UJUMBE: 60-0518 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2
- 25-0511 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2
- 21-0627 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2
- 18-0617 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2 – Preliminari
- 16-0224 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2
Mpendwa Ukuhani Wa Kifalme,
Kila mtu na aume kidole chake, finya nafsi yako, na ufanye moyo wako thabiti. Leo, Bibi-arusi wa Yesu Kristo anapaza sauti:
Leo, unabii huu umetimia mbele ya macho yetu.
Ninaamini, moja ya siku hizi tukufu, wakati muungano huu wa umoja wa kanisa utakapoungana, kisha papa mpya atoke Marekani na kuwekwa huko juu kulingana na unabii, ndipo basi watafanya sanamu kama ya yule mnyama.
Sauti ya nabii wa Mungu ililinena hilo Tarehe 19 mwezi Desemba, 1954, na miezi 9 baadaye, Robert Prevost, ambaye sasa anajulikana kama Papa Leo XIV, alizaliwa. Yeye sasa ndiye papa mpya wa Rumi. “Bwana Asema Hivi” imetimia.
Tarehe 7 mwezi Mei, 1946, MUNGU alimweka nabii Wake kule Green’s Mill, Indiana, kumpa agizo lake na kuutangazia ulimwengu, huyu ndiye malaika-mjumbe Wangu wa saba mwenye nguvu, Sauti Yangu kwa ulimwengu. Msikieni Yeye.
Wakati Malaika wa Bwana alipokutana nami kule Green’s Mill, Indiana, miaka minane iliyopita; baada ya kuwa tangu utotoni, akinifuata, akionyesha maono. Nilipomwendea, alisema, “Kama utakuwa mwaminifu, wafanye watu wakuamini, hakuna kitakachosimama mbele ya maombi.”
William Marrion Branham ndiye Sauti teule ya Mungu kwa ulimwengu. Nabii hodari ambaye Neno la Mungu humjia. Kulingana na Neno, yeye ndiye mfasiri PEKEE wa Kiungu wa Neno la Mungu.
Yeye alithibitishwa na Mungu Mwenyewe, kwa Nguzo ya Moto.
Tarehe 7 mwezi Mei, 2025, SHETANI aliliweka Baraza lake la Makardinali katika Kanisa la Sistine huko Rumi ili kumchagua Halifa wao wa Kristo, ili kuitimiza Bwana Asema Hivi.
Yeye alithibitishwa na mtu mwenye PAFU LA MOSHI MWEUPE.
Bibi-arusi wa Kristo ulimwenguni kote anafurahi, anapiga kelele, anapiga vifijo na kumsifu Bwana tunaposikia, na kuona kwa macho yetu wenyewe, unabii wa nabii ukitimia.
Ni kana kwamba tunaiona Bahari ya shamu ikifunguka mbele ya macho yetu. Mana mpya ikianguka kutoka angani. Mamilioni ya kware wakimshibisha Bibi-arusi. Maji yakitoka kwenye Mwamba. Moto ukishuka na kuiteketeza dhabihu tukiwa na Eliya.
Unabii unatimizwa kila siku. Neno la Mungu lililoahidiwa linadhihirishwa katika maisha yetu. Mambo yanatukia pande zote. Bibi-arusi amejiweka mwenyewe tayari kwa kulisikia na kuliamini Neno. Sisi ni Neno lililofanyika mwili.
Hakika, tumewasili. Muda umewadia. Bibi-arusi anafurahi na kuungana pamoja ulimwenguni kote kuliko hapo awali. Nabii anamhakikishia upya Bibi-arusi kwa kutuambia sisi ni ukuhani wa kifalme wa Mungu, taifa takatifu, watu wa kipekee walioitwa watoke, wateule, waliochaguliwa na wakatengwa.
Sisi SASA TU Wana na Binti za Mungu, Tukiongozwa na Roho wa Mungu; si na mwanadamu, bali na Roho. Tunajua, pasipo na shaka hata chembe, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE. IMANI yetu inafikia viwango vipya kila siku. Hakuna wa kutuzuia au kutupunguza mwendo, Mungu ametufunulia hilo na kulitia nanga katika mioyo na nafsi zetu.
Bibi-arusi tumetambua kikamilifu sisi ni nani. Tuko katika Nchi yetu ya ahadi ya kiroho, tumemiliki kabisa kila kitu. Tuna amani ya Kimbinguni, baraka za Kimbinguni, Roho wa Kimbinguni. KILA KITU NI CHETU. Tunajiweka tayari tu kwa ajili ya yale yajayo ambayo Yeye ametutayarishia.
Parapanda ya Bwana italia, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Miili hii ya mbinguni itashuka ije ivae ya duniani, miili ya utukufu nasi tutabadilishwa kwa dakika moja, kufumba na kufumbua. Tutanyakuliwa pamoja nao, kumlaki Bwana hewani.
Ni siku ilioje. Ni wakati wa jinsi gani. Hakuna njia ya mimi kusema kwa maneno ya kibinadamu kile sisi sote tunachokihisi katika nafsi zetu. Mioyo yetu inaenda mbio. Hatulifanyi hilo, Roho Mtakatifu ni kama kisima kinachofoka maji kikibubujika ndani yetu. Bibi-arusi amekuwa akiungojea wakati huu tangu siku za Adamu…NA SASA SISI TUMEWASILI.
Tunawakaribisheni. Tunawaalika. Tunawasihi. Njooni muungane nasi kwa ajili ya wakati mkuu sana ambao ulimwengu umepata kuujua, tunapoisikia Sauti ya Mungu ikilifunua Neno Lake kwetu Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia: 60-0518 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:
Mwanzo 1:26
Waefeso Sura ya 1
Warumi 8:19
Wagalatia 1:6-9
Waebrania Sura ya Sita
Yohana 1:17