UJUMBE: 65-1205 Mambo Yatakayokuwapo
- 25-0803 Mambo Yatakayokuwapo
- 21-1205 Mambo Yatakayokuwapo
- 21-1204 Unyakuo
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 20-0719 Mambo Yatakayokuwapo
- 18-0114 Mambo Yatakayokuwapo – Preliminari
- 15-1206 Mambo Yatakayokuwapo
Mpendwa Sifa za Mungu,
Kila Neno lililonenwa katika Ujumbe huu ni barua ya mahaba kwa Bibi-arusi Wake. Kuwazia kwamba Baba yetu wa Mbinguni Yeye anatupenda sana, si tu kwamba Yeye alitaka tulisome Neno Lake, bali Alitaka tuisikie Sauti Yake ikizungumza na mioyo yetu ili aweze kutuambia: “Wewe ndiye usia Wangu ulio hai, sifa Yangu iliyo hai, ambayo ninaweza kuionyesha kwa ulimwengu.”
Kisha kuwazia kwamba baada ya dhabihu zake zote alizotoa hapa duniani, maisha aliyoishi, njia aliyofuata. Aliomba jambo moja:
“Ili nilipo Mimi, nao wawepo.” Yeye aliomba ushirika wetu. Hicho ndicho kitu pekee alichomwomba Baba katika maombi, ushirika wenu milele.
Nilipo Mimi, “Neno Lake,” hatuna budi kuwapo pia, kupokea ushirika Wake, ushirika Wake, milele. Kwa hiyo, ni lazima tuishi kwa kila Neno Yeye alilonena nasi kwenye kanda ili tuwe Bibi-arusi Neno Bikira Wake, ambalo linatufanya kuwa sehemu ya Bwana-arusi.
Huo ndio UFUNUO wa Yesu Kristo katika wakati huu. Si vile Yeye alivyokuwa katika wakati mwingine, Yeye ni nani SASA HIVI. Neno la siku hii. Mungu yuko wapi leo. Huo ndio Ufunuo wa siku hii. Sasa unakua katika Bibi-arusi, ukitufanya kufikia kimo kikamilifu cha wana na binti.
Tunajiona wenyewe katika Neno Lake. Tunajua sisi ni nani. Tunajua tuko katika mpango Wake. Hii ndiyo Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Tunajua Unyakuo umekaribia. Hivi karibuni wapendwa wetu wataonekana. Kisha tutajua: Tumewasili. Sote tunaenda Mbinguni…ndiyo, Mbinguni, mahali halisi tu kama hapa.
Tunaenda mahali halisi ambapo tutafanya mambo, ambapo tutaenda kuishi. Tutafanya kazi. Tutapafurahia. Tutaishi. Tunaenda kwenye Maisha, kwenye Maisha halisi ya Milele. Tunaenda Mbinguni, paradiso. Kama tu vile Adamu na Hawa walivyoshughulika, na kuishi, na kula, na kufurahia, katika bustani ya Edeni kabla dhambi haijaingia, tuko njiani tukirudi moja kwa moja kule tena, moja kwa moja, kurudi moja kwa moja. Adamu wa kwanza, kwa njia ya dhambi, alitutoa. Adamu wa Pili, kwa njia ya haki, anaturudisha kutuingiza ndani tena; anatuhesabia haki na kuturudisha ndani.
Mtu yeyote anawezaje kuliweka katika maneno Kile jambo hili linachomaanisha kwetu sisi? Uhalisia kwamba tunakwenda kwenye paradiso ambapo tunaishi katika umilele wote pamoja. Hakuna huzuni tena, maumivu au kilio, ni ukamilifu tu juu ya ukamilifu.
Mioyo yetu inafurahi, roho zetu zinawaka moto ndani yetu. Shetani anazidi kutupa presha kila siku, lakini bado tunafurahi. Kwa nini:
• TUNAJUA, SISI NI NANI.
• TUNAJUA, HATUJA, NA HATUTA, MWANGUSHA YEYE.
• TUNAJUA, TUKO KATIKA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.
• TUNAJUA, YEYE AMETUPA UFUNUO WA KWELI WA NENO LAKE.
Ndugu Joseph, unaandika jambo lile lile kila wiki. UTUKUFU, nitaliandika kila wiki kwa sababu Yeye anakutaka ujue jinsi gani anavyokupenda. Wewe ni nani. Ni wapi unakokwenda. Hasi inakuwa chanya. Wewe ni Neno ukifanyika Neno.
Mpendwa ulimwengu, njooni muungane nasi Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville, (ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) kwenye mawasiliano ya simu, si kwa sababu “Mimi” ninawaalika, bali kwa sababu “YEYE” anawaalika. Si kwa sababu “Mimi” niliichagua kanda, bali kulisikia Neno pamoja na sehemu ya Bibi-arusi ulimwenguni kote kwa wakati mmoja.
Je! tunaweza kutambua kwamba inawezekana kwa Bibi-arusi kuisikia Sauti ya Mungu ulimwenguni kote, wote kwa wakati ule ule hasa? Huyo hana budi kuwa ni Mungu. Mungu alimfanya nabii afanye hivyo wakati ule malaika Wake alipokuwa hapa duniani. Yeye alimuhimiza Bibi-arusi kuungana katika maombi, WOTE KWA WAKATI ULE ULE WA JEFFERSONVILLE, saa 3:00, 6;00, 9:00; hilo ni kuu jinsi gani sasa hivi, kwamba Bibi-arusi anaweza kuungana kama KITU KIMOJA kuisikia Sauti ya Mungu ikinena nao wote kwa wakati mmoja?
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: Mambo Yatakayokuwapo 65-1205
Maandiko:
Mathayo 22:1-14
Yohana 14:1-7
Waebrania 7:1-10