Pasaka 2025 – Ibada Maalum ya Ushirika na Kutawadhana Miguu

UJUMBE: 62-0204 Ushirika

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Wa Kristo,

Ni wakati mzuri sana jinsi gani ambao Bibi-arusi atakaokuwa nao Wikendi hii ya Pasaka. Naamini itakuwa moja ya mambo muhimu katika maisha yetu; wakati ambao hatutausahau kamwe. Wikendi kuu maalum.

Kila Pasaka imekuwa wakati ulio maalum kwa Bibi-arusi, tunapoufungia milango yetu ulimwengu wa nje kwa kuvizima vifaa vyetu vyote na vikengeusha-fikira vya kilimwengu, na kuyaweka tu wakfu upya maisha yetu Kwake. Ni wikendi nzima iliyowekwa wakfu kwa ajili Yake katika ibada, tunapozungumza Naye siku nzima kila siku, na kisha kulisikia Neno Lake.

Adui ameyafanya maisha yetu kukengeuka sana na kujaa shughuli za mambo mengi sana ya maisha hadi imekuwa vigumu sana kuufungia ulimwengu nje na kuongea Naye. Hata vifaa vile vile tunavyovitumia kusikia Neno, Shetani hutumia kuhatarisha wakati wetu.

Lakini wikendi hii itakuwa tofauti, na si kama wikendi nyingine ya Pasaka ambayo tumewahi kuwa nayo.

Wakati Bwana alipoweka moyoni mwangu kusikiliza ile Mihuri, sikujua jinsi gani tarehe zingeangukia. Lakini kama kawaida, wakati Wake ni mkamilifu. Jumapili mbili zilizopita, tulikuwa na majaliwa ya kuusikia Muhuri wa 4, Wakati wa Tai, tarehe 6 Aprili, siku ya kuzaliwa ya nabii; jinsi inavyofaa.

Lakini sasa, Bwana anayo hata na zaidi mengi aliyotuwekea sisi. Kama nilivyosema, nilipojisikia Bwana ameweka moyoni mwangu kuicheza Mihuri, nilijua ingechukua wiki kadhaa kumaliza kuicheza kwani kuna Jumbe 10 katika mfululizo huo.

Nilipoitazama kalenda, niliona kwamba Pasaka iliiangia kabla hatujamaliza kuusikia huu mfululizo mzima. Nikawaza mwenyewe, nadhani inatubidi tuache kuisikiliza ile Mihuri na Yeye atanipa Jumbe kwa ajili ya Pasaka.

Mara moja niliona… itakuwa KAMILIFU. Tunaweza kuendelea kuicheza Mihuri huku Muhuri wa Saba ukichezwa Asubuhi ya Jumapili ya Pasaka. Sikuweza kuamini, hilo liliendana kabisa na ratiba. Nilijua papo hapo, HUYU NI WEWE, BWANA.

Nimekuwa nimechangamshwa na nikiwa chini ya matarajio makubwa kwa ajili ya wakati wetu wa Pasaka pamoja na kila mmoja wetu, na pamoja Naye. Nilijua Yeye ametutengenezea ratiba.

Hivyo, ikiwa Bwana akipenda, tutaendelea kuisikiliza Mihuri katika kipindi chote cha Wikendi yetu ya kipekee ya Pasaka.

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu alishiriki Karamu ya Mwisho na wanafunzi Wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Ni fursa iliyoje tuliyo nayo ya kufanya ushirika na Bwana majumbani mwetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba atusamehe dhambi zetu, na atupe sisi sote kile tunachohitaji katika safari yetu.

