UJUMBE: 63-0818 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 25-0928 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 23-1126 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 22-0515 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 19-0811 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 17-0702 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
- 15-0909 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake
Mpendwa Bibi-arusi Aliyeungana,
Nimechangamshwa sana, na niko chini ya matarajio makubwa ya aina yake, kuwa sehemu ya yote Mungu anayofanya katika siku yetu. Mawazo ya Mungu ya huko mwanzo sasa yanatimizwa mbele ya macho yetu, na sisi tu sehemu ya hilo.
Kote katika Biblia, manabii walitabiri na kunena yale ambayo yangetukia. Wakati fulani unabii huo haukutimia kwa mamia ya miaka baadaye, lakini wakati utimilifu wa wakati ulipowadia, ulitimia; kwa maana mawazo ya Mungu yaliyonenwa kwa kinywa cha nabii Wake LAZIMA yatimie.
Nabii Isaya alisema, “Bikira atachukua mimba”. Kila familia ya Kiebrania ilimtayarisha binti yao mdogo kumpata mtoto huyu. Walinunua viatu na vibuti, na nguo ndogo za kichanga, nao wakajitayarisha kwa ajili ya mtoto huyo kuwasili. Vizazi vilipita, lakini hatimaye Neno la Mungu lilitimia.
Nilipokuwa mvulana mdogo nilishangaa daima, Bwana, naona katika Neno Lako kwamba Wewe daima umewaunganisha watu Wako pamoja ili kulitimiza Neno Lako. Uliwaunganisha watoto Wako wa Kiebrania kupitia mtu mmoja, Musa, ambaye aliwaongoza kwa Nguzo ya Moto kwenda Nchi ya Ahadi.
Ulipofanyika mwili na kukaa hapa duniani, Wewe uliwaunganisha wanafunzi Wako. Uliwatenga na kila kitu na kila mtu ili uwafunulie Neno Lako. Siku ya Pentekoste, kwa mara nyingine tena ulilikusanya Kanisa Lako mahali pamoja, kwa nia moja kwa umoja kabla hujaja na kuwapa Roho Wako Mtakatifu.
Nikawaza, hilo litawezekanaje leo Bwana? Bibi-arusi Wako ametawanyika kote ulimwenguni. Je! Bibi-arusi wote watakuja Jeffersonville? Sijaona hilo likitendeka Bwana. Lakini BWANA, Wewe kamwe haubadilishi mpango Wako. Ni Sheria Yako, hakuna njia ya kulizuia hilo. Utalifanyaje?
UTUKUFU…LEO, tunaweza kuona kwa macho yetu wenyewe, na muhimu zaidi, KUWA SEHEMU YAKE: Neno la Milele la Mungu likitimizwa. HATUKO KIMWILI mahali pamoja, tumetawanyika ulimwenguni kote, lakini Roho Mtakatifu SASA AMEMUUNGANISHA BIBI-ARUSI WAKE KWA SAUTI YA MUNGU. NENO LAKE LILILONENWA NA KUREKODIWA KWENYE KANDA, Yakini ya Mungu ya siku hii, inamkusanya na KUMUUNGANISHA BIBI-ARUSI WAKE… NA HAKUNA LOLOTE LINALOWEZA KULIZUIA HILO.
Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake. Anakusanyika pamoja, kutoka Mashariki na Magharibi, na Kaskazini na Kusini. Kuna wakati wa kuungana, na huo unaendelea sasa hivi. Anaungana kwa sababu gani? Unyakuo. Amina!
Wakati wa kuungana unafanyika SASA HIVI!!! Ni kitu gani kinachotuunganisha? Roho Mtakatifu kwa Neno Lake, Sauti Yake. Tunaungana kwa sababu gani? UNYAKUO!!! Nasi tunakwenda sote na hatuachi hata MMOJA nyuma.
Mungu anamtayarisha. Naam bwana, kuungana! Anaungana na kitu gani? Na Neno!
Neno la siku yetu ni lipi? UJUMBE Huu, SAUTI YAKE, Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake. Sio mtu. Sio watu. Sio kundi. Ni SAUTI ya Mungu iliyo kwenye kanda Iliyothibitishwa, kwa Nguzo ya Moto.
