UJUMBE: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 24-0908 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 23-0219 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 21-1024 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 21-0530 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 19-1013 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe – Preliminari
- 17-1112 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
Mpendwa Maskani ya Branham,
Jinsi gani macho yetu yalivyobarikiwa; maana yanaona. Jinsi gani masikio yetu yalivyobarikiwa; maana yanasikia. Manabii na watu wenye haki walitamani kuona na kusikia yale tuliyoyaona na kuyasikia, lakini hawakuyaona. Sisi vyote viwili TUMEONA NA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU.
Mungu Mwenyewe alichagua kuiandika Biblia Yake kupitia manabii Wake. Mungu Mwenyewe pia alichagua kufunua siri Zake zote katika wakati huu wa mwisho kwa Bibi-arusi Wake kupitia nabii Wake. Ni sifa Zake, Neno Lake lililodhihirishwa, likifanya jambo hilo lote kuwa sehemu Yake.
Pindi wakati wetu ulipowadia, Yeye alimwasilisha nabii Wake akawasili wakati uo huo. Alimvuvia na kunena kupitia yeye. Ilikuwa ndiyo njia Yake iliyokusudiwa tangu zamani na iliyoandaliwa ya kufanya jambo hilo. Kama vile Biblia, Ni Neno la Mungu, na si neno la mwanadamu.
Ni lazima tuwe na Yakini, mkataa; Neno la mwisho. Baadhi ya watu husema Biblia ndio Yakini yao, si yale yanayosemwa kwenye kanda; kana kwamba zinasema kitu tofauti. Ni ajabu sana jinsi Mungu ameuficha Ufunuo wa kweli wa Neno Lake kwa wengi sana, lakini ameufunua na kuuweka wazi sana kwa Bibi-arusi Wake. Wengine hawawezi kujizuia, wamepofushwa na hawana Ufunuo kamili wa Neno la Mungu lililofunuliwa.
Mungu alisema katika Neno Lake (Biblia) kupitia nabii Wake na kutuambia, “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi”. Hivyo, manabii wa Mungu waliiandika Biblia. Haikuwa wao, bali Mungu akinena kupitia wao.
Alisema katika siku yetu Yeye angemtuma Roho wake wa kweli ili atuongoze katika kweli zote. Yeye hatanena kwa shauri lake mwenyewe; lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atatuonyesha.
Ujumbe uliyo kwenye kanda ndio kweli za Mungu zilizofunuliwa. Haihitaji fasiri yoyote. Ni Mungu akilifasiri Neno Lake Mwenyewe wakati anapolinena kwenye kanda.
Hakuna mwendeleo katika yale watu wengine wanachozungumza, Ila tu kile Mungu anenacho. Kile kinachosemwa kwenye kanda ndio Sauti pekee ambayo HAITABADILIKA KAMWE. Watu hubadilika, mawazo hubadilika, fasiri hubadilika; Neno la Mungu halibadiliki kamwe. Ndio Yakini ya Bibi-arusi.
Nabii anatupa mfano wa rifarii kuwa ndio yakini katika mchezo wa mpira. Neno lake ndilo la mwisho. Huwezi kulihoji. Kile anachosema, ndivyo hivyo, Mwisho wa maneno. Sasa rifarii ana kitabu cha sheria ambacho lazima akipitie. Kinamwambia mahali yalipo maeneo ya mpira kawaida au goli, ni wakati gani salama kwako na wakati gani uko nje; sheria ni zipi kwa mchezo wa mpira.
Anasoma na kukisoma kitabu hicho ili anaponena, na kufanya uamuzi wake, hiyo ndiyo sheria, hilo ndilo neno la mwisho. Hamna budi kudumu na kile anachosema, hakuna swali, hakuna mabishano, chochote anachosema, hivyo ndivyo kinavyopaswa kuwa nacho hakiwezi kubadilishwa. Utukufu.
