UJUMBE: 62-1231 Lile Shindano
- 24-1231 Lile Shindano Na Ushirika
- 24-1229 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya I
- 22-1231 Lile Shindano & Ushirika
- 16-1231 Lile Shindano
Mpendwa Bibi arusi,
Natumai kila mmoja wenu alikuwa na Krismasi nzuri pamoja na marafiki na familia yako. Ninayo shukurani jinsi gani leo kujua ya kwamba Bwana wetu Yesu hajakwama horini kama ulimwengu unavyomwona Yeye leo, lakini yu hai na Yuko katikati ya Bibi-arusi Wake, akijifunua Mwenyewe kupitia Sauti Yake kuliko hapo awali, BWANA ASIFIWE.
Kama nilivyokwishatangaza, ningependa tuwe na Ushirika kwa mara nyingine tena katika nyumba zetu/makanisa yetu katika mkesha wa Mwaka Mpya, tarehe 31 Desemba. Kwa wale wanaotaka kushiriki, tutasikiliza Ujumbe, 62-1231 Lile Shindano, na kisha kuingia moja kwa moja kwenye ibada ya Ushirika, ambayo Ndugu Branham anaitambulisha wakati wa kuhitimisha Ujumbe.
Kwa waamini walio eneo hili, tutaanza kanda saa 1:00 MOJA JIONI. Hata hivyo, kwa wale walio katika maeneo ya majira tofauti, tafadhali uanzeni Ujumbe kwa wakati unaofaa kwenu. Baada ya Ndugu Branham kuleta Ujumbe wake wa Mkesha wa Mwaka Mpya, tutasimamisha kanda mwishoni mwa aya ya 59, na kuwa na takriban dakika 10 za muziki wa piano wakati tunapokula Meza ya Bwana. Kisha tutaendeleza tena kanda Ndugu Branham anapofunga ibada. Kwenye kanda hii, yeye anaiacha sehemu ya ibada ya Kutawadhana miguu, ambayo na sisi pia tutaiacha.
Maagizo ya jinsi ya kupata divai, na jinsi ya kuoka mkate wa Ushirika yanaweza kupatikana katika anuani zilizo hapa chini. Unaweza kucheza au kupakua sauti kutoka kwenye tovuti, au unaweza tu kuicheza ibada kwenye Redio ya Sauti kwenye programu ya Lifeline (ambayo itachezwa kwa Kiingereza saa 1:00 JIONI saa za Jeffersonville.)
Wakati tunapoukaribia mwaka mwingine wa huduma kwa Bwana wetu, hebu na tuonyeshe upendo wetu Kwake kwa kuisikia kwanza Sauti Yake, na kisha tushiriki Meza Yake. Utakuwa wakati wa utukufu na mtakatifu jinsi gani wakati tunapoyaweka upya maisha yetu kwa ajili ya Huduma Yake.
Mungu awabariki,
Ndugu Joseph