25-0518 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3

UJUMBE: 60-0522M Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bikira Safi, 

Tunapobonyeza Play, ni asali mwambani, ni furaha isiyotamkika, ni dhamana iliyobarikiwa, ni nanga ya nafsi zetu, ndio tumaini na tegemeo letu, ni Mwamba wenye Imara, ni kila kitu kilicho chema, ndio Njia ya Mungu iliyoandaliwa ya siku hii. 

Kwa sababu Tunabonyeza Play, Sauti ya Mungu imetuposea; imetuposa kwa Kristo, kama Bikira Safi kwa Neno Lake. Tunaye ila Mwalimu Mmoja tu, Sauti Moja, Nabii Mmoja, anayetuongoza kwa Roho Mtakatifu. 

Bali hili ni kanisa, ninawafundisha. Haya yananaswa kwenye kanda. Nawataka watu wanaosikiliza kanda, wakumbuke, hili ni kwa ajili ya kanisa langu.

Ni thibitisho lililoje kwetu sisi ya kwamba tuko katika Mapenzi Yake makamilifu. Kanda hizo ni kwa ajili ya kanisa Lake. Yeye anatufundisha. Anatuambia, sikilizeni kanda.

Yeye aliuanza mfululizo huu wa Kufanywa Wana Wenye Mamlaka kwa kutueleza kile kilichotokea siku chache zilizopita. Ndipo, kwenye kila Ujumbe, yeye hunena habari za wakati alipokuwa amebadilishwa. Jinsi gani Hilo litakuwa ni muhimu kwa Bibi-arusi kusikia kile kilichotukia na kile Bibi-arusi alichomwambia yeye.  

Nabii wetu atahukumiwa kwa Neno alilohubiri na kuliacha kwenye kanda. Wale Bibi-arusi kule ng’ambo ya pili walimwambia atakubaliwa na Bwana wetu. Kisha yeye atatukabidhi Kwake kama tunu za huduma yake, kisha tutarudi duniani tena tukaishi milele.

Kila Neno tunalolisikia ni kito cha thamani. Tunaendelea tu kuliweka wazi na kuliweka wazi Yeye anapozidi kufunua zaidi tunaposoma katikati ya mistari. 

Jinsi gani tupendavyo kulishiriki Hilo na ndugu na dada zetu, “Je, umelisikia hili?” 

“Yeye alituchagua katika Yeye kabla ulimwengu hata haujakuweko”? Huo ndio urithi wetu. Mungu alituchagua, kisha akamwacha Yesu aje alipe ile deni. Hiyo ni nini? Kumwaga Kwake kwa Damu Yake, kusudi tusihesabiwe dhambi. Hufanyi lo lote.

Kisha, mara tu baada ya hilo, Je, umelipata hili?

“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana.” Umeelekeza macho yako Kalvari, na hakuna kitu kitachokuzuia! Mwenendo wa maisha yako, unatembea katika Barabara Kuu ya Mfalme, umepakwa na Mafuta ya thamani, ukielekea kwenye Patakatifu pa patakatifu. Whiu! Amina.

Sisi tulikuwa kama ile fimbo ya Haruni, fimbo ya kale iliyokauka ambayo alikuwa ameibeba kwa miaka arobaini kule jangwani.  Lakini sasa, kwa sababu tumewekwa katika Mahali pale Patakatifu kwa kuisikia Sauti ya Mungu ikinena nasi kwenye kanda, tumechipuka na kuchanua, tukiwa tumejaa Roho Wake Mtakatifu, nasi Bibi-arusi Wake tukipaza sauti kwa mapafu yetu yote.

⚪ Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana, kanda ndizo nafasi ya kwanza mioyoni mwetu.  

⚪ Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu kwa Bwana, Yeye alituchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

⚪ Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana, sisi ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

⚪ Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana, haileti tofauti yo yote yale mtu ye yote asemayo, hatuzirudishi kanda, tunazicheza nyingi zaidi. 

⚪ Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana, tumeyaelekeza macho yetu Kalvari, na hakuna kitu kitakachotuzuia. 

Nina furaha sana kuungana moyoni na watu wengi hapa ambao wanajua kwamba Hili ni Neno la Mungu lisilokosea. Basi Hilo, Hilo ni Kweli kwa kila Neno, kila Neno Lake, kila fungu Lake. Na kwa neema ya Mungu, kama nilivyotunukiwa kuiangalia ile Nchi ambayo siku moja tutaizuru.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika) Nabii anapolichukua kila Neno na kulifafanua tu kindani. Atalipeleka hadi Mwanzo na kulifafanua kindani, na atalipeleka hadi Kutoka na kulifafanua tena, na hata hadi Ufunuo; na Ni Yesu kwa kila kipengee!

Ndugu. Joseph Branham 

Ujumbe: 

Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3 60-0522M

Maandiko:

Mathayo 28:19

Yohana 17:7-19

Matendo 9:1-6, Sura ya 18 na 19

Warumi 8:14-19

1 Wakorintho 12:12-13

Wagalatia 1:8-18

Waefeso Sura ya 1

Waebrania 6:4-6, 9:11-12