UJUMBE: 65-0711 Kuonea Haya
Mpendwa Bibi-arusi Asiyeonea Haya,
Hakujawahi kuwa na wakati au watu kama leo hii. Sisi tumo ndani yake, warithi wa yote aliyotununulia. Anashiriki utakatifu wake pamoja nasi, mpaka ndani yake, tumekuwa haki halisi ya Mungu.
Yeye alitujua tangu zamani kwa amri ya Kiungu, ya kwamba tungekuwa Bibi-arusi Wake. Alituchagua sisi, hatukumchagua Yeye kamwe. Hatukuja wenyewe, ilikuwa ni chaguo Lake. Sasa ameweka ndani ya mioyo yetu na nafsi zetu Ufunuo mkamilifu wa Neno Lake.
Siku baada ya siku, Yeye anatufunulia Neno Lake, akimimina Roho Wake juu yetu, akiyadhihirisha maisha Yake mwenyewe ndani yetu. Kamwe Bibi-arusi Wake hakuwahi kutia nanga zaidi mioyoni mwao wakijua wako katika mapenzi Yake makamilifu, na katika mpango Wake, kwa kukaa na Neno Lake, kuisikia Sauti Yake.
Upendo wa Mungu na Ujumbe huu umejaa mioyoni mwetu mpaka unabubujika tu. Hakuna kitu kingine sisi tunachotaka kusikia, kuzungumzia, kufanyia ushirika, au kushiriki tu nukuu ambayo tumesikia na kumsifu Bwana.
Sisi ni kama vile Musa upande wa nyuma ya jangwa. Tumetembea uso kwa uso na Mwenyezi Mungu, nasi tunaiona hiyo Sauti ikisema nasi; imeambatana kabisa na Neno na ahadi ya wakati huu. Imetufanyia kitu fulani. Hatuionei haya. Tunapenda kuitangaza kwa ulimwengu. Tunaamini Bwana Yesu ndiye Ujumbe wa saa hii na sisi NDIO BIBI-ARUSI WAKE.
Ametuimarisha kwa Neno Lake. Hakuna shaka hata kidogo, hii ndiyo njia iliyoandaliwa na Mungu. Mungu kamwe habadilishi nia Yake kuhusu Neno Lake. Yeye alimchagua malaika Wake wa saba kumwita Bibi-arusi Wake atoke, na kisha kumweka Yeye kwenye mstari sawa na Neno Lake.
Hakuna kitu katika maisha haya ila Yeye na Neno Lake. Hatuwezi kupata ya kutosha ya jambo hilo. Ni zaidi ya uhai kwetu sisi. Injili na Nguvu za Mwenyezi Mungu zimeenea ulimwenguni kote kuliko hapo awali. Neno sasa liko mikononi na masikioni mwa Bibi-arusi. Wakati wa kutengana unatukia sasa, wakati Mungu anamwita Bibi-arusi, naye shetani analiita kanisa.
Tunakupenda Wewe na Neno Lako, Bwana. Hatuwezi kupata ya kutosha. Tumeketi katika uwepo wa Neno lako kila siku, tukiivishwa, tukijitayarisha kwa ajili ya Kuja Kwako hivi karibuni. Baba, litakuwa limekaribia sana. Tunaweza kulihisi, Bwana. Tunasubiri kwa hamu kubwa.
Baba, jalia tuwe waaminifu vya kutosha na tuzifanye upya nadhiri zetu tena. Tunajua Imani yetu katika Neno lako inawaka mioyoni mwetu. Umeondoa mashaka yote. Hakuna kitu hapo ila Neno Lako. Tuna hakika, nasi hatuoni haya kuuambia ulimwengu, sisi ni Bibi-arusi Wako wa Kanda.
Ninataka kuualika ulimwengu kuja kusikiliza pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia Ujumbe: Kuonea Haya 65-0711.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Kanda:
Marko 8:34-38