UJUMBE: 65-0725E Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
- 24-0811 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
- 23-0122 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
- 21-0926 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
- 20-0419 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
- 18-1028 Nini Kinachovutia Kule Mlimani? -Preliminari
- 17-0122 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?
Wapendwa Jamii Moja,
Tuko chini ya matarajio na matazamio makubwa. Twaweza kulihisi jambo hilo, jambo fulani linaenda kutukia. Tunataka kuungana pamoja ili kuisikia Sauti Yako; kupata cho chote na kila kitu unachosema. Tunalitaka. Tunataka kuwa sehemu Yake. Tunaamini kila Neno.
Nini kinatendeka? Mungu anafanya historia. Mungu anatimiza unabii. Hiyo Daima husababisha kuvutia macho. Huwakusanya wapinzani wote, wale nderi wa Ujumbe tuliousikia Jumapili iliyopita, lakini pia linawakusanya Tai Wake pamoja. Kwa maana palipo Mzoga, hapo Tai watakusanyika.
Ni jibu la unabii wa nabii, angalieni, nitawapelekea Eliya nabii. Mungu anamthibitisha nabii Wake. Ni Mungu akitimiza unabii. Mungu akifanya historia, akilitimiza Neno Lake. Ni ule Mvuto wa Tatu ukitimia.
Najua yaonekana kama yote Nifanyayo tu ni kutokukubaliana na viongozi wote wa makanisa, naonekana kulaumu chochote wanachofanya, lakini ninaamini sisi ndio lile kundi fulani la watu ambao wamechaguliwa tangu asili Kubonyeza Play na kuusikia Ujumbe huo, Sauti hiyo, na kuufuata.
Sisi hatujali umati wa watu. Hatujali lawama za asiyeamini. Hatubishani nao. Tuna wajibu mmoja, huo ni kuamini na kupata kila sehemu Yake tuwezayo; tuiingize ndani kama Mariamu aliyeketi miguuni pa Yesu.
Hatuvutiwi na kitu kingine chochote. Hatuhitaji kitu kingine chochote. Tunaamini kwamba kila kitu tunachohitaji kusikia kiko kwenye kanda. Neno la Mungu halihitaji fasiri yoyote.
Ile ahadi imetimizwa. Ni wakati gani, bwana, na mvuto huu ni wa nini? Mungu akitimiza Neno Lake! Ni yeye yule jana, leo, na hata milele.
Ni mvuto gani? Mungu, kwa mara nyingine tena, akilitimiza Neno Lake, akiwakusanya watu Wake pamoja makanisani, vituo vya mafuta, majumbani, wamekusanyika kuzunguka vipaza sauti vidogo kutoka kote nchini, kote kote hata kwenye Pwani ya Magharibi, kule juu kwenye milima ya Arizona, chini kwenye mabonde ya Texas, mbali sana hata Pwani ya Mashariki; kote nchini na ulimwenguni kote.
Tuko umbali wa masaa mengi katika wakati, lakini Bwana, tuko pamoja kama jamii moja, waamini, tukingojea Kuja kwa Masihi. Ninajaribu kufuata na kufanya vile tu nabii Wako alivyofanya ili kumuunganisha Bibi-arusi Wako wakati yeye alipokuwa hapa. Kile yeye alichokifanya ndio mfano wangu.
Hatuna nafasi ya kumketisha kila mmoja hapa kwenye Maskani ya Branham, kwa hivyo inatulazimu tu kuwatumia Neno kwa njia ya simu, kama vile yeye alivyofanya wakati huo. Tumekusanyika hapa, Jeffersonville, katika makanisa yetu ya nyumbani, tukingojea Kuja kwa Bwana.
Umetoka kutuambia kutakuwa na wengi katika siku hizi za mwisho ambao watajaribu kukufanyia wewe kazi bila ya kuwa mapenzi Yako makamilifu. Kutakuwa na wengi ambao watatiwa mafuta na Roho Mtakatifu wa kweli, lakini watakuwa waalimu wa uongo. Bwana, njia pekee tunayojua KUWA NA HAKIKA ni kudumu na Neno, kudumu na mafundisho ya kanda, kudumu na Sauti Yako iliyothibitishwa.
Tunaamini sisi ndio Uzao Wako uliochaguliwa tangu asili ambao hatuwezi kutenda chochote bali kulifuata; ni zaidi ya maisha kwetu. Twaa maisha yetu, bali usichukue Hilo.
Nini kitatendeka Jumapili hii? Mungu atakuwa akitimiza Neno lake. Kote nchini, kwa njia ya simu, mamia ya watu watawekeleana mikono wao kwa wao kote taifani, pwani kwa pwani, kutoka Kaskazini hata Kusini, Mashariki hata Magharibi.
Hata kutoka nchi za ng’ambo ulimwenguni kote, sote tutawekeana mikono . Ulituambia, “hatuhitaji kadi ya maombi, si lazima kupitia kwenye mstari, tunahitaji tu IMANI.”
Tutainua mikono yetu na kusema, “Mimi ni mwamini.” Yapi yatatendeka?
Shetani, umeshindwa. Wewe u muongo. Na, kama mtumishi wa Mungu, na kama watumishi, tunakuamuru ya kwamba katika Jina la Yesu Kristo, ya kwamba utii Neno la Mungu na utoke ndani ya watu, kwa maana imeandikwa, “Katika Jina Langu watatoa pepo.”
Mungu mpendwa. Wewe ndiye Mungu wa Mbinguni uliyeshinda, siku hiyo kwa mvuto juu ya Mlima Kalvari, magonjwa yote na maradhi na kazi zote za Ibilisi. Wewe ni Mungu! Na watu wameponywa kwa mapigo Yako. Wao ni huru. Katika Jina la Yesu Kristo. Amina.
Mungu ATATIMIZA Neno Lake!
Ningependa kukualika uje kusikiliza pamoja nasi, sehemu ya Bibi-arusi Wake, tunapousikia Ujumbe: 65-0725E Nini Kinachovutia Kule Mlimani? Tutakusanyika Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville.(Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki).
Wengine wanaweza kuhisi sisi tu madhehebu kwa kukusanyika pamoja, kusikiliza Ujumbe uleule kwa wakati mmoja, lakini naamini kama Ndugu Branham angekuwepo hapa, angekuwa anafanya kile hasa tutakachokifanya, kumkusanya Bibi-arusi pamoja, kutoka ulimwenguni kote, kusikiliza kwa wakati mmoja KUMSIKIA YEYE.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko:
Mathayo 21:1-4
Zekaria 9:9 / 14:4-9
Isaya 29:6
Ufunuo 16:9
Malaki 3:1 / Sura ya 4
Yohana Mt 14:12 / 15:1-8
Luka Mt 17:22-30