UJUMBE: 64-0830E Maswali na Majibu #4
- 26-0215 Maswali na Majibu #4
- 24-0519 Maswali na Majibu #4
- 22-1023 Maswali na Majibu #4
- 18-0225 Maswali na Majibu #4
Wapendwa Familia ya Kifalme,
Kuna mahali PAMOJA tu palipothibitishwa ambapo unaweza kwenda kumsikia Bwana akinena kupitia malaika Wake na kukuambia, “Daima Kumbukeni, ninyi ni watoto wa Mungu, Familia ya Kifalme wenye Damu ya Kifalme. Hakuna Damu bora zaidi duniani kuliko yenu. Ninyi ni watoto wangu, mmetawanyika kote ulimwenguni, ambao nimemzalia Kristo.”
Sisi ni Familia ya Mungu ya Kifalme wenye Damu ya Kifalme ikitiririka mishipani mwetu. Watoto aliomzalia Kristo kwa Sauti ya Mungu inenayo kupitia nabii Wake mwenye nguvu. Hakuna njia bora ya kulieleza kuliko hiyo, enyi marafiki.
Ndugu Branham, je, Bibi-arusi atahitaji kuhamia Jeffersonville au Arizona ili kuwa katika Unyakuo?
“Wawili watakuwa kitandani; nitamtwaa mmoja na kumwacha mmoja; na wawili watakuwa kondeni; nitamtwaa mmoja na kumwacha mmoja.” Ona? Kwa hivyo huenda wao…Kote ulimwenguni, hawatakusanyika mahali pamoja na kuwa na vitu shirika. Lakini makundi madogo yatakuwa yametawanyika kote duniani.
Kwa hivyo kimwili, hatutakuwa mahali pamoja kwa wakati mmoja. Bali utukufu kwa Mungu, Yeye alikuwa na mpango mkuu zaidi wa kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja.
Tunayaombea makanisa yote na makusanyiko ambayo yamekusanyika kuzunguka vile—vile—vile vipaza sauti vidogo nchini kote, kutoka kwenye taifa, kote kote hata kwenye Pwani ya Magharibi, kule juu kwenye milima ya Arizona, chini kwenye mabonde ya Texas, mbali sana hata Pwani ya Mashariki, nchini kote, Bwana, ambako wao wamekutanika. Tuko umbali wa masaa mengi, bali, Bwana, sisi tuko pamoja usiku wa leo kama jamii moja, waamini, tukingojea kuja kwa Masihi.
Leo, si tu kwamba Yeye anamkusanya Bibi-arusi Wake kutoka kote nchini, bali pia Yeye anatukusanya SISI kutoka mabara 7 ya dunia. Kuanzia Afrika hadi Antaktika. Amerika Kaskazini hadi Amerika Kusini, Asia, Australia na Ulaya. Yeye anamkusanya na kumuunganisha Bibi-arusi Wake kama JAMII MOJA ili kuisikia Sauti ya Mungu.
Yeye alituambia twende kanisani; hata pale wafundishapo nusu ya Neno, MPAKA tutakapolipata kanisa ambapo wanafundisha NENO LOTE. Mungu asifiwe Bibi-arusi Sasa yeye amepapata mahali hapo, ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye Kanda ndio NENO LOTE.
Iwe uko katika kanisa lako la Kanda la Nyumbani, kanisa lako ambamo familia nyingi zimekusanyika, au katika kibanda katika misitu ya Amazon au Afrika, popote unapoweza Kubonyeza Play kuisikia Sauti ya Mungu ikizungumza nawe mdomo kwa sikio, utakuwa u katika KANISA LA NENO LOTE.
Sisi tumelipata hilo kanisa la Neno lote nasi tunakualika uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) tunaposikia: Maswali na Majibu #4 64-0830E.
Ndugu Joseph Branham