Ndugu Branham hakusema hupaswi kuhubiri, au kufundisha; kinyume chake, yeye alisema muhubiri, na kuwasikiliza wachungaji wenu, lakini Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda haina budi kuwa Yakini yenu.
Kunapaswa kuwe na nguzo ya kushikilia; kwa maneno mengine, mkataa. Kila mtu hana budi kuwa na mkataa huo. Ni neno la mwisho. Mungu ametoa mahali pamoja tu pa kulipata hilo, Sauti ya Mungu kwenye kanda. Ndio fasiri ya kiungu ya Neno la Mungu. NDILO NENO LA MWISHO, ILE AMINA, ILE BWANA ASEMA HIVI.
Yesu Mwenyewe alisema tunawaita “miungu,” walionena Neno Lake; nao walikuwa miungu. Alisema wakati manabii walipotiwa mafuta na Roho wa Mungu, walilileta Neno la Mungu sawasawa. Ilikuwa ni Neno la Mungu likinena kupitia kwao.
Hiyo ndiyo sababu nabii wetu alikuwa jasiri sana. Aliongozwa na Roho Mtakatifu kunena Neno la Mungu lisilokosea. Mungu alikuwa amemchagua kwa ajili ya wakati wetu. Akauchagua Ujumbe ambao angeunena, hata tabia ya nabii wetu na kile kingetukia katika wakati wetu.
Maneno aliyonena, vile alivyotenda, imewapofusha wengine, lakini imeyafungua macho yetu. Yeye hata alimvalisha kwa namna ya mavazi aliyovaa; tabia yake, shauku yake, kila kitu jinsi tu ilivyompasa kuwa, alichaguliwa tu kikamilifu kwa ajili yetu sisi, Bibi-arusi wa Mungu.
Ndiyo maana, wakati TUNAPOKUSANYIKA PAMOJA, Ni Sauti ndio tunayotaka kuiweka KUWA YA KWANZA kuisikia. Tunaamini kwamba tunalisikia Neno Safi lililonenwa kutoka kwa mjumbe mteule na aliyechaguliwa wa Mungu.
Tunajua wengine hawawezi kuliona au kulielewa hilo, lakini yeye alisema alikuwa akilizungumzia kusanyiko lake peke yake. Yeye hakuwajibika na wale ambao Mungu aliowapa wengine kuwachunga; yeye aliwajibika tu na aina ya Chakula anachotulisha sisi.
Ndiyo maana tunasema sisi ni Maskani ya Branham, kwa sababu yeye alisema Ujumbe ulikuwa kwa ajili ya watu wake tu katika Maskani, lile kundi dogo lililotaka kuzipata na kuzisikiliza kanda. Alikuwa anawazungumzia wale Mungu aliyompa kuwaongoza.
Yeye alisema, “kama watu wanataka kutengeneza chakula cha kisasa na kadhalika huko nje, wewe pata ufunuo kutoka kwa Mungu kisha ufanye yale ambayo Mungu anakwambia ufanye. Nitafanya jambo lilo hilo. Bali Jumbe hizi, kwenye kanda, ni kwa ajili ya kanisa hili peke yake.”
Jinsi gani alivyolifanya Hilo rahisi kweli kweli kwa Bibi-arusi Wake kuliona na kuisikia Sauti ya Mungu na kufuata maagizo Yake.
Iwapo ungependa kuungana nasi kuisikia Sauti hiyo, tutakuwa tukisikiliza sote kwa wakati mmoja Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika mashariki): 65-0822M – “Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe”.
Ikiwa huwezi kuungana nasi, nakuhimiza usikilize Ujumbe huu wakati wowote uwezapo.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:
Kutoka 4:10-12
Isaya 53:1-5
Yeremia 1:4-9
Malaki 4:5
Luka Mt. 17:30
Yohana Mt.1:1 / 1:14 / 7:1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13
Wagalatia 1:8
2 Timotheo 3:16-17
Waebrania 1:1-3 / 4:12 / 13:8
2 Petro 1:20-21
Ufunuo 1:1-3 / 10:1-7 / 22:18-19