Lijalie, Bwana. Waponye walio wagonjwa. Wafariji walio wachovu. Wape furaha wanaodhulumiwa. Wape amani walio wachovu, Chakula kwa wenye njaa, Maji kwa wenye kiu, furaha kwa wenye huzuni, uwezo kwa kanisa. Bwana, mlete Yesu miongoni mwetu usiku wa leo, tukiwa tunajitayarisha kushiriki ushirika unaowakilisha mwili Wake uliovunjwa-vunjwa. Tunaomba, Bwana, kwamba Yeye atatuzuru kwa njia ya ajabu sana…

Wabariki wengine, Bwana, kila mahali ulimwenguni, ambao wanangojea kwa furaha kuja kwa Bwana, taa zimetengenezwa, na dohani zimesuguliwa kabisa, na Nuru ya Injili ikiangaza katika sehemu zenye giza.

Hebu na tuanze sote saa 12:00 KUMI NA MBILI JIONI. kwa masaa ya nchi unayoishi ili kusikia Ushirika 62-0204, na kisha nabii atatupeleka katika ibada yetu maalum ya Ushirika na Kutawadhana Miguu, ambayo itakuwa ikicheza kwenye app ya Lifeline (kwa Kiingereza), au unaweza kuipakua ibada hiyo kwa Kiingereza au lugha nyinginezo kwa kubofya anuani iliyo hapa chini.

Tukiufuata Ujumbe, tutakusanyika pamoja na familia zetu majumbani mwetu na kuishiriki Meza ya Bwana.

IJUMAA

Hebu na twende kwenye maombi na familia zetu saa 3:00 TATU ASUBUHI(Ni saa 10:00 KUMI JIONI ya Afrika Mashariki)., na kisha tena saa 06:00 SITA MCHANA, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tukimkaribisha Bwana awe pamoja nasi na azijaze nyumba zetu kwa Roho Mtakatifu tunapojiweka wakfu Kwake.

Mawazo yetu na yarudi huko nyuma hadi kwenye siku ile pale Kalvari, yapata miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani, na kisha tujitoe vivyo hivyo kufanya daima yale yanayompendeza Baba:

Iwapo siku hii ni muhimu sana, moja ya siku zilizo kuu sana, hebu na tuangalie mambo matatu ambayo siku hiyo ilimaanisha kwetu. Tungechukua mamia. Bali asubuhi ya leo nimechagua tu mambo matatu tofauti yaliyo muhimu sana ambayo tunataka kuyachunguza katika muda mfupi ujao; ambayo Kalvari ilimaanisha kwetu. Nami naomba ya kwamba itamhukumu kila mwenye dhambi aliyeko, ya kwamba itamfanya kila mtakatifu kupiga magoti yake, ya kwamba itamfanya kila mgonjwa ainue imani yake kwa Mungu na aondoke ameponywa, kila mwenye dhambi aokolewe, kila aliyerudi nyuma arudi na ajionee aibu, na kila mtakatifu afurahi na apate tumaini jipya na tumaini jipya.

Kisha saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA,(Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) Hebu na tuungane pamoja majumbani mwetu kusikia: 63-0323 Muhuri wa Sita.

Kisha tuungane pamoja katika maombi mara baada ya ibada, katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Tuungane tena sote katika maombi Saa 3:00 TATU ASUBUHI (Ni saa 10:00 KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na saa 6:00 Saa SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na kuitayarisha mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu Yeye atakayotufanyia miongoni mwetu.

Ninaweza kumsikia akisema, “Shetani, njoo hapa!” Yeye ni Bosi sasa. Ananyosha mkono, anaunyakua ule ufunguo wa mauti na kuzimu kutoka ubavuni mwake, akauning’iniza ubavuni Mwake Mwenyewe. “Ninataka kukupa notisi. Umekuwa laghai muda mrefu kutosha. Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai niliyezaliwa na bikira. Damu Yangu ingali imelowa msalabani, na deni kamili limelipwa! Huna haki tena. Umenyang’anywa zote. Nipe funguo hizo!”

Kisha saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, sote tutakusanyika pamoja kulisikia NENO: 63-0324m Maswali na Majibu Juu ya Mihuri.

