25-0608 Kiongozi

UJUMBE: 62-1014E Kiongozi

PDF

BranhamTabernacle.org

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Anayejikusanya Pamoja,

Sasa Mungu daima amewatuma viongozi Wake, Yeye daima hajakosa kuwa na kiongozi, katika nyakati zote. Mungu daima amekuwa na mtu fulani aliyemwakilisha katika dunia hii, katika nyakati zote.

Mungu hataki sisi tutegemee akili zetu au mawazo yoyote yaliyobuniwa na mwanadamu. Ndiyo maana Yeye humtumia Bibi-arusi Wake Kiongozi; kwa kuwa yeye ana fahamu, jinsi ya kwenda na nini cha kufanya. Mungu HAJAWAHI KAMWE KUBADILI mpango Wake. Yeye hajashindwa kamwe kuwatumia watu Wake Kiongozi, bali huna budi kumkubali Kiongozi huyo.

Huna budi kuamini kila Neno Yeye analosema kupitia Kiongozi Wake. Huna budi kwenda njia Kiongozi Wake anayosema uende. Ukipata kusikiliza na kuamini sauti zingine kama kiongozi wako, mwishowe utapotea tu.

Yohana Mtakatifu 16 inasema Yeye alikuwa na mambo mengi ya kutuambia na kutufunulia, hivyo Yeye angemtuma Roho Wake Mtakatifu Kutuongoza na kutuambia. Alisema Roho Mtakatifu ndiye nabii-kiongozi wa kila kizazi. Hivyo, manabii Wake walitumwa kumwakilisha Roho Mtakatifu ili kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Roho Mtakatifu anatumwa kuliongoza kanisa, si kundi fulani la watu. Roho Mtakatifu ndiye hekima yote. Mwanadamu huwa mgumu, asiyejali.

Si huyo mtu, bali ni Roho Mtakatifu NDANI ya mtu huyo. Mtu Aliyemchagua kujiwakilisha Mwenyewe na kuwa kiongozi wetu wa duniani ambaye anaongozwa na Kiongozi wetu wa Mbinguni. Neno linatuambia hatuna budi kumfuata Kiongozi huyo. Haidhuru tunafikiri nini, yale yanayoonekana ni ya maana, au kile mtu mwingine asemacho, sisi hatuwezi kupambanua jambo hilo, kiongozi ndiye tu anayeweza.

Mungu hutuma Kiongozi, naye Mungu anataka mkumbuke ya kwamba huyo ni Kiongozi Wake aliyemchagua.

Nabii-kiongozi wetu amechaguliwa na Mungu kulinena Neno Lake. Neno lake ni NENO LA MUNGU. Nabii- kiongozi, na yeye peke yake, ndiye aliye na fasiri ya kiungu ya Neno. Mungu alilinena Neno Lake kwake mdomo kwa sikio. Kwa hivyo, huwezi kupinga, kubadilisha, au kulihoji Neno la Kiongozi wako.

Lazima umfuate Yeye, na Yeye peke yake. Usipofanya hivyo, mwishowe utapotea. Kumbuka, unapomwacha, Kiongozi aliyechaguliwa na Mungu, unakuwa peke yako, kwa hiyo sisi tunataka kuwa karibu na kiongozi Aliyemchagua, na kusikia na kutii kila Neno Yeye analolisema kupitia yeye.

Kiongozi wetu ametufundisha kwamba agano la kale lilikuwa kivuli cha agano jipya.

Israeli walipotoka Misri wakienda kwenye ile nchi ya ahadi, katika Kutoka 13:21, Mungu alijua ya kwamba wao hawajapita njia hiyo hapo kabla. Ilikuwa tu maili arobaini, bali hata hivyo walihitaji kitu fulani cha kwenda pamoja nao. Wangepotea njia. Kwa hiyo Yeye, Mungu, akawatumia Kiongozi. Kutoka 13:21, kitu kama hiki, “Ninamtuma Malaika Wangu aende mbele zenu, ile Nguzo ya Moto, ili awalinde njiani,” kuwongoza kwenye nchi hii ya ahadi. Nao wana wa Israeli wakamfuata Kiongozi yule, ile Nguzo ya Moto (usiku), Wingu mchana. Wakati iliposimama, wao wakasimama. Wakati iliposafiri, wao wakasafiri. Basi Yeye alipowafikisha karibu na ile nchi, nao hawakuwa wanastahili kuvuka, Yeye aliwaongoza akawarudisha jangwani tena.

