UJUMBE: 64-0719E Kuenda Nje Ya Kambi
- 25-1221 Kuenda Nje Ya Kambi
- 24-0317 Kuenda Nje Ya Kambi
- 22-0828 Kuenda Nje Ya Kambi
- 21-0411 Kuenda Nje Ya Kambi
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 17-1011 Kuenda Nje Ya Kambi
- 15-1216 Kuenda Nje Ya Kambi – Preliminari
Laazizi Mpendwa,
Mungu habadiliki. Neno Lake halibadiliki. Mpango Wake haubadiliki. Na Bibi-arusi Wake habadiliki, tutadumu na Neno. Ni zaidi ya uhai kwetu; Ni chemchemi ya Maji Yaliyo Hai.
Kitu pekee tulichoagizwa kufanya ni kulisikia Neno, ambalo ni Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ambayo imerekodiwa na kuwekwa kwenye kanda. Kitu pekee tunachokiona si kanuni ya imani, si kundi la watu, hatuoni kitu kingine ila Yesu, Naye ni Neno lililofanyika mwili katika siku yetu.
Mungu yuko katika Kambi yetu nasi tuko njiani kuelekea Utukufuni tukiongozwa na Nguzo ya Moto, ambayo ni Mungu Mwenyewe akizungumza kupitia nabii Wake aliyethibitishwa wa Malaki 4. Tunakula ile Mana iliyofichwa, Maji Yaliyo Hai ambayo ni Bibi-arusi peke yake ndiye anayeweza kula.
Mungu habadilishi njia Zake, na wala shetani habadilishi zake. Kile alichofanya miaka 2000 iliyopita, yeye anafanya jambo lile lile leo, isipokuwa tu amekuwa mwerevu zaidi.
Sasa, baada ya miaka mia nne, Mungu alitembea moja kwa moja miongoni mwao siku moja. Kulingana na Maandiko, Yeye alikuwa afanyike mwili na akae miongoni mwao. “Jina Lake ataitwa Mshauri, Mfalme wa Amani, Mungu mwenye Nguvu, Baba wa Milele.” Na wakati alipokuja miongoni mwa watu, wao walisema, “Hatutaki Mtu huyu atutawale!….”
Kulingana na Maandiko, Mwana wa Adamu angekuja kwa mara nyingine tena na kuishi na kujifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu, Naye alifanya hivyo, nao wanasema kitu kile kile. Hakika, wanaunukuu na kuuhubiri Ujumbe, lakini hawatataka mtu huyo awatawale.
Hiki ndicho hasa kinachotendeka:
Na kama ilivyokuwa wakati huo, ndivyo ilivyo leo! Biblia ilisema kanisa la Laodikia lingemtupa nje, Naye alikuwa anabisha, akijaribu kuingia. Kuna kasoro mahali fulani. Sasa, kwa nini? Walikuwa wamefanya kambi yao wenyewe.
Mtu anaweza kusema, “Ninajua na ninaamini Ndugu Branham alikuwa nabii. Alikuwa ndiye malaika wa saba. Alikuwa ndiye Eliya. Tunauamini Ujumbe huu. Kisha kutoa aina fulani ya udhuru, wowote ule uwao, wa kutoicheza Sauti PEKEE ya Mungu iliyothibitishwa kanisani mwao… Kuna kasoro mahali fulani. Sasa, kwa nini? Walikuwa wamefanya kambi yao wenyewe.
Ninayasema mambo haya si kulitenganisha kanisa, Neno la Mungu ndilo linalofanya jambo hilo. Mimi Nataka tuungane pamoja, tuwe KITU KIMOJA sisi kwa sisi na pamoja Naye, lakini kuna njia moja tu ya kufanya hivyo: kwenye Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Hiyo ndio BWANA ASEMA HIVI PEKEE.
Mungu ametufunulia njia Yake kamilifu kwetu. Ni tukufu sana na hata hivyo ni rahisi sana. Kila Ujumbe tunaousikia akituambia, anatuhakikishia, anatutia moyo, kwamba SISI NDIO BIBI-ARUSI WAKE. Tuko katika mapenzi Yake makamilifu. Tumejiweka wenyewe tayari kwa KUMSIKIA YEYE.
Ujumbe huu ni wa hivi sasa kuliko gazeti la kesho. Sisi ni unabii unaotimizwa. Sisi ni Neno lililodhihirishwa. Mungu anatuthibitishia kwa kila Ujumbe tunaousikia kwamba leo, Maandiko haya yanatimizwa.
Yawezekana kuwe na baadhi huko nje katika mataifa, ulimwenguni kote, ambao hata kanda hii ingewakuta manyumbani mwao au makanisani mwao. Tungeomba, Bwana, kwamba wakati ibada inaendelea, pale—pale… au kanda inachezwa, au nafasi yo yote tunayoweza kuwamo, au—au hali, yule Mungu mkuu wa Mbinguni na aheshimu huu unyofu wa mioyo yetu asubuhi hii, na kuponya wahitaji, kuwapa wao yale wanayohitaji.
Hebu Subiri kidogo…. hivi Sauti ya Mungu kwa ulimwengu imetoka kutabiri nini na kusema nini?…. watu wangekuwa wakicheza kanda majumbani mwao au makanisani mwao.
Lakini tunakosolewa na kukemewa Kwa kusema ati HATUWEZI kuwa na Kanisa la Kanda la Nyumbani? Ati Ndugu Branham hakuwahi kusema chezeni kanda MAKANISANI mwenu?
UTUKUFU KWA MUNGU, LISIKIE, LISOME, NI BWANA ASEMA HIVI. Na si tu kwamba YEYE alilisema hilo, bali kwa kuzicheza kanda majumbani mwenu na makanisani MWENU, Yule Mungu mkuu wa Mbinguni ataheshimu unyofu wa mioyo yetu na kuwaponya wahitaji na kutupa YOYOTE YALE TUNAYOHITAJI!!
Hii nukuu moja INATHIBITISHA kwamba hawa watu wanawasikiliza wachungaji wao na HAWALISIKII NENO, la sivyo wangewapa changamoto na kuwathibitishia kwa NENO kwamba sisi tuko katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU, na kuko katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU KUZICHEZA KANDA KATIKA MAKANISA YAO.
Siliweki mahali pasipo pake au kulinukuu vibaya Neno kama wengi wasemavyo ati nafanya. Lisikie na ulisome wewe mwenyewe.
Ni rahisi sana na kamilifu sana, BONYEZA PLAY na uisikie Sauti ya Mungu ikizungumza nawe. Sema “Amina” kwa kila Neno usikialo. Hata huna haja ya kulielewa, wewe yakupasa tu kuliamini.
“Nataka kwenda nje ya kambi. Haidhuru itanigharimu nini, nitautwaa msalaba wangu na kuubeba kila siku. Nitatoka nje ya kambi. Hata watu waseme nini juu yangu, nataka kumfuata nje ya kambi. Niko tayari kwenda.”
Njoo upite kizuizi cha sauti uingie kwenye Neno la Mungu pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville.(ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) Hayapimiki yale Mungu anayoweza na atakayofanya na mtu ambaye yuko tayari kwenda nje ya kambi ya mwanadamu.
Ndugu Joseph Branham
Ujumbe: 64-0719E Kuenda Nje Ya Kambi
Maandiko: Waebrania 13:10-14 / Mathayo 17:4-8