24-1201 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

UJUMBE: 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

PDF

BranhamTabernacle.org

Habari Za Asubuhi Marafiki,

Haijawahi kutokea katika historia ya ulimwengu kuwepo na wakati ambapo Bibi-arusi wa Kristo kutoka ulimwenguni kote angeweza kuungana pamoja katika nia moja, wakati sauti kutoka Mbinguni, ile Sauti halisi ya Mungu, ingeweza kuja ikienda kasi.

Maandiko yanatimia. Ni ishara ya Mbegu ya wakati wa kuungana. Ule muungano usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo unafanyika tukiketi katika uwepo wa Mwana, tukiivishwa, tukijiweka wenyewe tayari kwa kuisikia Sauti ya Mungu halisi.

Sisi tunakamilishwa na huduma tano Yake.

Ni wangapi wanaoamini kwamba karama na miito havina majuto? Biblia ilisema kuna karama tano katika kanisa. Mungu ameweka katika kanisa Mitume, au wamishenari, mitume, manabii, waalimu, wainjilisti, wachungaji.

  • . Mhubiri: Ningeenda barabarani. Mtu fulani angesema, “Je, wewe ni mhubiri?” Ningesema, “Ndiyo bwana. Loo, Ndiyo, mimi ni mhubiri.”
  • . Mwalimu: Na sasa sababu sikuchukua kuhubiri asubuhi ya leo, ilikuwa ni kwamba, nilifikiri, katika kufundisha, tungelielewa vizuri zaidi kuliko kuchukua somo na kulipitia juu juu. Tungelifundisha tu.
  • . Mtume: Neno “mmishenari” linamaanisha “mtu aliyetumwa.” “Mtume” maana yake ni “mtu aliyetumwa.” Mmishenari ni mtume. Mimi—mimi, mimi ni mmishenari, kama mjuavyo, ninafanya uinjilisti, kazi ya kimishenari, karibu mara saba nchi za ng’ambo, kote ulimwenguni.
  • . Nabii: Je, unaniamini mimi kuwa nabii wa Mungu? Basi nenda ukafanye kile ninachokuambia.
  • . Mchungaji: Je, mumeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mumeniita “mchungaji wenu”; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

Nami nikawaona hao mamilioni wamesimama pale, nikasema, “Hivi hawa wote ni wa Branham?” Kasema, “La.” Kasema, “Hao ni waongofu wako.” Ndipo nikasema, ni—nikasema, “Ninataka kumwona Yesu.” Akasema, “Bado. Itachukua muda kabla Yeye hajaja. Ila atakuja kwako kwanza nawe utahukumiwa kwa Neno ambalo ulihubiri,

Ndipo sisi sote tutainua mikono yetu na kusema, “Tunatumainia hilo!”

Jambo fulani liko karibu kutukia. Nini kinatendeka? Waliokufa katika Kristo wameanza kufufuka pande zote kunizunguka. Ninahisi badiliko likija mwilini mwangu. Nywele zangu za mvi, zimeondoka. Angalia uso wangu… makunyanzi yangu yote yametoweka. Kuugua kwangu na maumivu…. YAMEKWISHA. Kuhisi kwangu huzuni kumetoweka mara moja. Nimebadilishwa kwa dakika moja, katika kufumba na kufumbua jicho.

Kisha tutaanza kutazama kando yetu na kuwaona wapendwa wetu. Loo, yule pale Mama na Baba…Utukufu, mwanangu…binti yangu. Babu, Bibi, loo, nimewakumbuka sana nyote wawili. Halo …yule pale rafiki yangu wa zamani. LOO, TAZAMA, ni Ndugu Branham, nabii wetu, Haleluya!! yuko hapa. Linatukia!

Kisha pamoja, wote kwa pamoja, tutanyakuliwa huko juu mahali fulani hewani ng’ambo ya nchi. Tutamlaki Bwana wakati akishuka. Tutasimama huko pamoja Naye juu ya mizingo ya dunia hii na kuziimba nyimbo za ukombozi. Tutaimba na kumsifu Yeye kwa ajili ya neema Yake ya ukombozi ambayo ametupa.

Ni mangapi yote yanayomngojea Bibi-arusi Wake. Tutakuwa na wakati ulioje katika umilele sisi kwa sisi, na pamoja na Bwana wetu Yesu. Maneno ya kibinadamu hayawezi kueleza, Bwana, jinsi tunavyojisikia mioyoni mwetu.

Kama ungependa kumsikia Yeye akikuita Bibi-arusi Wake, na kukuambia jinsi gani itakavyokuwa pamoja Naye, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki), nawe utabarikiwa kupita kipimo.

Ndugu. Joseph Branham

60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini na Nne Elfu