24-0922 Edeni Ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni Ya Shetani

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa sifa ya Mungu,

Sisi ndio sifa halisi ya Baba yetu wa Mbinguni; kwa maana tulikuwa ndani yake hapo mwanzo. Hatukumbuki hilo sasa, lakini tulikuwa pamoja Naye, na Yeye alitujua. Alitupenda sana hata akatufanya kuwa mwili, ili aweze kuwasiliana nasi, kuzungumza nasi, kutupenda, hata kutushika mikono.

Lakini Shetani alikuja na kupotosha Neno la asili la Mungu, Ufalme Wake, na mpango Wake kwa ajili yetu. Aliwapotosha wanaume na wanawake na kufanikiwa katika kupotosha na kuuteka ulimwengu huu tunaoishi. Ameufanya ulimwengu kuwa ufalme wake, bustani yake ya Edeni.

Ni saa danganyifu na yenye hila iliyowahi kuwako. Ibilisi ameweka kila mtego wa ujunja awezao; maana yeye ni mdanganyifu mkuu. Mkristo hana budi kuwa mwangalifu zaidi leo kuliko alivyowahi kuwa katika wakati wowote.

Lakini wakati huohuo, ndio wakati uliyo mzuri zaidi ya nyakati zote, kwa sababu tunaelekea kwenye ule Utawala wa Miaka Elfu mkuu. Bustani yetu ya Edeni inakuja hivi karibuni, ambamo tutakuwa na upendo mkamilifu na ufahamu mkamilifu wa upendo wa Mungu. Tutakuwa hai na salama pamoja Naye katika Edeni yetu Milele yote.

Yesu alituambia katika Mathayo 24 tunapaswa kuwa waangalifu jinsi gani katika siku hii. Alituonya kwamba ingekuwa ni siku ya udanganyifu sana iliyowahi kuwepo, “inafanana sana hata ingewadanganya wale Walioteuliwa na Mungu kama yamkini”; kwa kuwa ujanja wa Ibilisi utawafanya watu waamini ya kwamba wao ni Wakristo, wakati wao sio.

Lakini wakati huu pia ungemtoa Bibi-arusi Neno safi wake ambaye hangedanganyika na asingeweza kudanganywa; kwa maana wangedumu na Neno Lake la asili.

Kama Yoshua na Kalebu, Nchi yetu ya ahadi imeanza kuonekana kama vile yao ilivyoanza kuonekana. Nabii wetu alisema Yoshua maana yake ni, “Yehova-Mwokozi”. Alimwakilisha kiongozi wa wakati wa mwisho ambaye atakuja kwa kanisa, kama vile Paulo alivyokuja kama kiongozi wa kwanza.

Kalebu aliwakilisha wale waliomtii Yoshua. Kama vile wana wa Israeli, Mungu alikuwa amewaanzisha kama bikira kwa Neno Lake; bali wao walitaka kitu tofauti. Nabii wetu alisema, “vivyo hivyo na kanisa hili la siku za mwisho nalo.” Kwa hiyo, Mungu hakuwaacha Waisraeli waingie katika nchi ya ahadi mpaka wakati Wake Mwenyewe uliokusudiwa ulipowadia.

Watu walimsonga Yoshua, kiongozi wao waliyepewa na Mungu, na kusema, “Hiyo nchi ni yetu, hebu na twende tukaitwae. Yoshua, umeshindwa, lazima umepoteza agizo lako. Huna ile nguvu uliyokuwa nayo. Ulikuwa ukisikia kutoka kwa Mungu na kujua mapenzi ya Mungu, na kutenda kwa haraka. Una kasoro fulani wewe.”

Yoshua alikuwa nabii aliyetumwa na Mungu, naye alijua ahadi za Mungu. Nabii wetu alituambia:

“Mungu aliuweka uongozi mzima katika mikono ya Yoshua kwa sababu alikuwa amedumu na Neno. Mungu aliweza kumwamini Yoshua lakini si hao wengine. Kwa hiyo itajirudia katika siku hizi za mwisho. Shida ile ile, usumbufu ule ule.”

Kama vile Mungu alivyofanya na Yoshua, Yeye aliuweka UONGOZI MZIMA mikononi mwa malaika-nabii Wake, William Marrion Branham; kwa maana alijua angeweza kumwamini yeye, lakini si hao wengine. Ilibidi kuwe na Sauti Moja, Kiongozi Mmoja, Neno Moja la mwisho, wakati huo, na SASA HVI.

Ninapenda jinsi nabii alivyotuambia kutakuwa na maelfu mara maelfu ambao watakaozisikia kanda. Alisema kuwa hizo kanda NI HUDUMA. Kutakuwa na baadhi yetu tutakaoingia kwa siri Majumbani na makanisani tukiwa na kanda (huduma yake) ili kuupata Uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu awali.

Tuliporudi na kusema, Bwana, tumetii maagizo yako, nako kulikuwa na watu tuliowapata tulipozicheza kanda walioamini. Sasa tumehubiri jambo hilo, kote ulimwenguni, Je, utatimiza hilo?

Yeye atasema: “Hilo ndilo Mimi nililowatuma kufanya.”

Mungu atalitimiza hilo. Nyumba yako kamwe haitaporomoka. Wakati Mungu atakapotoa ishara ya kukiangamiza kitu hicho chote, familia yako yote, mali zako zote, zitakuwa salama nyumbani mwako. Unaweza kusimama humo. Haikulazimu kuchungulia dirishani, wewe Bonyeza Play tu huku vita vikiendelea.

Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.

Ninakualika uje uungane nasi wakati tunapokula huduma kuu ya Mungu, hai, ya wakati wa mwisho, Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 Jioni ya Afrika mashariki) tunaposikia yote yanayohusu: Edeni ya Shetani 65-0829.

Hebu tuishi mpaka kuja Kwake Bwana kama ikiwezekana. Hebu na tutende kila kitu kilicho katika uwezo wetu kwa upendo, na uelewano—kuelewa kwamba Mungu anauchunguza ulimwengu, siku hii ya leo, kutafuta kila kondoo aliyepotea. Hebu tuzungumze nao kwa maombi ya upendo yaliyokolea chumvi na Neno la Mungu, ili tuweze kumpata huyo wa mwisho kusudi tupate kwenda nyumbani, na tutoke katika Edeni hii ya kale ya Shetani hapa, Bwana.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

2 Timotheo 3:1-9
Ufunuo 3:14
2 Wathesalonike 2:1-4
Isaya 14:12-14
Mathayo 24:24