26-0920 Mbegu Ya Hitilafu

Ujumbe: 65-0118 Mbegu Ya Hitilafu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa 1 WAO, [ 1 of TM inamaanisha pia 1 of Tape Ministry- 1 wa Huduma ya Kanda—Mh.]

Watu wanapotuuliza:

S: Je, wewe ni mmoja wao “Bonyeza Play” watu wa kanda wale wanaoamini kwamba Mungu alimtuma William Marrion Branham kumwita Bibi-arusi wa Mungu atoke?

J: NDIYO, Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Je, Unaamini kila Neno lililonenwa kwenye hizo Kanda?

J: Bwana asifiwe, Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Basi lazima unaamini pia kwamba yakulazimu Kubonyeza Play na kuisikia Sauti Yake ili uwezekuwa Bibi-arusi wa Kristo?

J: Utukufu, huyo ndiye hasa Mimi niliye, huyo ni mimi kindakindaki…Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Unaniambia, unaamini kweli kwamba wewe ni aliyechaguliwa, mteule, Uzao wa Kifalme ambao umekusudiwa kimbele tangu misingi ya ulimwengu kuliamini Neno Lake, kuwa Bibi-arusi Wake, na ni mkamilifu machoni Pake, bila dhambi yoyote, na huwezi kabisa kudanganywa?

J: Haleluya, umeelewa, huyo ni mimi kabisa kabisa, MIMI NI Mmoja Wao.

Kulingana na Yesu Mwenyewe, sisi ndio fasiri ya Neno Lake. Wana wa Ufalme. Dhihirisho la Roho Mtakatifu. Ule Uzao wa Ufalme wa wakati huu.

Unajua nini? Ni wakati wa kila mtu kujua sisi ni nani hasa ili kusiwe na kutatanika. Tutamwacha Mungu azungumze kupitia nabii Wake na ayaweke yote pamoja kwa ajili yenu.

Nguvu zizo hizo zilizounena ulimwengu ukawa ziko katika wale watu walio na Roho Mtakatifu. Hiyo ni kweli. Wanaume kwa wanawake, wakati umewadia kwetu kujua wewe ni nani. Ibilisi anajaribu kukuficha, kukwambia ya kwamba wewe ni maskini kitu kidogo kilichodhalilishwa. Sivyo ulivyo. Ninyi ni wana na binti za Mungu.

Uungu hauko Mbinguni; uko ndani yenu. Haleluya!

J: Uungu hauko Mbinguni, unaishi na kukaa ndani ya kila mmoja wetu!

Kwa kila siku mpya, kwa kila pumzi tunayotwaa, ule Ufunuo Yeye aliotupa wa sisi ni nani unakuwa mkubwa zaidi na zaidi. Sisi ni Neno lililo hai linalokaa katika mwili.

Tunalijua hili kwa sababu Yeye ametupa sisi Ufunuo ni nani Yeye aliyemtuma katika siku yetu; ni yupi ambaye Mungu Yeye Mwenyewe alisema angemtuma kuhubiri na kulifundisha Neno Lake katika Ufunuo 22.

Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa.

Yeye alimtuma malaika Wake: William Marrion Branham, kunena katika MAKANISA YAKE…Hilo ewe rafiki linamaanisha ZICHEZENI KANDA KATIKA MAKANISA YENU. Hilo hata halihitaji ufunuo, unatakiwa tu kusoma.

Kulingana na Neno, huu ndio wakati wa udanganyifu zaidi kuliko katika historia ya ulimwengu. Ile roho ya kweli na ya uongo itafanana sana kiasi kwamba ingewadanganya walio wateule kama yamkini.

Mungu alimtuma MALAIKA WAKE kwa makanisa. Tunayo Sauti Yake viganjani mwetu. Tunaweza kusikia kabisa Neno kwa Neno kile hasa Yeye alichosema. Haihitaji ufafanuzi au fasiri, kile tu Bibi-arusi anachopaswa kufanya ni KUBONYEZA PLAY na KUAMINI.

Yeye alituonya, msibadilishe nukta moja au yodi moja kwenye kanda. Usiweke uelewa wako au mawazo yako, isikieni tu Sauti Yangu na muamini. Hadi leo hii, hilo halijawezekana; bali leo ni kwa sababu Ndio njia ya Mungu iliyoandaliwa ya siku hii.

Tumetoka kuzisikia Nyakati Saba za Kanisa na jinsi ambavyo katika kila wakati, roho hizo ziliinuka ili kuwatoa watu kutoka kwenye Neno la kweli. Jinsi ambavyo katika kila wakati, baada ya mjumbe kuondoka, vile walivyofanya ili kuwapeleka watu kwenye kanuni ya imani au fundisho la sharti; kwao wenyewe na kwenye wazo la mwanadamu.

Leo wao wanajaribu kuuua ushawishi wetu na kusema, “Loo, wanaamini kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia. Yakupasa ucheze kanda kanisani mwako… huo ni upuuzi. Ndugu Branham hakusema kuzicheza kanda kanisani. Hivi sasa ni sauti ya wahudumu ndiyo mnayopaswa kuisikia.”

Kwangu mimi, hiyo ndiyo mbegu ya hitilafu! NI LAZIMA MBONYEZE PLAY na muisikie Sauti ya Mungu makanisani mwenu kwani Ndiyo Sauti PEKEE iliyothibitishwa na Mungu Mwenyewe. Lazima mtii kila Neno alilonena Mungu.

Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa.

Malaika huyo aliyethibitishwa ananena katika Kanisa letu, kwa hivyo Mimi ninawaalika mje muungane nasi kuisikia Sauti hiyo pamoja na Bibi-arusi Wake kutoka kote ulimwenguni kwenye mawasiliano ya simu saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika mashariki) na kusikia: 65-0118 – “Mbegu Ya Hitilafu”.

Ndugu Joseph Branham