“Kwa maana mbingu zote na nchi zitapita, bali Neno Langu halitapita kamwe.” Anajiunganisha Mwenyewe na BWANA ASEMA HIVI haidhuru madhehebu yoyote ama mtu yeyote mwingine anasema nini.
Haidhuru MTU YEYOTE anasema nini, sisi tunajiunganisha na Sauti ya Bwana Asema Hivi iliyohakikishwa, iliyothibitishwa ya siku yetu. Sio fasiri ya mtu fulani; kwa nini tufanye hivyo? Hiyo hubadilika kwa kila mtu, lakini Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda HAIBADILIKI KAMWE nayo Imetangazwa na Nguzo ya Moto Yenyewe kuwa Neno la Mungu na Sauti ya Mungu.
Shida yake ni kwamba, kwa binadamu, yeye hamjui kiongozi wake. Naam, bwana. Watakusanyika chini ya dhehebu fulani, watakusanyika chini ya askofu ama mtu fulani, bali hawatakusanyika chini ya yule Kiongozi, Roho Mtakatifu katika Neno. Unaona? Wao wanasema, “Loo, vema, nahofu nitakuwa kidogo mshupavu wa dini; ninahofu nitaelekea kubaya.” Loooo, haya basi!
Hapa ndipo wakosoaji wanapoelekezea makutano yao na kusema, “Ona, wanamwinua mtu, Ndugu Branham. Wao ni waabudu mungu-mtu nao wanakusanyika chini yake, mtu huyo, si Roho Mtakatifu.”
Upuuzi, sisi tunaungana chini ya SAUTI YA MUNGU ILIYOTHIBITISHWA ILIYONENWA KUPITIA MTU HUYO. Kumbukeni, huyo ndiye mtu ambaye Mungu alimchagua kuwa Sauti Yake kumwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake katika siku hii. Hiyo ndiyo Sauti PEKEE iliyothibitishwa na Mungu Mwenyewe. Lakini kinyume chake, WAO wanaungana chini ya WANADAMU. HAWATA icheza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda katika makanisa yao. Unaweza kuliwazia hilo??? Mhudumu anayedai kuuamini Ujumbe huu kuwa ndio Ujumbe wa wakati huu, Bwana Asema hivi, lakini anatafuta aina fulani ya kisingizio cha KUTO icheza Sauti hiyo makanisani mwao, bali kuwahudumia watu LAZIMA wawasikilize wao na wahudumu wengine wakihubiri Neno… kisha wao wanasema ati sisi tunamfuata mtu!!!
Tumetoka kusikia jumapili iliyopita kile Mungu alichowafanya watu hao!!
Tunajiandaa kufanya Harusi. Tunafanyika Mmoja na Yeye. Neno linakuwa wewe, na wewe unakuwa Neno. Yesu alisema, “Katika siku ile mtaijua. Yote aliyo Baba, ndivyo nilivyo Mimi; na yote niliyo Mimi, ndivyo mlivyo ninyi; na yote mliyo ninyi, ndivyo nilivyo Mimi. Katika siku hiyo mtajua ya kwamba Mimi niko ndani ya Baba Yangu, Baba ndani Yangu, Mimi ndani yenu, nanyi ndani Yangu.”
Asante Bwana kwa Ufunuo wa Wewe Mwenyewe, na wa sisi wenyewe, katika siku yetu. Bibi-arusi Wako anajiweka mwenyewe tayari kwa Neno Lako Lililonenwa. Tunajua tuko katika Mapenzi Yako makamilifu kwa sisi kukaa na Neno Lako lililorekodiwa.
Ninaualika ulimwengu kuisikiliza Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa ya siku yetu Jumapili hii. Mnakaribishwa muungane nasi Jumapili saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia: 63-0818, Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake. Ikiwa hamuwezi kujiunganisha kwa simu na kusikiliza pamoja nasi, chagueni kanda, KANDA YOYOTE; zote ni Bwana Asema Hivi, na msikilize Neno la Mungu liwakamilishe na kuwafanya tayari kwa ajili ya ujio Wake uliyokaribu.
Ndugu. Joseph Branham
Zaburi 86:1-11
Mathayo 16:1-3
Anajiunganisha Mwenyewe. Anajitayarisha. Kwa nini? Yeye ni Bibi-arusi. Hiyo ni kweli. Naye amejiunganisha pamoja na Bwana Arusi Wake, unaona, na Bwana Arusi ni Neno. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu.”