UJUMBE: 63-0707M Lile Shtaka
- 25-0921 Lile Shtaka
- 23-1015 Lile Shtaka Na Ushirika wa Nyumbani Na Kutawadhana Miguu
- Pasaka 2022
- 21-0416 Lile Shtaka
- 22-0414 Kutoka kwa Tatu na Kutawadhana Miguu
- 21-0404 Lile Shtaka
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
Wapendwa Walioachiwa Huru,
Sasa, Hapo “wao,” sio wenye dhambi, “Wao,” hao ni, kanisa la siku hiyo, walimwonea makosa yule Mtu aliyekuwa ndiye lile Neno. Sivyo? Walimwonea makosa yule Mtu aliyekuwa lile Neno. Sasa wao hulionea makosa lile Neno likitenda kazi kupitia kwa mtu.
Tangu mwanzo ulimwengu umemtupilia Yeye mbali, umemkataa, umekataa kudumu na Neno Lake kwa kuyashika mapokeo yao, kanuni zao za imani, mawazo yao. Daima wao wameukosa mpango wa Mungu; Mungu, kama Mtu, ambaye alikuwa Neno, na sasa Neno likifanya kazi kupitia huyo mtu.
Lakini katika siku yetu Yeye alisema, “Nitakuwa na kundi dogo, wateule wachache. Wao walikuwa ndani Yangu tangu mwanzo. Watanipokea Mimi na kuliamini Neno Langu na yule mtu Niliyemchagua kulifunua Neno Langu. Yeye atakuwa Sauti Yangu kwao.”
“Wao hawataonea haya kuitangaza Sauti Yangu. Hawataonea haya kuuambia ulimwengu kwamba Mimi nimekuja tena na Nimejidhihirisha Mwenyewe kupitia mwili wa mwanadamu kama nilivyosema Ningefanya. Wakati huu wao hawatamwabudu huyo mtu, lakini wataniabudu Mimi, Neno, litakalonena kupitia mtu huyo. Wao watanipenda Mimi na kunitangaza Mimi kwa kila mshipa wa utu wao.”
“Kwa hivyo, Nimewapa yote wanayohitaji kufanyika Bibi-arusi Wangu. Nimewaimarisha kwa Neno Langu; kwa maana wao NI NENO LANGU lililofanyika mwili. Ikiwa wanahitaji uponyaji, wao hulinena Neno Langu. Ikiwa wana kizuizi chochote kinachowazuia, wao hulinena Neno Langu. Ikiwa wanaye mtoto ambaye amekengeuka, wao hulinena Neno Langu. Chochote kile wanachohitaji, wao hulinena Neno Langu, kwa kuwa wao ni Neno Langu lililofanyika mwili ndani yao.”
“Wanajijua wao ni nani, kwa kuwa Mimi nimejifunua Mwenyewe kwao. Wamedumu wa kweli na waaminifu kwa Neno Langu nao wanaungana pamoja kwenye Sauti Yangu. Kwa maana wanaijua Sauti Yangu, Neno Langu, Roho Wangu Mtakatifu. Wanajua, pale Neno lilipo ndipo Tai watakapokusanyika.”
Wakati nabii Wake alinenapo Neno Lake na kukishtaki kizazi hiki kwa kumsulubisha Yesu Kristo mara ya pili na kuwatangaza kuwa wameangamia, Bibi-arusi atakuwa akifurahi. Kwa maana tunajua SISI NDIYE Bibi-arusi Wake ambaye amelikubali na kulipokea Neno Lake. Tunapaza sauti kutoka ndani ya mioyo yetu na kusema:
Mimi ni Wako, Bwana. Najilaza mwenyewe kwenye madhabahu haya, kwa kujitakasa kama tu nijuavyo kujitendea mwenyewe. Ondosha ulimwengu ndani yangu, Bwana. Yaondoe mambo yaharibikayo kwangu; nipe mambo yasiyoharibika: Neno la Mungu. Na niweze kuishi karibu sana na hilo Neno, hata lile Neno liwe ndani yangu na mimi ndani yake. Nijalie, Bwana. Nisiondoke kwalo kamwe.
Kuna uzima, na kuna mauti. Kuna njia sahihi, na kuna njia mbaya. Kuna ukweli, na kuna uongo. Ujumbe huu, Sauti hii, ndio njia kamilifu iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Njoo uuungane na sehemu ya Bibi-arusi mkuu wa Mungu tunapokusanyika kulizunguka Neno Lake lililofunuliwa na kuusikia Ujumbe: Lile Shtaka 63-0707M.
Ndugu. Joseph Branham