24-0707 Je! Mungu Habadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

UJUMBE: 65-0418E Je! Mungu Habadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Wa Mapenzi Makamilifu,

Siku imeenda sana na Kuja kwa Bwana kumekaribia. Mlango unajifunga na wakati unaisha, ikiwa bado haujaisha. Muda umeenda sana kushangaa-shangaa; wa kuwa kama unyasi unaotikiswa na upepo; wa kuwa na masikio ya utafiti. Ni wakati wa kufanya maamuzi dhahiri. Yanilazimu nifanye nini ili kuwa Bibi-arusi Wake?

Je! Mungu hubadilisha Nia Yake kuhusu Neno Lake? KAMWE. Basi tunapaswa kujitahidi kila siku, kwa moyo na roho zetu zote kuwa katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU. Inatupasa kujikabidhi wenyewe kwenye mapenzi Yake na Neno Lake. Usilihoji kamwe, liamini tu na ulikubali. Usijaribu kutafuta njia ya kuliepa. Lichukue tu jinsi lilivyo.

Nabii anatuambia katika Ujumbe huu ya kwamba kusudi lake lote ni kutuonyesha ya kwamba Mungu hana budi kutimiza Neno Lake kusudi adumu kuwa Mungu, lakini watu wengi wanataka kuliepa, na kupitia njia nyingine. Wanapofanya jambo hilo, wanajikuta wakipiga hatua, na Mungu akiwabariki, bali wanafanya kazi katika mapenzi Yake ya kuruhusia na wala si katika mapenzi Yake makamilifu, ya Kiungu.

Nabii anaturudisha kwenye Neno na kutupa mifano ya kutazama, kujifunza, na kutukumbusha, Mungu HABADILISHI Nia Yake wala njia Yake, Yeye ni Mungu wala HABADILIKI.

Sasa, tunaona ya kwamba wote hawa wawili walikuwa watu wa kiroho, wote wawili walikuwa manabii, wote wawili walikuwa wameitwa. Naye Musa, akiwa moja kwa moja kazini, akiwa na Nguzo ya Moto mpya mbele yake kila siku, Roho wa Mungu akiwa juu yake, akiwa kazini. Huyu hapa mtumishi mwingine wa Mungu anakuja, aliyeitwa na Mungu, aliyechaguliwa na Mungu, nabii ambaye anajiliwa na Neno la Mungu. Hapa ndipo penye hatari. Hakuna mtu angaliweza kukataa mtu huyo kuwa ni wa Mungu—wa Mungu, kwa maana Biblia ilisema Roho wa Mungu alinena naye, naye alikuwa nabii.

Bwana, jinsi gani hilo linavyofanana sana? Ninawezaje kujua, wakati WOTE wawili walikuwa manabii? Wote wawili ni watu waliojazwa na Roho walioitwa na Mungu, waliochaguliwa na Mungu; manabii wa Mungu ambao Neno la Mungu huwajia. Wote wawili wakisema Roho Mtakatifu anawaongoza.

Hebu tusome na tujifunze nukuu chache kwa makini sana kuhusu kile ambacho malaika-mjumbe wa saba wa Mungu asemacho. Tunataka kile yeye anachosema; si kile kanisa linachosema, kile ambacho Daktari Jones asemacho, ama kile mtu mwingine yeyote asemacho. Sisi Tunataka kile BWANA ASEMA HIVI asemacho kupitia nabii Wake.

Musa, akiwa nabii aliyechaguliwa na Neno la Bwana, alithibitishwa ya kwamba alikuwa amechaguliwa kuwa kiongozi wao kwa ajili ya majira hayo, na ya kwamba Ibrahimu alikuwa ameahidi mambo haya yote,…

Hakuna mtu angaliweza kupachukua mahali pa Musa. Haidhuru ni Kora wangapi walioinuka, na ni Dathani wangapi; ilikuwa ni Musa, Mungu alikuwa amemwita, kwa vyo vyote.

