UJUMBE: 60-0515E Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1
- 25-0504 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1
- 21-0620 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1
- 18-0603 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1
- 16-0221 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1
Wapendwa Waliofanywa Wana Wenye Mamlaka,
Sasa hivi tunakula vile vitu vigumu vya Mungu na kuwa na ufahamu pevu wa Neno Lake. Mungu ametupa Ufunuo wa kweli wa Neno Lake. Ufahamu wetu wa kiroho haujavurugika.
Sisi TUNAJUA Yeye ni Nani hasa. TUNAJUA hasa kile Yeye alicho. TUNAJUA hasa wapi tunakoelekea. TUNAJUA hasa sisi ni nani. TUNAMJUA Yeye tunayemwamini na kusadiki kuwa Yeye aweza kukilinda kile tulichoweka amana kwake hata siku ile.
Yeye amenena na kutufunulia sisi siri zote zilizokuwa zimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alituambia jinsi ambavyo wengine daima wao wameikataa njia Yake iliyoandaliwa na kutamani uongozi tofauti, lakini Yeye angekuwa na kundi dogo ambalo litadumu waaminifu kwa Neno Lake.
Kote ulimwenguni, hawatakusanyika mahali pamoja na kuwa na vitu shirika. Lakini makundi madogo yatakuwa yametawanyika kote duniani.
Utukufu, tumetawanyika duniani kote, lakini Tumeungana kama Mmoja kwa Kubonyeza Play na kuisikiliza Sauti ya Mungu ikizungumza nasi.
Hebu na tuchunguze na tutangulie kuonja yale Yeye atakayokuwa akitueleza kupitia malaika Wake mwenye nguvu siku ya Jumapili.
Wapendwa Wangu waliochaguliwa, sasa mmeketi pamoja katika Mahali pa Mbinguni. Si popote pale, bali katika mahali pa “Mbinguni”; ndipo mahali pako kama mwaminio. Mmeomba vya kutosha nanyi mko tayari kwa Ujumbe. Mmekusanyika pamoja kama watakatifu, mliobatizwa na Roho Mtakatifu, mliojazwa na baraka za Mungu. Mmeitwa, mmeteuliwa, nazo roho zenu zimewaleta katika hali ya Kimbinguni.
Nini kingetokea. Roho Wangu Mtakatifu atakuwa akitembea katika kila moyo. Mmezaliwa upya na mmekuwa kiumbe kipya katika Kristo Yesu. Dhambi zenu zote ziko chini ya Damu. Mko katika ibada kamilifu, huku mikono na mioyo yenu imeinuliwa Kwangu Mimi, mkiniabudu MIMI pamoja katika mahali pa Mbinguni.
Ninyi mlichaguliwa kimbele, Mkateuliwa, katika kutangulia Kwangu Kujua. Mkachaguliwa, Mkatakaswa, mkahesabiwa Haki kwa Kukusudiwa Kimbele. Haiwezekani kwenu ninyi kudanganywa. Nimewakusudia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ninyi ni mungu mdogo, mliotiwa muhuri kwa Roho Mtakatifu wa ahadi; sio tu waliozaliwa katika familia, Wana na Binti Zangu wenye mamlaka.
Nitawabariki kwa uponyaji wa kiungu, kutangulia kujua, ufunuo, maono, nguvu, lugha, fasiri, hekima, maarifa, na baraka zote za Kimbinguni, kwa furaha isiyoneneka na iliyojawa na Utukufu.
Kila moyo utajazwa na Roho Wangu. Mtakuwa mkitembea pamoja, mkiketi pamoja, katika mahali pa mbinguni. Hakuna wazo moja baya kati yenu, hakuna hata sigara moja inayovutwa, hakuna nguo moja fupi, hakuna jambo hili, lile au lingine, hakuna wazo moja baya, hakuna aliye na neno dhidi ya mwingine, kila mtu akinena kwa upendo na upatanifu, kila mmoja katika moyo mmoja na mahali pamoja.
Ndipo kutakuja ghafla toka Mbinguni sauti kama upepo wa nguvu ukienda kasi Nami nitawabariki kwa baraka zote za rohoni. Ndipo mtakuwa kama vile Daudi, mkicheza mbele ya Sanduku, mkiuambia ulimwengu hamuonei haya, NINYI NI BIBI-ARUSI WANGU WA KANDA! Mnabonyeza play na mnaamini KILA NENO ninalosema. Ninyi hamta, na hamwezi kuondoshwa!
Wengine wanaweza kulikataa, au wasilielewe, lakini kwenu ninyi, Ni Beji yenu ya Heshima. Kama vile Daudi alivyomwambia mkewe; “Hivi Mnadhani hili lilikuwa ni kitu, ngojeni tu hadi kesho, tutakuwa tukisikiliza kanda hata na zaidi, tukimsifu Bwana, tukiwa tumejazwa na Roho Wake; kwa maana tunaishi Kanaani, tukielekea nchi ya ahadi.”
Kisha nitaangalia chini kutoka Mbinguni na kukuambia:
“Wewe ni Bibi-arusi aupendezaye moyo Wangu.”
Baraka hizi zinaweza kuwa zako pia. Njoo, uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na ujionee uwepo wa Bwana zaidi ya hapo awali tunapoisikiliza Sauti ya Mungu ya siku hii ikinena nasi na kutuletea Ujumbe: Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1 60-0515E.
Kumbukeni, hili ni kwa ajili ya kanisa, si kwa mtu aliyeko nje. Kwake ni siri katika mafumbo kwake, hawezi kulielewa kamwe, linamshinda akili, hajui kitu hata kidogo juu yake. Bali, kwa kanisa, ni asali mwambani, ni furaha isiyotamkika, ni dhamana iliyobarikiwa, ni nanga ya nafsini, ni tumaini na tegemeo letu, ni Mwamba wenye Imara, loo, ni kila kilicho chema. Kwa kuwa mbingu na nchi zitapita, bali Neno la Mungu halitapita kamwe.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:
Yoeli 2:28
Waefeso 1:1-5
I Wakorintho 12:13
1 Petro 1:20
Ufunuo 17:8
Ufunuo 13