24-0519 Maswali na Majibu #4

UJUMBE: 64-0830E Maswali na Majibu #4

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Familia ya Kanda,

Nakusudia ninyi, familia yangu, na familia kule ulimwenguni ambako tume—ambapo kanda zetu huenda.

Hao ni sisi, Familia ya Kanda ya nabii; watoto wake waliotawanyika ulimwenguni kote, wale aliomzalia Kristo. Wale ambao Baba amewapa Ufunuo Wake Mwenyewe katika siku hizi za mwisho.

Nataka kuwakusanya wote pamoja mojawapo wa siku hizi (ona?)—Baba atafanya hivyo, kisha tuta—tutakuwa na Makao na hatutazurura tena.

NATAKA KUWAKUSANYA WOTE PAMOJA. Hilo linatendeka sasa hivi. Ujumbe huu, Neno Lake, Kanda hizi zinatenda jambo hilo hasa: zinakusanya Bibi-arusi wote pamoja, zinatuunganisha kama KITENGO KIMOJA kutoka ulimwenguni kote. Hakuna kingine ila Sauti Yake; Sauti ya Mungu kwenye kanda, ndiyo inayoweza kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja.

Nanyi, mnapojazwa na Roho Mtakatifu, hapa kuna mojawapo ya ishara bora nizijuazo: unapendana sana na Kristo na kuamini kila Neno ambalo Yeye asema kuwa ni Kweli. Ona? Hiyo ndiyo ishara kuwa umempokea Roho Mtakatifu. Na maisha yako yamejawa na furaha, na—na lo, kila kitu ni tofauti (ona?) kuliko vile ilivyokuwa. Huyo ni Roho Mtakatifu.

Mioyo yetu, akili na roho zetu zimejawa furaha, upendo na Ufunuo, hatuwezi kabisa kujizuia. Kila ujumbe tunaousikia huleta Ufunuo zaidi. Tunaona sisi ni nani na yale tufanyayo ili kuwa katika Mapenzi yake Makamilifu. Hakuna kitu kinachoweza kutuondoa kutoka kwenye yale Mungu aliyoweka ndani ya mioyo yetu. Kubonyeza Play ndiyo Njia Iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku ya leo. Hakuna kubahatisha, hakuna kutumai, hakuna kumuuliza Roho Mtakatifu, “Je! hili nililotoka kusikia ni Neno la kweli?” “Je! Ninahitaji kulichunguza kwa Neno?”

Sio sisi. Yale Tunayosikia kwenye kanda NI NENO. Neno hilo tunalosikia kwenye kanda ndilo NENO PEKEE ambalo limethibitishwa na Roho Mtakatifu Mwenyewe, ile Nguzo ya Moto, kuwa Bwana Asema Hivi kwa Bibi-arusi.

Endapo mtu fulani akituambia, “Kuna mengi sana yaliyosemwa kwenye kanda ambayo yalikuwa tu ni Ndugu Branham akinena, si Neno lililotiwa mafuta. Huyo alikuwa mtu tu. Roho Mtakatifu ametuongoza kwenye yale ambayo ni Neno na yale yaliyokuwa tu ni Ndugu Branham akizungumza.”

Sio kwetu sisi. Sisi tunaamini tu yale nabii aliyotuambia tusisahau kamwe.

Nawatakeni msisahau kamwe hilo Neno. Yale aliyosema Musa, Mungu aliyaheshimu, kwa maana Neno la Mungu lilikuwa ndani ya Musa.

Hatutasahau kamwe yale nabii aliyosema, nasi Tunayaamini; kwa maana yamechorwa kwa kalamu ya chuma juu ya mioyo yetu. Yale aliyosema kwenye kanda, Mungu aliyaheshimu, nasi tunayaamini.

Hakuna heshima iliyo kubwa kuliko kuketi kuisikia Sauti ya Mungu ikinena nasi. Atakuwa akizungumza na Bibi-arusi Wake Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na kuyajibu maswali: 64-0830E Maswali Na Majibu #4. Ningependa kukualika kuungana nasi. Ni uamuzi ambao hautaujutia kamwe.

Ndugu. Joseph Branham