24-1229 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya I

UJUMBE: 60-1231 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya I

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watakatifu Waliovikwa Mavazi Meupe,

Wakati tunapoisikia Sauti ya Mungu ikisema nasi, jambo fulani hutokea ndani kabisa ya nafsi zetu. Utu wetu wote unabadilishwa na ulimwengu unaotuzunguka unaonekana kufifia.

Mtu anawezaje kueleza kile kinachotendeka katika mioyo yetu, akili zetu, na nafsi zetu, wakati Sauti ya Mungu inapofunua Neno Lake kwa kila Ujumbe tunaousikia?

Kama vile nabii wetu, tunahisi tumenyakuliwa hadi kwenye mbingu ya tatu nazo nafsi zetu zinaonekana kuuacha mwili huu upatikanao na mauti. Hakuna maneno ya kueleza kile tunachojisikia Mungu anapotufunulia Neno Lake kuliko hapo awali.

Yohana aliwekwa kwenye kisiwa cha Patmo naye akaombwa aandike kile alichokiona na kukiweka kwenye kitabu kiitwacho Ufunuo, ili kiende katika nyakati zote. Siri hizo zilikuwa zimefichwa hadi zilipofunuliwa kwetu kupitia malaika-mjumbe Wake wa 7 aliyemchagua.

Kisha Yohana akasikia Sauti iyo hiyo juu yake naye akanyakuliwa hadi katika mbingu ya tatu. Sauti hiyo ilimwonyesha nyakati za kanisa, kuja kwa Wayahudi, kumwagwa kwa yale mapigo, Kunyakuliwa, Kuja mara ya pili, Utawala wa Miaka Elfu, na Makazi ya Milele ya waliookolewa Wake. Alimchukua na kumwonyesha Yohana kitu hicho chote kikifanyiwa mazoezi kama Yeye alivyosema angefanya.

Lakini Yohana alimwona nani wakati alipoyaona yale mazoezi? Hakuna kweli aliyejua hadi leo hii.

Kitu cha kwanza alichoona katika kule Kuja kilikuwa ni Musa, aliyewawakilisha watakatifu waliokufa ambao wangefufuliwa; nyakati zote sita walizolala. Lakini si Musa tu peke yake aliyekuwa amesimama pale, bali Eliya alikuwa pale pia.

Yule Eliya aliyekuwa amesimama alikuwa ni nani?

Bali Eliya alikuwako; yule mjumbe wa siku ya mwisho, pamoja na kundi lake, la waliobadilishwa, Walionyakuliwa.

UTUKUFU…HALELUYA… ni nani ambaye Yohana alimuona akiwa amesimama pale?

Si mwingine ila malaika-mjumbe wa 7 wa Mungu, William Marrion Branham, pamoja na KUNDI LAKE LA WALIOBADILISHWA, WALIONYAKULIWA…KILA MMOJA WETU!!

Eliya aliwakilisha watakatifu waliokufa …Ninamaanisha Musa, na kufufuliwa. Eliya aliwakilisha kundi lililohamishwa. Kumbukeni, Musa alikuwa wa kwanza, na kisha Eliya. Eliya alikuwa awe ndiye mjumbe wa siku za mwisho, ili kwa yeye na kundi lake ungekuja ufufuo…ungekuja ninii…vema, ungekuja Unyakuo, namaanisha. Musa alileta ufufuo na Eliya akaleta kundi Lililonyakuliwa. Na, hapo, wote wawili waliwakilishwa papo hapo.

Nena kuhusu kufichua, kufunua, na Ufunuo.

Hii hapa! Tunaye moja kwa moja pamoja nasi sasa, Roho Mtakatifu, Yesu Kristo, yeye yule jana, leo, na hata milele. Wewe ni…Anawahubiria, anawafundisha, anajaribu kuwafanya muone yaliyo mema na mabaya. Ni Roho Mtakatifu Mwenyewe akinena kupitia midomo ya wanadamu, akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, akijaribu kuonyesha rehema na neema.

Sisi ndio wale Watakatifu Waliovikwa Mavazi Meupe ambao malaika Wake aliwaona wakija kutoka kote ulimwenguni kula Mkate wa Uzima. Tumeposwa na kuolewa Naye nasi tumehisi busu Lake la posa mioyoni mwetu. Tumetoa kiapo Kwake, na kwa Sauti Yake tu. Hatuna, nasi hatutajitia unajisi kwa sauti nyingine yoyote.

Bibi-arusi anajitayarisha kupanda juu kama Yohana alivyofanya; kuingia Uweponi mwa Mungu. Tutatwaliwa juu kwenye Unyakuo wa Kanisa. Jinsi hilo linavyozizungusha nafsi zetu!

Ni kipi kifuatacho Yeye anachoenda kutufunulia?

Hukumu; jiwe la akiki, na kile linachowakilisha; kazi yake. Yaspi, na mawe yote mbalimbali. Yeye atayachukua haya yote kote kupitia kwa Ezekieli, arudi kwenye Mwanzo, arejee kwenye Ufunuo, aje katikati ya Biblia, ayafungamanishe pamoja; mawe haya yote mbalimbali na rangi.

Ni Roho Mtakatifu yeye yule, Mungu yeye yule, akionyesha ishara zile zile, maajabu yale yale, akifanya jambo lile lile kama Yeye alivyoahidi. Ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo akijiweka mwenyewe tayari kwa kuisikia Sauti Yake.

Tunawakaribisha kuungana nasi tunapoingia katika ulimwengu wa roho saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville (Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki), kumsikia Eliya, mjumbe wa Mungu kwa wakati huu wa mwisho, akifunua siri ambazo zimefichwa katika nyakati zote.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: 60-1231 Ufunuo, Mlango wa Nne Sehemu ya I

. Tafadhali ukumbukeni Ujumbe wetu wa Mwaka Mpya, Jumanne usiku: Lile Shindano 62-1231. Hakuna njia bora ya kuuanza Mwaka Mpya.