Alisema hilo ni kanisa leo hii. Tungekuwa tayari tumekwishaondoka kama tu tungejisahihisha wenyewe na kujiweka sawa, bali Yeye hana budi kuzidi kutuongoza kuzunguka na kuzunguka na kuzunguka.

Wao walipaswa tu kumfuata kiongozi wao kama vile YEYE ALIVYOIFUATA na kusikia kutoka kwenye ile Nguzo ya Moto. Yeye aliwaambia yale Mungu aliyosema nao walipaswa kutii kila Neno yeye alilosema. Yeye alikuwa ndiye Sauti ya yule Kiongozi. Lakini wao walihoji na kubishana na yule kiongozi aliyechaguliwa na Mungu, hivyo wakatangatanga nyikani kwa miaka 40.

Kulikuwa na wahudumu wengi katika siku za Musa. Mungu alikuwa amewachagua kuwasaidia hao watu, kwa vile Musa asingeweza kufanya yote. Lakini wajibu wao ulikuwa ni kuwaelekeza watu kwenye yale Musa aliyosema. Biblia haisemi chochote kile hao watu walichosema, inasema tu yale Musa aliyosema kuwa ndilo Neno la kuwaongoza hao watu.

Wakati Mungu alipomwondoa Musa jukwaani, Yoshua alitawazwa kuwaongoza hao watu, ambalo inamwakilisha Roho Mtakatifu leo. Yoshua hakuhubiri jambo lolote jipya, wala yeye hakujaribu kupachukua mahali pa Musa, wala hakujaribu kufasiri kile kiongozi alichosema; yeye aliyasoma tu yale Musa aliyosema na kuwaambia watu, “Kaeni na Neno. Kaeni na yale Musa aliyosema”. Yeye aliyasoma tu yale Musa aliyosema.

Ni mfano mkamilifu jinsi gani wa leo hii. Mungu alimthibitisha Musa kwa Nguzo ya Moto. Nabii wetu alithibitishwa kwa Nguzo ile ile ya Moto. Maneno ambayo Musa aliyoyanena yalikuwa ni Neno la Mungu na yakawekwa ndani ya lile Sanduku. Nabii wa Mungu alinena katika siku yetu na Hilo liliwekwa kwenye kanda.

Wakati Musa alipoondolewa jukwaani, Yoshua alitawazwa kuwaongoza hao watu kwa kuyadumisha Maneno aliyoyanena Musa mbele yao. Aliwaambia waamini na wadumu na kila Neno lililonenwa na kiongozi wa Mungu.

Yoshua aliyasoma kila mara yale Musa aliyoyaandika Neno kwa Neno kutoka kwenye magombo. Yeye aliliweka Neno mbele yao daima. Neno la siku yetu halikuandikwa, bali lilirekodiwa ili Roho Mtakatifu aweze kumfanya Bibi-arusi Wake asikie Neno kwa Neno kile Yeye alichosema, kwa Kubonyeza Play.

Mungu kamwe habadilishi mpango Wake. Yeye ndiye Kiongozi wetu. Sauti Yake ndiyo inayomwongoza na kumuunganisha Bibi-arusi Wake leo. Sisi tunataka tu kuisikia Sauti ya Kiongozi wetu vile Inavyotuongoza kwa Nguzo ya Moto. Ni muungano usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo. Tunaijua Sauti Yake.

Wakati kiongozi wetu anapokuja mimbarani, Roho Mtakatifu anamshika na Si yeye tena, bali ni yule Kiongozi wetu. Anakiinua kichwa chake hewani na kupaza sauti, “Bwana Asema Hivi, Bwana Asema Hivi, Bwana Asema Hivi! Na kila mshiriki wa Bibi-arusi wa Kristo kote ulimwenguni huja moja kwa moja kwake. Kwa nini? TUNAMJUA KIONGOZI WETU KWA JINSI TU YEYE ANAVYOONGEA.

Kiongozi wetu = Neno
Neno = Humjia nabii
Nabii = Mfasiri pekee wa kiungu wa Mungu; kiongozi Wake wa duniani.

Kaeni nyuma ya Neno! Loo, naam, bwana! Kaeni na Kiongozi huyo. Kaeni vema sawasawa nyuma Yake. Msiende mbele Yake, kaeni nyuma Yake. Hebu Hilo na liwaongoze, msiliongoze. Liachilieni liende.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe:

62-1014E – Kiongozi

Maandiko:

Marko 16:15-18
Yohana Mtakatifu 1:1 / 16:7-15
Matendo 2:38
Waefeso 4:11-13 / 4:30
Waebrania 4:12
2 Petro 1:21
Kutoka 13:21