UJUMBE: 60-1211E Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 24-1208 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 23-0618 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 20-1227 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 19-0310 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 16-0410 Wakati wa Kanisa La Laodikia
Wapendwa Wateule,
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja Nami.
Enyi wahudumu, mfungulieni milango yenu malaika wa Mungu kabla hamjachelewa. Irudisheni Sauti ya Mungu kwenye mimbara zenu kwa kuzicheza kanda. Ndiyo Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa kwa ajili ya siku yetu yenye Maneno ya kutokosea. Ndiyo Sauti pekee yenye Bwana Asema Hivi. Ndiyo Sauti pekee ambayo Bibi-arusi wote wanaweza kusema AMINA kwake.
Huu ndio wakati mkuu wa nyakati zote. Yesu anatupa sifa Yake kwa vile siku za neema Yake zinakwisha. Wakati umefika mwisho. Ametufunulia tabia Zake hasa katika wakati huu wa mwisho. Yeye ametupa mtazamo mmoja wa mwisho wa Uungu Wake mkuu wa neema. Wakati huu ni ufunuo wa jiwe la kifuniko wa nafsi Yake.
Mungu alikuja katika wakati huu wa Laodikia na kunena kupitia mwili wa mwanadamu. Sauti Yake imerekodiwa na kuhifadhiwa ili kumwongoza na kumkamilisha Bibi-arusi Neno Wake. Hakuna kabisa Sauti nyingine inayoweza kumkamilisha Bibi-arusi Wake ila Sauti Yake Mwenyewe.
Katika wakati huu wa mwisho, Sauti Yake iliyo kwenye kanda imewekwa kando; imetolewa nje ya makanisa. Hawataki tu kabisa kuzicheza kanda. Kwa hiyo Mungu anasema, “Mimi niko kinyume nanyi nyote. Nitawatapika mtoke katika kinywa Changu. Huu ni mwisho.”
“Kwa kuwa saba kati ya nyakati saba, sijaona kitu ila watu wakiliheshimu neno lao wenyewe kuliko Langu. Kwa hiyo mwishoni mwa wakati huu ninawatapika mtoke katika kinywa Changu. Yote yamekwisha. Nitazungumza basi. Naam, niko hapa katikati ya Kanisa. Amina wa Mungu, aliye mwaminifu na wa kweli atajifunua Mwenyewe na itakuwa KWA NJIA YA NABII WANGU.”
Kama ilivyokuwa hapo awali, wao wanafanya vile vile walivyofanya baba zao katika siku za Ahabu. Kulikuwa na jumla yao mia nne na wote walikubaliana; na wote wakisema jambo lile lile, waliwadanganya watu. Lakini nabii MMOJA, MMOJA TU, alikuwa sahihi na hao wengine wote walikuwa makosani kwa sababu Mungu alikuwa ametoa ufunuo kwa MMOJA TU.
Hii si kusema kwamba huduma zote ni za uongo na zinawadanganya watu. Wala Mimi sisemi mtu mwenye wito wa kuhudumu hawezi kuhubiri au kufundisha. Ninasema huduma tano ya KWELI itaweka KANDA, Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi, kuwa ndio Sauti iliyo muhimu sana UNAYOPASWA KUISIKIA. Sauti iliyo kwenye kanda ndio Sauti PEKEE ambayo imethibitishwa na Mungu Mwenyewe kuwa Bwana Asema Hivi.
Jihadharini na manabii wa uongo, kwa maana wao ni mbwa mwitu wakali.
Utajuaje kwa hakika njia sahihi kwa ajili ya siku hii? Kuna mgawanyiko jinsi hii miongoni mwa waaminio. Kundi moja la watu linasema huduma tano itamkamilisha Bibi-arusi, huku jingine linasema Bonyeza Play tu. Hatupaswi kugawanyika; tunapaswa kuungana kama BIBI-ARUSI MMOJA. Jibu sahihi ni lipi?
Hebu na tuifungue mioyo yetu pamoja na tusikie kile Mungu anachosema kwa Bibi-arusi kupitia nabii Wake. Kwa maana sote tunakubali, Ndugu Branham ndiye malaika-mjumbe Wake wa saba.
