UJUMBE: 64-0823M Maswali na Majibu #1
- 26-0125 Maswali na Majibu #1
- 24-0428 Maswali na Majibu #1
- 22-1002 Maswali na Majibu #1
- 18-0204 Maswali na Majibu #1
Mpendwa Maskani Ya Branham,
Salamu kwa Bibi-arusi wa Yesu Kristo waliopo kote ulimwenguni, wanaoamini Maskani ya Branham, Sauti ya Mungu, ndio kanisa lao la nyumbani ambapo wanalishwa kiroho kwa Mana iliyofichwa ambayo imehifadhiwa na kutunzwa kwa ajili ya Bibi-arusi wa Kristo.
Hiki ndicho kituo changu cha nyumbani; haya ndiyo makao yangu makuu; hapa ndipo tumeimarika. Sasa, shikilia hilo mawazoni haijalishi itakuwaje. Sasa, kama mna busara, mtashika jambo fulani. Haijalishi itakuwaje, haya ndiyo makao yetu makuu, papa hapa!
Waamini wengi wamekuwa wakielewa vibaya au kuweka wazo lao wenyewe au fasiri yao wenyewe kwenye kile nabii alichosema hapa, bali yeye anamwambia Bibi-arusi moja kwa moja, “kama mna busara, mtashika jambo fulani, haya ndiyo makao yetu makuu, papa hapa!”
Alimaanisha nini kwa jambo hilo?
Ndugu Branham alipokuwa hapa, wengi hawakumwelewa nao walidhani Bibi-arusi alipaswa kwenda Arizona na kumfuata yeye huko, ili waweze Kunyakuliwa. Ndugu Branham aliwajibu waziwazi: KAENI HAPA, HAPA NDIPO MAHALI PENYEWE.
Kundi kubwa mno lao waliondoka hivyo, nao walitaka kuenda hivi na kufanya yale baada ya mimi kuwaambia wakae pale. Kaeni pale, kaeni papa hapa; hapa ndipo mahali panapofaa.
Watu waliondoka kutoka kila mahali kote Marekani kwenda Arizona, lakini yeye aliwaambia waziwazi: Kaeni papa hapa, hapa ndipo mahali penyewe!
Kaeni Jeffersonville? Hivyo ndivyo yeye alivyosema!
Ufunuo wangu ni kwamba, ilikuwa ni Mungu, akizungumza kupitia nabii Wake na kuwaambia watu, “KAENI NA KANDA.” Hapo ndipo MAHALI PENYEWE!
Alikasirika mno na akasema ilibidi afanye jambo fulani kuhusu watu hao wote. Yamlazimu afanye nini? Angewapeleka kwenye kanisa gani? Wao wanapaswa waende wapi? Ndugu Branham alisema inamlazimu afanye nini?
Kwa hivyo sasa, yanipasa kuwarudisha hao watoto hapa wapate kula. Wako chini kule jangwani wakiumia kwa njaa.
Yeye hakusema ati wangehitaji kwenda kwenye kanisa la mahali na kupata vipande vidogo ambavyo wangeweza kula. Yeye alisema lazima AWARUDISHE HAPA wapate kula, la sivyo WANGEKUFA KWA NJAA.
UFUNUO WANGU, Enyi MARAFIKI.
Sasa, msimwelewe vibaya kwa mara nyingine tena, au kusema kitu fulani ambacho hakusema, kwa kusema, “Ndugu Branham alitaka kila mwamini ahamie Jeffersonville ili kuwa Bibi-arusi.” Ndugu Branham aliwajua watu hao wote, na KILA mwamini kutoka kote ulimwenguni, hawangeweza kuhamia na kuishi Jeffersonville. Hilo lisingewezekana. Kwa hivyo yeye alimaanisha nini? Yeye alikuwa ANAMUUNGANISHA Bibi-arusi wa Kristo kwenye KANDA ambazo zilikuwa zimerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi kuzila.
Ujumbe huu, Sauti Hii, ndilo Neno la Mungu Lililonenwa kwa ajili ya siku hii nalo Litamuunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi wa Yesu Kristo.
Mzoga ni kile anachokula tai. Sasa, tai huhesabiwa katika Biblia, nabii. Nabii ni tai. Mungu—Mungu hujiita Mwenyewe Tai, nasi tu “wana tai” basi, wa—waamini. Mwaona? Na mzoga waulao ni nini? Ni Neno. Po pote lilipo Neno, tabia halisi ya ndege itajidhihirisha yenyewe.
Liko wapi Neno la Bwana lililo safi, lililothibitishwa, lisilo na mkanganyiko, Bwana Asema Hivi kwa ajili ya siku hii? Kuna mahali pamoja tu, kwenye Kanda.
Ningeweza kuendelea na kuendelea, nukuu kwa nukuu, lakini Ujumbe huu na kile Ndugu Branham alichosema kinahitaji Ufunuo kutoka kwa Mungu. Yatupasa kusoma katikati ya mistari kwa ufunuo, bali tuseme kile yeye alichosema. Kwa maana ni NENO SAFI.
Maswali na Majibu ya leo na kile MIMI NINACHOAMINI.
Leo, wahudumu wengi wanawaambia watu kwamba kwa sisi kuwa na Kanisa La Kanda La Nyumbani tumetoka nje ya Neno na kile Ndugu Branham alichosema tufanye. Wao wanahisi ni lazima tuende kwenye kile wanachokiita na kukichukulia kanisa.
Kuna nukuu nyingi, nyingi sana kiukweli ambapo Ndugu Branham analisema hili waziwazi.