Musa ndiye ambaye Mungu alikuwa amemchagua kuwaongoza watu. Wanaume wengine waliinuka na kusema wamepakwa mafuta, watu waliojazwa na Roho Mtakatifu pia. Mungu alikuwa amewaita waongoze pia. Lakini Musa alikuwa ndiye kiongozi wa Mapenzi Makamilifu ya ya Mungu ya asili wa kuwaongoza.

Lakini, na iwapo watu hawatatembea katika mapenzi Yake makamilifu, Yeye ana mapenzi ya kuruhusia atakayokufanya uende kwayo. Angalia, Yeye hurusu jambo hilo, kweli, bali atalifanya litende kazi kwa utukufu Wake, katika mapenzi Yake makamilifu. Sasa kama mngetaka…

Hakuna anayetaka kuwa katika mapenzi ya Mungu yakuruhusia. Bibi-arusi wa kweli anataka kuwa katika mapenzi Yake makamilifu, wakati wote, haijalishi gharama.

Kuna kutokubaliana kwingi, mawazo mengi, mkanganyiko mwingi, maoni mengi, juu ya umuhimu wa kucheza kanda.

Sote tunajua hili ndilo suala lenyewe ambalo limewatenganisha waaminio wa Ujumbe leo. Tunajua Bibi-arusi LAZIMA, NA ATA-ungana pamoja; hilo ni Neno.

Kuna watu waliojazwa na Roho, walioitwa na Mungu katika Kanisa leo. Wao ni watu waliotiwa mafuta na Mungu walioitwa kuhubiri Ujumbe huu. Lakini hakuna hata mmoja wao ambaye tunaweza sote kukubaliana kwake.

Wanawezaje wao kuwa ndio wa kumuunganisha Bibi-arusi? Je, twaweza kuungana kwenye huduma yao? Kwa kweli wao wameitwa kuliongoza kundi lao, lakini kuwarudisha hao kwenye MPANGO WA ASILI wa Mungu. kwa KIONGOZI WAKE. Kwa NABII WAKE. Sio kwenye huduma yao.

Kama wao hawakufundishi kwamba ile Sauti iliyo kwenye kanda hiyo ndio UNAPASWA uifuate, na lazima uamini kuwa ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia, wako tu katika mapenzi Yake ya kuruhusia.

Iwapo wanakuambia kuwa Ndio Sauti iliyo muhimu zaidi, nao wanaamini kweli hivyo, basi inakuwaje hawabonyezi play kila wakati mnapokutana?

Ikiwa unataka kuwa na hakika, NA HAKIKA, kwamba uko katika mapenzi Yake makamilifu, kuna NJIA moja tu ya HAKIKA. Ni kusikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda.

Muda si muda, kanda inaangukia nyumbani mwao. Imelenga penyewe, basi. Kama yeye ni kondoo, anakuja moja kwa moja Nalo. Kama yeye ni mbuzi, anapiga hiyo kanda teke.

Lazima niwe na HAKIKA. Siwezi, na sita-bahatisha hata kidogo kwa kikomo changu cha Milele. NAJUA Sauti iliyo kwenye kanda ni Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi. NAJUA Hiyo haikosei. NAJUA Ilithibitishwa na Nguzo ya Moto. NAJUA Ndiye ambaye Mungu alimchagua kumwongoza Bibi-arusi Wake. NAJUA ya kwamba Sauti hiyo ndiyo Sauti pekee inayoweza na itakayo muunganisha Bibi-arusi. NAJUA itakuwa ni Sauti hiyo nitakayoisikia ikisema “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu”.

LAZIMA NIBONYEZE PLAY niisikie hiyo Sauti. Unaalikwa kuja kuungana nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia: 65-0418E Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Ndugu. Joseph Branham

Tutauanza Ujumbe huu kwenye aya ya 61.

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Kutoka sura ya 19
Hesabu 22:31
Mathayo Mt. 28:19
Luka 17:30
Ufunuo sura ya 17