Juu ya msingi wa tabia za wanadamu peke yake, mtu ye yote anajua ya kwamba palipo na watu wengi kuna hata na maoni yasiyopatana juu ya mambo madogo-madogo ya fundisho muhimu ambalo wote wanashikilia pamoja. Ni nani basi atakayekuwa na mamlaka ya kutokosea ambayo itarudishwa katika wakati huu wa mwisho, kwa kuwa wakati huu wa mwisho utarudi kwenye kumdhihirisha Bibi-arusi wa Neno Halisi? Hiyo inamaanisha tutakuwa na Neno tena kama lilivyotolewa kikamilifu, na kueleweka kikamilifu katika siku za Paulo. Nitakwambia ni nani atakayekuwa nalo. Itakuwa ni nabii aliyethibitishwa kinaganaga, ama hata aliyethibitishwa kinaganaga zaidi kuliko nabii ye yote katika nyakati zote tangu Henoko hata siku hii, kwa sababu mtu huyu itambidi kuwa na huduma ya kinabii ya jiwe la kifuniko, na Mungu atamtambulisha. Haitambidi kujitetea, Mungu atamtetea kwa sauti ya ishara. Amina.
Hivyo, Ujumbe huu ulionenwa na mjumbe Wake ulitolewa kikamilifu, na unaeleweka kikamilifu.
Ni kitu gani kingine ambacho Mungu alichosema kumhusu malaika-mjumbe Wake wa saba na Ujumbe wake?
- . Yeye atasikia tu kutoka kwa Mungu.
- . Atakuwa na “Bwana asema hivi” na kunena kwa niaba ya Mungu.
- . Yeye atakuwa kinywa cha Mungu.
- . YEYE, KAMA INAVYOTANGAZWA KATIKA MALAKI 4:6, ATAIGEUZA MIOYO WA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO.
- . Ata warudisha wateule wa siku za mwisho nao watamsikiliza nabii aliyethibitishwa akitoa kweli halisi kama vile ilivyokuwa kwa Paulo.
- . Ata irudisha kweli kama walivyokuwa nayo.
Na kisha Yeye alisema nini kutuhusu sisi?
Na hao wateule walio pamoja naye katika siku hiyo watakuwa ndio wanaomdhihirisha Bwana kwa kweli na watakuwa ndio Mwili Wake na kuwa sauti Yake na kutenda kazi Zake. Haleluya! Unaliona hilo?
Kama ungali una mashaka yo yote juu ya jambo hili mwombe Mungu kwa Roho Wake akujaze na kukuongoza, kwa kuwa Neno linasema, “KWA MAANA WALIO WATEULE HAWAWEZI KUPUMBAZWA”. Hakuna mtu anayeweza kukupumbaza kama wewe ni Bibi-arusi.
Wakati Wamethodisti waliposhindwa, Mungu aliwainua wengine na kwa hiyo jambo hilo limeendelea kwa miaka mingi mpaka katika wakati huu wa mwisho kuna watu wengine nchini, ambao chini ya mjumbe wao watakuwa ndio sauti ya mwisho kwa wakati wa mwisho.
Naam bwana. Kanisa si “kinywa” cha Mungu tena. Ni kinywa chake lenyewe. Kwa hiyo Mungu analiacha. Ataliangamiza kupitia kwa nabii na bibi-arusi, kwa kuwa sauti ya Mungu itakuwa ndani ya bibi-arusi. Naam iko, kwa maana inasema katika sura ya mwisho ya Ufu. aya ya 17 “Roho na bibi-arusi wasema, njoo.” Mara nyingine tena ulimwengu utasikia moja kwa moja kutoka kwa Mungu kama ilivyokuwa wakati wa Pentekoste; lakini bila shaka huyo Bibi-arusi Neno atakataliwa kama ilivyokuwa katika wakati wa kwanza.
Bibi-arusi anayo sauti, bali itasema tu kile kilicho kwenye kanda. Kwa maana Sauti hiyo INATOKA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU, hivyo haihitaji kufasiriwa kwa vile ilivyotolewa kikamilifu na inaeleweka kikamilifu.
Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti hiyo ikitufunulia: Wakati wa Kanisa la Laodikia 60-1211E.
Ndugu. Joseph Branham