Sasa, ninyi endeni kwa kanisa fulani nzuri la Injili Nzima mpate kanisa la nyumbani.
Nami naliamini hilo kwa moyo wangu wote, kwa sababu yeye alisema hivyo. Lakini naamini sisi tunafanya hivyo kwa KUWA NA KANISA LA KANDA LA NYUMBANI. Mahali petu si ndipo palipo muhimu kwa Bwana. Hilo ni jengo tu. Lakini wajibu wetu kwa Bwana ni kukaa na Neno Lake, SIO MAHALI AU JENGO. Mahali hapo hapamwokoi na kumkamilisha Bibi-arusi, NENO NDILO.
Kama nikienda kwenye jengo la kanisa, lakini wao wamesahau JAMBO LILILO KUU: kuisikia Sauti ya Mungu kwa Kubonyeza Play, nao wameibadilisha hiyo kwa kuwasikia wahudumu TU wakiuhubiri Ujumbe, Je, hilo litairidhisha na kuilisha nafsi yako kabisa? Huenda hilo likairidhisha nafsi yako, ndugu na dada yangu, bali hilo halitamridhisha Bibi-arusi.
Hebu niingilie kati hapa na niseme kuna maelfu ya watu ambao hawana jengo la kanisa la kwenda. Je, wamepotea? Ikiwa hawana mchungaji au kanisa, Je, hiyo ina maana kwamba hawawezi kuwa Bibi-arusi? Ikiwa unaishi ndani ya maili 100 kutoka kwenye jengo la kanisa, Je, ni lazima uende kwenye kanisa hilo? Lakini ikiwa ninaishi mbali zaidi, si lazima? Nalazimika kumsikiliza Mhubiri hewani, lakini siwezi kusikiliza kanda hewani? Je, jengo la kawaida ndilo ambalo nabii anasema ndilo jambo lililo muhimu zaidi tunalopaswa kwenda?
Nabii alitaka kumleta Bibi-arusi wapi?
Kama hamwezi kuja hapa maskanini, tafuteni kanisa fulani mahali fulani; enendeni kwalo.
Kwa mara nyingine tena, liko wapi chaguo lake la kwanza la kuwapeleka watu? Kwenye Maskani ya Branham, Neno, kanda. Hilo ndilo Mungu amempa Bibi-arusi Wake kufanya katika wakati huu wa mwisho, nasi tunafanya hivyo kila siku NA kila Jumapili.
Msinielewe vibaya. MIMI SISEMI lazima usikilize kanda hewani pamoja na Maskani ya Branham ili uwe Bibi-arusi. SISEMI hupaswi kwenda kanisani. SISEMI huwezi kuwasikiliza wahudumu. Ikiwa unaamini hivyo, uko nje ya Neno. Ninasema kuisikia Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio Sauti iliyo muhimu zaidi UNAYOPASWA KUISIKIA, na ninaamini kwamba kila mchungaji anapaswa kuicheza Sauti hiyo, Kanda, katika makanisa yao. Lakini wao wametoa kila namna ya udhuru uliopo ILI KUTOZICHEZA KANDA. Ikiwa hilo ndilo kanisa lako, wewe huli Neno.
Hili ni wazi jambo ambalo yeye hakutaka litokee na ndicho ambacho watu walichokuwa wakifanya.
Nanyi nendeni kanisani; msiketi nyumbani, kuenda kuvua samaki, na kuwinda, na mambo kama hayo mnamo Jumapili.
Sisi hatufanyi hivyo. Sisi tunaungana kwenye kitu pekee kitakachomuunganisha Bibi-arusi, Ujumbe huu, Sauti hii.
Kwa mara nyingine tena, Mimi ninaamini katika kwenda kanisani. Kuna makanisa mengi ulimwenguni kote ambayo yanaziweka kanda nafasi ya kwanza kwenye mimbara zao, Bwana asifiwe. Je, ninaamini lazima ukae nyumbani la sivyo wewe si Bibi-arusi? LA, LA, LA….Sijawahi kuliwazia, sijawahi kuliamini. Nataka tu UBONYEZE PLAY bila kujali uko wapi au unaenda kwenye kanisa gani.
Kama huna Ufunuo wa kile anachosema, basi unaweza kusema waziwazi, “Sihitaji kumsikiliza Ndugu Branham au hata kulazimika KUKUBALIANA na yote asemayo. Hata hivyo alisema, kuna watu wengine wengi walioitwa na Mungu.”
Endelea. Twaona hapa lasema, “Yatupasa kuhuduria kanisa lingine lisilokubaliana nawe?” Hakika, si…Mimi siye changarawe pekee pwani, mwajua. Kuna—kuna watu wengine wacha Mungu kila mahali; natumai mimi ni mmojawao.
Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio JIWE LA UFUKWENI LANGU, MWAMBA WANGU. Ndio Sauti ninayotaka Mimi kuisikia na ndio Sauti ninayotaka Maskani ya Branham waisikie.
Kama mngependa kuungana nasi, mnakaribishwa mno, ndugu na dada zangu. ungeneni nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikinena na kuyajibu maswali mengi unayoweza kuwa nayo moyoni mwako. Na usikie mwenyewe ikiwa mambo niliyoyasema katika barua hii hayako sawa na Neno na nimeelewa vibaya kile Mungu anachomwambia Bibi-arusi Wake.
Kile yeye anachosema kwenye kanda ni Bwana Asema Hivi. Si kile mimi Ninachosema anasema, au kile Ninachoamini anasema, na Mungu PEKE YAKE ndiye anayeweza kukupa Ufunuo wa kweli.
Ndugu Joseph Branham