25-0810 Matukio Ya Sasa Yanadhihirishwa Na Unabii

UJUMBE: 65-1206 Matukio Ya Sasa Yanadhihirishwa Na Unabii

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kweli na Aliye Hai,

Wakati Yesu, Neno Mwenyewe, alipokuja duniani miaka 2000 iliyopita, Yeye alikuja kama vile alivyosema angekuja, kama Nabii. Neno Lake linatangaza, ya kwamba kabla Yeye hajaja tena, kule kudhihirishwa kukamilifu kwa Utu wa Yesu Kristo kutadhihirishwa tena katika mwili, katika nabii. Nabii huyo amekuja, jina lake ni William Marrion Branham.

Mtu yeyote anawezaje kutotambua kwamba kuisikiliza Sauti ya Mungu ikizungumza nao moja kwa moja kwenye kanda ndiyo Mapenzi makamilifu ya Mungu? Tunajua Neno daima humjia nabii Wake; Haliwezi kuja kwa njia nyingine yoyote. Halina budi kuja kupitia njia ya Mungu ambayo Yeye alitutabiria. Hiyo ndiyo njia pekee litakavyopata kuja. Mungu anasonga mbele moja kwa moja jinsi Yeye alivyoahidi angefanya. Yeye kamwe hakosi kufanya kwa njia ile ile Yeye aliyofanya daima.

Kila mmoja wao alikula kitu kile kile, wote walicheza katika Roho, wote walikuwa na kila kitu shirika; bali ilipofikia wakati wa utengano, Neno lilitenganisha. Ndivyo ilivyo siku hizi! Neno lilitenganisha! Wakati utakapowadia…

Tunauona wakati huo unatukia sasa hivi, Neno linatenganisha. Bibi-arusi anashutumiwa kwa kumwinua sana nabii wakati wao wanaposema, “Kuna wengine walioitwa na Mungu, watu waliojazwa na Roho Mtakatifu wa kumwongoza Bibi-arusi leo. Mnahitaji zaidi ya hizo kanda tu. Mungu amewaweka watu leo kuliongoza kanisa.”

“Unajaribu kuwazia wewe ndiwe uliye peke yako kwenye kundi lile. Kusanyiko lote ni takatifu!” Mungu kamwe hajawahi kushughulika jinsi hiyo. Alipaswa kuwa amejua vyema kuliko hivyo. Naye akasema, “Vema, kusanyiko lote ni takatifu. Unajaribu kujifanya…” Kama tungalilisema siku hizi, maneno ya mtaani, “Changarawe pekee ufukoni.”

Naye Musa alijua ya kwamba Mungu alikuwa amemtuma huko chini kwa ajili ya jambo hilo.

Mungu anao watu waliojazwa na Roho Mtakatifu wa kumwongoza Bibi-arusi Wake; kuwaongoza KWENYE BWANA ASEMA HIVI, NABII-MJUMBE. Kwani Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja. Hiyo ndiyo njia ya Mungu isiyobadilika kamwe kwa ajili ya siku hii, na daima.

Kwa sababu walisikiliza kosa fulani. Wakati Musa, aliyethibitishwa na Mungu, na kiongozi wa kuwaonyesha njia ya kwenda kwenye nchi ya ahadi, nao walikuwa wamekuja umbali huo vema, lakini basi wasingeendelea pamoja naye… Sasa, waaminio wanaweza kuona jambo hilo, bali wasioamini hawawezi kuliona Hilo limethibitishwa.

Sio tu kwamba wewe ulichaguliwa kuupokea Ufunuo huu mkuu wa wakati wa mwisho wa siku hii, bali Mungu, kwa njia ya Chakula Chake kilichohifadhiwa cha kanda, hunena katikati ya mistari na Bibi-arusi Wake kipenzi.

Ndipo endapo wewe ni mwana wa Mungu ama binti ya Mungu, ulikuwa ndani ya Mungu wakati wote. Lakini Yeye alijua utapandwa kwenye tuta gani na katika wakati gani. Kwa hiyo sasa umefanywa kiumbe, mwana wa Mungu, mwana ama binti ya Mungu aliyedhihirishwa upate kukabiliana na changamoto ya wakati huu kumthibitisha Mungu wa kweli na aliye hai wa wakati huu, Ujumbe unaotokea katika wakati huu. Hiyo ni kweli! Ulikuwapo pale kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Ni barua ya mahaba ilioje ya katikati ya mistari kwa Bibi-arusi Wake, UTUKUFU!!! Sio tu kwamba Yeye alitujua na kutuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, bali hapa Yeye anatuambia kwamba alituchagua sisi tuwe wana na binti zake waliodhihirishwa wa SIKU HII. Alituweka hapa duniani leo, juu ya watakatifu wengine wote tangu mwanzo, kwa maana Alijua sisi tungekabiliana na changamoto ya wakati huu kumthibitisha Mungu wa kweli na aliye hai wa wakati huu, Ujumbe unaotokea katika wakati huu.

Sisi tulikuwa ndani ya Mungu, jeni, neno, sifa tangu mwanzo, lakini SASA tunaketi PAMOJA katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu, tukishiriki pamoja Naye kwa Neno Lake, kupitia Neno Lake; kwa kuwa sisi ni NENO LAKE, nalo linazilisha nafsi zetu.

Hatuwezi, na hatutaingiza Kitu chochote maishani mwetu ila Neno la Mungu lisiloghoshiwa. Tunatambua na kuamini kuwa Ndio njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii.

Tungependa muungane nasi Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia SAUTI PEKEE, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda, unayoweza kusema AMINA kwayo, kwa kila Neno unalosikia.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: Matukio Ya Sasa Yanadhihirishwa Na Unabii 65-1206

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo 22
Kumbukumbu la Torati 18:15
Zaburi 16:10 / 22:1 / 22:18 / 22:7-8 / 35:11
Isaya 7:14 / 9:6 / 35:7 / 50:6 / 53:9 / 53:12 / 40:3
Amosi 3:7
Zekaria 11:12 / 13:7 / 14:7
Malaki 3:1 / 4:5-6
Mathayo 4:4 / 24:24 / 11:1-19
Luka 17:22-30 / 24:13–27
Waebrania 13:8 / 1:1
Yohana 1:1
Ufunuo 3:14-21 / 10:7