UJUMBE: 65-0815 Nawe Hujui
Ndugu na Dada Wapendwa,
Kaeni karibu na Kristo. Hebu niwaonye sasa, kama mhudumu wa Injili, juu ya jambo hili. Msichukue upumbavu wo wote. Msiwazie cho chote. Kaeni moja kwa moja pale mpaka huu wa ndani wa ndani umetiwa nanga kwenye Neno, mpaka uwe ndani ya Kristo kabisa, kwa maana hicho ndicho kitu pekee ambacho kitaninino…Kwa maana, tuko katika wakati wa udanganyifu sana tuliopata kuishi ndani yake. “Utawapoteza walio Wateule kama yamkini,” kwa maana wana upako, wanaweza kufanya cho chote kama wengine wao.
Baba, Ulituonya kwamba tunaishi katika wakati wa udanganyifu zaidi ya nyakati zote. Roho hizo mbili ulimwenguni zingefanana sana, ingewadanganya walio wateule, kama yamkini. Lakini Bwana asifiwe, isingewezekana kutudanganya sisi, Bibi-arusi Wako; tutakaa na Neno Lako.
Sisi ni Uumbaji Wako Mpya, nasi hatuwezi kudanganywa. Tutakaa na Sauti Yako. Tutaitikia na kushikilia kila Neno, bila kujali mtu yeyote anasema nini. Hakuna njia nyingine isipokuwa Njia Yako iliyoandaliwa; Bwana Asema Hivi kwenye kanda.
Wakati nabii Wako alipokuwa hapa duniani, yeye alijua jinsi gani ilivyokuwa muhimu kwa Bibi-arusi kusikia kila Neno lililonenwa, kwa sababu hiyo yeye alimuunganisha Bibi-arusi Wako kwa mawasiliano ya simu. Alituunganisha pamoja kwenye Sauti Yako iliyothibitishwa ya Neno Lililonenwa.
Yeye alijua hapakuwepo na upako mkuu kuliko Sauti Yako.
Huko nje kwenye mawimbi ya simu hii, naomba Roho Mtakatifu aliye mkuu aingie katika kila kusanyiko. Jalia Nuru ile ile Takatifu tunayoiangalia papa hapa kanisani, jalia imwangukie kila mmoja, na kila mtu.
Kila kitu ambacho Bibi-rusi Wako anachohitaji kwa ajili ya kule Kuja Kwako kilinenwa, kikahifadhiwa na kufunuliwa kwa Bibi-arusi Wako na malaika Wako; hilo ni Neno Lako. Ulituambia ikiwa tuna maswali yoyote, twende kwenye kanda. Ulituambia William Marrion Branham alikuwa ndiye Sauti Yako kwetu. Kunawezaje kuwa na swali niani mwa Bibi-arusi Wako jinsi gani ilivyo muhimu kuiweka Sauti Yako kama Sauti iliyo muhimu zaidi Anayoweza kuisikia? Hakuna swali Bwana, kwa Bibi-arusi Wako.
Nabii wako alituambia juu ya ndoto ambapo alisema, “Nitapanda farasi kupitia njia hii tena.” Hatujui hilo linamaanisha nini, lakini kwa hakika Bwana, Sauti Yako imepanda farasi kwa njia ya mawimbi ya hewa leo tena, ikinena, na kumwita Bibi-arusi Wako atoke kutoka kote ulimwenguni.
Unaalikwa uje uungane nasi, Maskani ya Branham, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika mashariki) tunaposikiliza Sauti ya Mungu kupitia mawimbi ya hewa ikituletea Ujumbe: 65-0815 – “Nawe Hujui”.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma:
Ufunuo 3:14-19
Wakolosai 1:9-20