwa ajili ya wakati huu tunaoishi.

Sisi tumeonja mambo Yako ya Mbinguni nasi tuna Neno Lako mioyoni mwetu. Tumeliona Neno Lako likidhihirishwa mbele yetu, na nafsi yetu yote imesitiriwa ndani Yake. Ulimwengu huu, na mambo yote ya Ulimwengu yamekufa kwetu.

Sisi ni chembechembe iliyo hai, mbegu Neno ambayo iliyokuwa ndani Yako tangu mwanzo Tukisimama hapa tukiivuta ile mbegu yako ya Uzima. Mbegu yako imo mioyoni mwetu kwa kujua kwako tangu awali. Ulituchagua tangu awali tusivute kupitia chochote kile, ila Neno Lako, Sauti Yako, kwenye kanda.

Ule wakati wa jicho umefika; hakuna kilichosalia ila Kuja Kwako kumjia Bibi-arusi Wako. Chujio letu ni Neno Lako, Malaki 4, Bwana Asema Hivi.

Hebu tulipande Neno Lako mioyoni mwetu, na tuazimie ya kwamba hatutageuka mkono wa kulia ama wa kushoto, bali tuishi tukiwa waaminifu Kwake siku zote za maisha yetu. Baba, tutumie juu yetu Roho Mtakatifu wa Uzima, na alihuishe Neno Lako kwetu, ili tupate kukudhihirisha Wewe.

Shauku ya mioyo yetu ni kuwa wana na binti wa kweli Kwako. Tumeketi katika uwepo wa Sauti Yako, tukiivishwa, tukijifanya wenyewe tayari kwa ajili ya Karamu yetu ya Harusi pamoja nawe hivi karibuni.

Mataifa yanavunjika. Ulimwengu unavurugika. Matetemeko ya ardhi yanaitikisa California kama vile Wewe ulivyotuambia ingefanya. Tunajua hivi karibuni Kipande kinene cha maili elfu moja na mia tano, upana wa maili mia tatu ama mia nne kitazama, labda maili arobaini ndani ya ule ufa kule. Mawimbi yataruka mpaka mkoa wa Kentucky, Na wakati kitakapozama, kitaitikisa dunia sana mpaka kila kitu juu yake kitaanguka chini.

Onyo lako la mwisho linaendelea. Ulimwengu uko katika machafuko kamili, lakini wakati wote Bibi-arusi Wako anapumzika ndani Yako na Neno Lako, ameketi pamoja katika ulimwengu wa roho unapozungumza nasi, na kutufariji njiani.

Jinsi gani tunavyoshukuru, Baba, kwamba tunaweza kwa urahisi “Kubonyeza Play” na kuisikia Sauti Yako ikizungumza nasi, kututia moyo na kutuambia:

Msiogope, enyi kundi dogo. Yote niliyo Mimi, ninyi ni warithi wake. Nguvu Zangu zote ni zenu. Uwezo Wangu ni wenu ninaposimama katikati yenu. Sikuja kuleta hofu na kushindwa, bali upendo na ujasiri na uwezo. Nimepewa mamlaka yote nanyi mnaweza kuitumia. Ninyi neneni Neno Nami nitalitimiza. Hilo ni agano Langu wala haliwezi kushindwa kamwe.”

Ee Baba, hatuna cha kuogopa. Unatupa upendo wako, ujasiri na uwezo wako. Neno Lako liko ndani yetu kulitumia tunapolihitaji. Tunalinena, na Wewe Utalitimiza. Ni agano Lako, nalo haliwezi KUSHINDWA KAMWE.

Maneno yapatikayo na mauti hayawezi kueleza jinsi gani tunavyojisikia, Baba, lakini tunajua Wewe unaona ndani ya mioyo na roho zetu; kwa maana sisi ni sehemu Yako.

Jinsi gani tunavyoshukuru kwamba Umeiandaa njia kwa ulimwengu kuisikia Sauti Yako katika wakati huu wa mwisho. Kila wiki, Wewe unaualika ulimwengu mzima uje kuungana kumsikia malaika-mjumbe wako wakati Wewe unapotulisha Chakula cha Kondoo ambacho kimehifadhiwa ili kutudumisha hadi Utakaporudi kutuchukua.

Tunakupenda Baba.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: 65-0822E Chujio La Mtu Mwenye Busara

Muda: Saa 06:00 SITA MCHANA, Saa za Jeffersonville(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika mashariki)

Maandiko: Hesabu 19:9 / Waefeso 5:22-26