Hii itakuwa SIKU ILIYO MAALUM jinsi gani kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

Kisha tuungane pamoja katika maombi mara baada ya ibada.

JUMAPILI

Hebu kwanza na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi wakati rafiki yake mdogo, robin, alipomwamsha saa 11:00 ASUBUHI.. Hebu na tumshukuru tu Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, maskini rafiki yangu mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa 3:00 TATU ASUBUHI (Ni saa 10:00 KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na saa 6:00 Saa SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tuungane kwa mara nyingine tena katika mnyororo wetu wa maombi, tuombeane na kujitayarisha kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, (Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) tutakusanyika pamoja kuusikia Ujumbe wetu wa Pasaka: 63-0324e Muhuri wa Saba.

Saa 9:00 TISA ALASIRI, Hebu na tuungane tena katika maombi, tumshukuru Yeye kwa Ajili ya WIKENDI YA AJABU ALIOTUPATIA KUWA PAMOJA NAYE NA PAMOJA NA BIBI-ARUSI WAKE ULIMWENGUNI KOTE.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama vile mwaka jana, ningependa kuwaalika kuungana nasi kwa masaa ya Jeffersonville, katika nyakati zote za maombi kwenye ratiba hii. Ninatambua, hata hivyo, kwamba kuzicheza Kanda Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri kwa masaa ya Jeffersonville ingekuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikieni huru kuzicheza Jumbe hizo katika masaa yanayowafaa. Ningependa, hata hivyo, tuungane pamoja sote Jumapili saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) ili kuusikia Ujumbe wetu wa Jumapili pamoja.

Ningependa pia kukualika wewe na watoto wako kushiriki vipindi vya Creations, Journaling, na maswali ya YF, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunafikiri mtayapenda kwa kuwa yote yanalenga NENO tutakalosikiliza wikendi hii.

Kwa ratiba ya wikendi, taarifa ya kuhusu jinsi ya kujiandaa na ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika kwa ajili ya vipindi vya Creations, Maswali ya Pasaka, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizopo hapa chini.

Hebu na tuzifunge simu zetu kwa ajili ya wikendi ya Pasaka isipokuwa kupiga picha, kusikia Nukuu ya Siku, na kucheza kanda kwenye app ya the Table, app ya Lifeline, au anuani inayoweza kupakuliwa.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kukusanyika pamoja na Bibi-arusi kote ulimwenguni kwa ajili ya wikendi iliyosheheni IBADA, SIFA NA UPONYAJI. Ninaamini kweli ni wikendi ambayo itayabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham

Unahitaji anuani za:

Vitu vya kupakuliwa

Ibada ya Ushirika na Kutawadhana

Kalenda ya ratiba

https://vgrwebsites.blob.core.windows.net/branhamtabernacle/48eec3f2-152c-4c94-8dd1-0a639108de49.pdf

https://vgrwebsites.blob.core.windows.net/branhamtabernacle/48eec3f2-152c-4c94-8dd1-0a639108de49.pdf

Taarifa juu ya jinsi ya kujiandaa na Ushirika

https://branhamtabernacle.org/en/articles/view/1212021_InstructionsForBakingBreadMakingWine

Nyenzo zinazohitajika kwa ajili vipindi vya Creations

https://youngfoundations.org/easter

Maswali ya Pasaka

https://youngfoundations.org/articles/TheRevelationOfTheSevenSeals

ALHAMISI– 6:00 PM (saa za ndani)

62-0204 Ushirika (Huduma Maalum ya Ushirika na Kuosha Miguu)

IJUMAA – saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA (saa za nchi mnayoishi)

63-0323
Muhuri wa Sita

JUMAMOSI– saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA (saa za nchi mnayoishi)

63-0324M
Maswali Na Majibu Juu Ya Mihuri

JUMAPILI– saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA (saa za Jeffersonville) (Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki)

63-0324E
Muhuri wa Saba