24-0825 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

UJUMBE: 65-0801E Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

BranhamTabernacle.org

Tai Wapendwa,

Palipo na Mzoga, tai wanakusanyika. Ni wakati wa jioni, na unabii umetimizwa mbele ya macho yetu. Mioyo yetu inawaka ndani yetu tunapomwalika katika makanisa yetu, nyumba zetu, na vibanda vyetu vya udongo huko msituni. Atazungumza nasi na kulifunua Neno Lake. Tunaona njaa na kiu ya Mungu zaidi.

Yeye amechagua njia ile Neno lake lingetujia; ni kwa nabii Wake, ambaye Yeye alimchagua tangu zamani na kumtenga tangu zamani. Alimchagua William Marrion Branham kuwa mtu wa wakati huu kuwashika wateule Wake wa wakati huu, SISI, Bibi-arusi Wake.

Hakuna mtu mwingine anayeweza kupachukua mahali pake. Tunapenda jinsi anavyojieleza; ii, siho, iyo, pepa, dafuta, ni Mungu akizungumza masikioni mwetu. Mungu, akinena kupitia midomo ya mwanadamu, akifanya yale hasa Yeye aliyosema angefanya. Hilo latosha!

Mungu aliongoza mikono na macho yake katika maono. Yeye hakuweza kusema kitu chochote ila kile alichokuwa akikiangalia. Mungu alitawala kabisa ulimi wake, kidole, hata kila kiungo cha mwili wake kilikuwa katika utawala mkamilifu wa Mungu. Alikuwa ndiye kinywa chenyewe cha Mungu.

Mungu alijua kimbele katika wakati huu kanisa lingeingia kwenye mchafuko. Kwa hiyo, Yeye alikuwa na nabii Wake tayari kwa ajili ya wakati wetu, kumwita na kumwongoza Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa kwa Neno Lake lililothibitishwa.

Katika mpango Wake mkuu, Yeye pia alijua angempeleka nabii Wake Nyumbani kabla ya Kuja Kwake, kwa hiyo Alihakikisha ameirekodi Sauti Yake na kuihifadhi, ili Bibi-arusi Wake mteule daima wangeweza kuwa na Bwana Asema Hivi kiganjani. Basi wasingekuwa na swali kamwe. Hakukuwa na fasiri iliyohitajiwa, Neno safi na bikira tu waliloweza kulisikia wakati wote.

Alijua kungekuwa na sauti nyingi na machafuko mengi katika siku za mwisho.
Wiki tatu zilizopita amezungumza nasi na kuweka saa tunayoishi. Alituambia kuhusu manabii wa uongo ambao wangetokea na kuwadanganya wateule, kama yamkini.

Jinsi gani huyu mungu wa kizazi hiki alivyoipofusha mioyo ya watu. Na jinsi ambavyo Mungu Mwenyewe alisema kupitia kwa nabii Zake ya kwamba mambo haya yangetukia katika Wakati huu wa Laodikia. Alituambia hakuna kitu ambacho kimeachwa bila kutimia.

Amejitambulisha Mwenyewe mbele zetu kwa mambo yale yaliyotabiriwa kumhusu Yeye kuyafanya katika siku hii. Matendo yake yenyewe yametuthibitishia Yeye ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Ni Sauti ya Mungu, ikizungumza na, na kuishi ndani ya, Bibi-arusi Wake.

Je! unaamini Ujumbe huu ni Waebrania 13:8? Kuwa ni Neno lililo hai? Kuwa ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili? Basi unabii utatendeka Jumapili hii ikiwa utaamini na kutii.

Kitu fulani kitakuwa kikitendeka ulimwenguni kote ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya dunia. Mungu atakuwa akinena kupitia midomo ya mwanadamu, akizungumza na Bibi-arusi Wake kila mahali ulimwengu mzima wote kwa wakati mmoja. Atatufanya tuwekeane mikono na kuombeana mmoja kwa mwingine wakati yeye anapotuombea sisi wote.

Ninyi mlio huko nje kwenye simu, kama mmekwisha amini kwa moyo wenu wote, wahudumu wakiwa wanawawekea mikono, na wapendwa wenu wakiwawekea mikono, kama mnaamini kwa moyo wenu wote ya kwamba imekwisha, imekwisha.

Chochote tunachohitaji, Mungu atatupa ikiwa tu tutaamini… NASI TUNAAMINI. SISI NDIO BIBI-ARUSI WAKE MWAMINIFU. Itatendeka. Nguzo ya Moto itakuwa popote tutakapokusanyika na kumpa kila mmoja wetu chochote tunachohitaji, ni BWANA ASEMA HIVI.

Jalia Nuru ile ile Takatifu tunayoiangalia papa hapa kanisani, jalia imwangukie kila mmoja, na kila mtu, na jalia waponywe wakati huu. Tunamkemea adui, Ibilisi, katika Uwepo wa Kristo; tunamwambia huyo adui, ya kwamba ameshindwa na—na mateso yaliyompata badala yetu, yale mauti ya Bwana Yesu na ushindi wa ufufuo katika siku ya tatu; na ushuhuda Wake uliothibitishwa ya kwamba Yeye yuko hapa kati yetu usiku wa leo, akiwa hai, baada ya miaka elfu moja mia tisa. Jalia Roho wa Mungu aliye hai aujaze kila moyo kwa imani na nguvu, na nguvu za kuponya kutokana na kufufuka kwa Yesu Kristo, Ambaye ametambulikana sasa kwa Nuru hii kuu inayolizunguka kanisa, katika Uwepo Wake. Katika Jina la Yesu Kristo, tujalie kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Wewe ni Bibi-arusi Wake. Hakuna kinachoweza kuliondoa hilo kutoka kwako, HAKUNA CHOCHOTE. Shetani ameshindwa. Unaweza kuhisi una kijiko tu kilichojaa Yeye, hicho ndicho tu unachohitaji, NI HALISI. NI YEYE. WEWE NI WAKE. NENO LAKE HALIWEZI KUSHINDWA.

Liamini, likubali, lishikilie, haliwezi kushindwa. Huna nguvu lakini una mamlaka yake. Sema, “Nimeichukua Bwana, ni yangu, Wewe umenipa hiyo nami sitamwacha Shetani aichukue.”

Tutakuwa na wakati ulioje. Hakuna mahali pengine ningependa kuwa. Roho Mtakatifu atatuzunguka sote. Tumepewa Ufunuo zaidi. Mioyo iliyovunjika. Kila mtu aliponywa. Hatuwezije kusema, “Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, nayo haiwaki sasa, kujua kwamba sasa tuko katika uwepo wa Yesu Kristo aliyefufuka, utukufu na sifa vina yeye milele.

Ndugu. Joseph Branham.

Tunaalika ulimwengu wote uje kuungana nasi:

Muda: saa 06:00 SITA MCHANA masaa ya Jeffersonville(ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika mashariki)
Ujumbe: 65-0801E Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo: 22:17-18
Zaburi: 16:10 / Sura ya 22 / 35:11 / 41:9
Zekaria 11:12 / 13:7
Isaya: 9:6 / 40: 3-5 / 50:6 / 53:7-12
Malaki: 3:1 / sura ya 4
Yohana 15:26
Luka Mt: 17:30 / 24:12-35
Warumi: 8:5-13
Waebrania: 1:1 / 13:8
Ufunuo: 1:1-3 / Sura ya 10