UJUMBE: 65-0801M Mungu Wa Wakati Huu Mwovu
- 24-0818 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu
- 23-0129 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu
- 21-1003 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu
- 20-0216 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu
Wapendwa Wakamilifu,
Sauti tunayosikia kwenye kanda ndio Sauti ile ile iliyolitangaza Neno Lake katika Bustani ya Edeni, juu ya Mlima Sinai, na kwenye Mlima wa Kugeuzwa Sura. Inasikika leo kwa Ufunuo kamili na wa mwisho wa Yesu Kristo. Inamwita Bibi-arusi Wake atoke, ikimtayarisha kwa ajili ya Kunyakuliwa. Bibi-arusi analisikia, analikubali, analiishi, naye amejiweka mwenyewe tayari kwa kuliamini.
Hakuna mtu anayeweza kuliondoa Hilo kutoka kwetu. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Roho wake anawaka na kuangaza ndani yetu. Yeye ametupa Uzima Wake, Roho Wake, naye Anaudhihirisha Uzima Wake ndani yetu. Tumefichwa ndani ya Mungu nasi Tunalishwa kwa Neno lake. Shetani hawezi kutugusa. Sisi hatuwezi kuondoshwa. Hakuna kinachoweza kutubadilisha. Kwa Ufunuo, sisi tumekuwa BIBI-ARUSI NENO.
Wakati Shetani anapojaribu kutuangusha, tunamkumbusha tu jinsi Mungu anavyotuona. Anapotutazama, anachokiona tu ni dhahabu SAFI. Haki yetu ni haki YAKE. Sifa zetu ni sifa ZAKE mwenyewe zenye utukufu. Utambulisho wetu unapatikana katika Yeye. Kile alicho Yeye, sasa tunakionyesha. Kile alicho nacho Yeye, TUNAKIDHIHIRISHA SASA.
Jinsi gani Yeye anavyopenda kumwambia Shetani, “Sioni dosari yoyote ndani Yake; Yeye ni MKAMILIFU. Kwangu mimi, Yeye ni Bibi-arusi Wangu, amejaa utukufu ndani na nje. Tangu mwanzo hata mwisho, Yeye ni Kazi Yangu, na Kazi Zangu zote ni kamilifu. Kwa kweli, ndani Yake kumejumlishwa na kudhihirishwa hekima na kusudi Langu la milele”.
“Nimemwona Bibi-arusi Wangu anayependeza anastahili. Kama vile dhahabu inavyofulika, Yeye amestahimili mateso kwa ajili Yangu. Yeye hajapatana, kukunjwa, au kuvunjwa, bali amefanywa kitu chenye uzuri. Majaribu na majaribio yake ya maisha haya yamemfanya Yeye kuwa Bibi-arusi wangu kipenzi”.
Je! hivyo si kama tu Bwana? Anajua jinsi ya kututia moyo. Anatuambia, “Msivunjike moyo kamwe, bali jipeni moyo”. Anaona kazi zetu za upendo Kwake. Anaona kile kinachotulazimu kupitia. Anaona vita vya kila siku tunavyovivumilia. Kwa vile anavyotupenda sisi kupitia kila moja ya hayo.
Machoni pake sisi ni wakamilifu. Ametungojea sisi tangu mwanzo wa wakati. Hataruhusu lolote litutokee isipokuwa ni kwa manufaa yetu. Anajua tutashinda kila kizuizi ambacho Shetani anachoweka mbele yetu. Anapenda kumthibitishia kwamba sisi ni Bibi-arusi Wake. Hatuwezi kuondoshwa. Sisi ndio Wale ambao amekuwa akingojea tangu mwanzo. Hakuna kinachoweza kututenganisha Naye na Neno Lake.
Alitutumia malaika-mjumbe wake mwenye nguvu ili aweze kusema nasi mdomo kwa sikio. Aliirekodi ili kusiwe na maswali yale aliyosema. Alikuwa ameihifadhi ili Bibi-arusi Wake awe na kitu cha kula mpaka Yeye ajapo kumchukua.
Haijalishi ikiwa wengine wanatuelewa vibaya na wanatutesa kwa kusema sisi ni “Watu wa Kanda”, tunafurahi, kwa kuwa hili ndilo Yeye alilotufunulia sisi tufanye. Wengine hawana budi kufanya kama wanavyohisi kuongozwa kufanya, lakini kwetu sisi, hatuna budi kuungana pamoja chini ya Sauti moja, Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda.
Hatuwezi kufahamu kitu kingine chochote. Hatuwezi kuelewa kitu kingine chochote. Hatuwezi kufanya kitu kingine chochote. Hatuwezi KUKUBALI kitu kingine chochote. Sisi hatupingani na kile waamini wengine wanachohisi wanaongozwa na Bwana kufanya, lakini hiki ndicho Mungu AMETUONGOZA SISI KUFANYA, nasi ni lazima TUDUMU hapa.
Tumeridhika. Tunalishwa na Sauti ya Mungu. Tunaweza kusema “amina” kwa KILA NENO tunalosikia. Hii ndiyo Njia Mungu aliyotuandalia. Hatuwezi kufanya kitu kingine chochote.
Ninapenda tu kuwaalika kila mmoja kuja kuungana nasi. Tunazifanya ibada jinsi vile tu Ndugu Branham alivyozifanya wakati yeye alipokuwa hapa duniani. Ingawa yeye hayuko hapa katika mwili, jambo kuu ni kile Mungu alichomwambia Bibi-arusi Wake kwenye kanda.
Yeye aliualika ulimwengu kuwa sehemu ya MAWASILIANO ya simu, lakini tu ikiwa wao WALITAKA KUFANYA HIVYO. Aliwafanya wakusanyike popote walipoweza kuisikia Sauti ya Mungu ikizungumza nao wote kwa wakati mmoja. Hivyo ndivyo nabii wa Mungu alivyofanya wakati huo, kwa hiyo mimi ninajaribu tu kufanya yale yeye aliyofanya kama mfano wangu.
Hivyo, unaalikwa kuja kuungana nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunapomsikiliza mjumbe wa Mungu akituletea Ujumbe: Mungu Wa Wakati Huu Mwovu 65-0801M.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:
Mathayo Mt. sura ya 24/27:15-23
Mtakatifu Luka 17:30
Yohana Mtakatifu 1:1 / 14:12
Matendo 10:47-48
1 Wakorintho 4:1-5 / sura ya 14
2 Wakorintho 4:1-6
Wagalatia 1:1-4
Waefeso 2:1-2 / 4:30
2 Wathesalonike 2:2-4 / 2:11
Waebrania sura ya 7
1 Yohana Sura ya 1 / 3:10 / 4:4-5
Ufunuo 3:14 / 13:4 / Sura ya 6-8 na 11-12 / 18:1-5
Mithali 3:5
Isaya 14:12-14