24-0512 Maswali na Majibu #3

UJUMBE: 64-0830M Maswali na Majibu #3

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Bikira Safi,

Jinsi gani ninavyopenda kuwahimiza kila wiki Kubonyeza Play na kuisikia Sauti ya Mungu ya siku yetu. Kwa maana najua ndio Mpango mkamilifu wa Mungu kwa ajili ya siku yetu.

Si yale Joseph Branham anayosema au kuamini. Ni yale Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ilichotuambia:

Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.

Ikiwa mna ufunuo wowote wa Ujumbe huu hata kidogo, nukuu hiyo ndogo inapaswa kutosha sana kwenu kumwambia kila mtu mnayekutana naye; kila mwaminio, kuyaambia makanisa yenu, Sauti hiyo ndiyo Sauti iliyo muhimu sana MNAYOPASWA KUISIKIA.

Kuwazia, Maneno yale tunayosikia tunapobonyeza Play ni Sauti ya Mungu inayozungumza nasi moja kwa moja. Baba aliamuru irekodiwe na kuhifadhiwa ili tuweze Bonyeza Play kila sekunde ya kila siku; ili tuweze kumsikia akitutia moyo, kutubariki, kututia mafuta, na kutupilia mbali hofu na mashaka yetu yote, yote kwa Kubonyeza Play tu.

Lolote tunalohitaji papo hapo, Bonyeza Play, na hilo hapo. Yupo kwa ajili ya kutukumbusha SISI NI NENO. Yuko pamoja nasi, karibu nasi, NDANI YETU. Shetani ni mwongo. Ameshindwa. Hakuna kinachoweza kuliondoa Neno hilo kutoka kwetu. Mungu alitupa Hilo kwa kujua kwake tangu zamani, akijua sisi ni Bibi-arusi Wake. Tulikuwa pamoja Naye tangu mwanzo.

Ni Sauti gani tuwezayo kuisikia ambayo ingekuwa kuu kuliko ile Sauti pekee ambayo imethibitishwa na Nguzo ya Moto kuwa ndio Sauti ya Mungu?

Hakuna Sauti nyingine.

Hiyo Sauti ilituambia nini wiki iliyopita?

Mimi kila mara huwadai ninyi kisha—kama ndugu yangu na dada. Ninyi ni watoto wangu; mi—mimi ni baba yenu katika Injili, si baba kama vile kasisi angalikuwa, mimi—mimi ni baba yenu katika Injili kama Paulo alivyosema pale. Nimewazaa ninyi kwa Kristo, na sasa na—nawaposea ninyi Kristo; hilo ni kufanya ninyi muweke nadhiri ya ndoa kwa Kristo kama bikira wasafi. Msiniaibishe! Msiniaibishe! Ninyi iweni bikira safi.

Hatuna budi kukaa bikira safi kwa Neno, hiyo Sauti. Kwetu sisi, kuna NJIA MOJA TU ya kuwa na hakika kuwa tunafanya hivyo: KUBONYEZA PLAY.

Kama mnaniamini mimi kuwa yale mnayosema, mtumishi wa Mungu, nabii, sikizeni yale ninayowaambia. Ona? Huenda msifahamu, na msipoweza, basi fanyeni tu yale ninayowaambia mfanye.

Ndiyo, kuna watu wengine waliotiwa mafuta na Roho Mtakatifu, na kwa neema na rehema za Mungu, Naomba kuwa mimi ni mmoja wa watu hao. Ninaamini kuwa nimeitwa na Yeye kulidumisha Neno Lake mbele zenu na kuwaelekeza ninyi kwenye Ujumbe huu, Neno la Mungu, ile Sauti.

Kama vile Petro alivyosema, sitazembea kuwakumbusha daima kwamba KUNA SAUTI MOJA TU ambayo Mungu aliyoiita kulifunua Neno Lake. Sauti Moja ambayo Mungu aliyoithibitisha. Sauti moja ile ambayo Mungu aliyosema, “Msikieni Yeye.” Sauti moja ile ambayo Mungu aliyosema, “Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.”

Kumbukeni hili kwa mioyo yenu yote: dumuni kwa Neno hilo! Msiache Neno hilo! Cho chote ambacho ni kinyume cha Hilo, kiachilie, haidhuru ni nini. Ndipo unajua ni sahihi.

Hakika ninaelewa kwa nini ninaeleweka vibaya na kwamba wengine wanahisi kuwa niko kinyume na wahudumu wote; kwamba naamini hakuna mtu anayepaswa kuhubiri. “Ukimsikiliza mhudumu mwingine isipokuwa Ndugu Branham, wewe si Bibi-arusi.” Kama nilivyosema mara nyingi, sijawahi kusema hivyo au kuamini hivyo.

Nabii alilieleza hilo kikamilifu wiki iliyopita jinsi gani kabisa Ninavyojisikia na kile Ninachoamini.

Kulikuwa na angalau makanisa mengine matatu ya Ujumbe katika eneo la Jeffersonville wakati Ndugu Branham alipokuwa hapa. Katika ibada ya Jumapili iliyopita, alisema kwamba wachungaji wa mahali hawakuwepo pale katika ibada ya jioni. Walikuwa na ibada zao wenyewe za jioni. Hivyo, hawakujisikia kuja kumsikiliza Ndugu Branham katika ibada ya jioni, bali wawe na ibada makanisani mwao. Huo ndio ulikuwa uamuzi wao na kile walichojisikia wanaongozwa kufanya, na Ndugu Branham alikubali.

Leo hii bado kuna makanisa kadhaa katika eneo la Jeffersonville. Wao pia yawapasa wafanye kama jinsi wanavyojisikia wanaongozwa na Bwana kufanya. Kama hawajisikii kuzicheza kanda, Bwana asifiwe, wanafanya kile wanachojisikia wanaongozwa kufanya, na hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanya. Wao bado ni ndugu na dada zetu na wanaupenda Ujumbe huu. Lakini lazima sisi tufanye kile tunachojisikia tunaongozwa kufanya: Kubonyeza Play. Tunataka kumsikia nabii.

Kama tu vile Ndugu Branham alivyofanya mnamo tarehe 30 Agosti, 1964, ninawaalika mje mkaungane nasi saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) kwa mara nyingine tena tunapomsikia nabii akituletea Ujumbe:  64-0830M Maswali Na Majibu #3.

Ndugu. Joseph Branham