24-0616 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

UJUMBE: 65-0220 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bi Yesu Kristo,

Kama tungeuliza swali kuhusu cho chote maishani mwetu, yapaswa kuwe na jibu la kweli. Kwaweza kuwe na lililo la karibu nalo, lakini kunapaswa kuwa na jibu la kweli, la moja kwa moja kwa kila swali. Kwa hiyo, basi kila swali linalozuka maishani mwetu, yabidi kuwe na jibu la kweli na sahihi.

Kama tuna swali la Biblia, lazima kuwe na jibu la Biblia. Hatutaki lije kutoka kwenye kundi la watu, kutoka kwenye ushirika wo wote ule, au kutoka kwa mwalimu fulani, au kutoka kwa madhehebu fulani. Tunataka litoke moja kwa moja katika Maandiko. Ni lazima tujue: ni mahali gani pa kweli na sahihi pa Mungu pa kumwabudia?

Mungu alichagua kukutana na binadamu; siyo kanisani, siyo katika madhehebu, siyo katika kanuni ya imani, lakini katika Kristo. Hapo ndipo mahali pekee ambapo Mungu atakutana na mtu, na anapoweza kumwabudia Mungu, ni katika Kristo. Ni mahali hapo pekee. Haidhuru kama wewe ni Mmethodisti, Mbatisti, Mkatoliki, Mprotestanti, hata uwe nani, kuna mahali pamoja tu ambapo unaweza kwa usahihi kumwabudu Mungu, hapo ni katika Kristo.

Mahali pekee sahihi, na alipopachagua Mungu pa kumwabudia Yeye ni katika Yesu Kristo; hiyo ni Njia Yake pekee iliyoandaliwa.

Biblia ilituahidi Tai katika Malaki 4; Nguzo ya Nuru tunayopaswa kuifuata. Atalionyesha kanisa lililokosea Yeye ni Waebrania 13:8, Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele. Pia tumeahidiwa katika Luka 17:30 kwamba Mwana wa Adamu (Tai) atakuwa akijifunua Mwenyewe kwa Bibi-arusi Wake.

Katika Ufunuo 4:7, inatuambia kwamba kulikuwa na Wenye Uhai wanne, na wa kwanza akiwa simba. Mwenye Uhai aliyefuata alikuwa ndama. Kisha, aliyefuata alikuwa ni mwanadamu; Na mwanadamu huyo alikuwa wale watengenezaji, elimu ya mwanadamu, theolojia, na kadhalika.

Lakini Biblia ilisema, wakati wa jioni, yule Mwenye Uhai wa mwisho ambaye alikuwa aje alikuwa Tai arukaye. Mungu angempa Bibi-arusi Wake wa wakati wa mwisho Tai; Mwana wa Adamu Mwenyewe, akijifunua Mwenyewe katika mwili kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Biblia pia inasema mambo yote ya kale, katika Agano la Kale, yalikuwa ni vivuli vya mambo yajayo. Kivuli hicho kinapokaribia, negativu humezwa na picha yenyewe. Kile Kilichotokea wakati huo ni kivuli cha kile ambacho kingetokea leo.

Katika I Samweli 8, Agano la Kale linatuambia Mungu alikuwa amemtoa Samweli nabii kuwaongoza watu. Watu walimwendea na kumwambia wanataka mfalme. Samweli alifadhaika sana hata moyo wake nusura ukome.

Mungu alikuwa anawaongoza watu Wake kupitia kwa nabii huyu aliyewekwa wakfu, aliyethibitishwa kwa Maandiko naye akaona kwamba alikuwa amekataliwa. Akawakusanya watu akawasihi wasimwache Mungu Ambaye alikuwa amewabeba kama watoto, na kuwafanikisha na kuwabariki. Lakini wao wakakaidi.

Wakamwambia Samweli. “Hujakosea katika uongozi wako. Hujakuwa mdanganyifu katika mambo yako ya fedha. Umejaribu uwezavyo kutuweka sawa na Neno la Bwana. Tunaifurahia miujiza, hekima, chakula na ulinzi wa Mungu.Tunauamini. Tunaupenda. Na isitoshe hatutaki kuukosa. Ni kwamba tu tanataka mfalme wa kutuongoza vitani.

Sasa bila shaka tunapotoka kwenda vitani yangali ni makusudio yetu kuacha makuhani watutangulie huku Yuda wakifuata, nasi tutapiga matarubeta na kupiga makelele na kuimba. Hatutarajii kuacha yo yote ya mambo hayo. LAKINI TUNATAKA MFALME AMBAYE NI MMOJA WETU APATE KUTUONGOZA.”
    
Hawa hawakuwa watu wa kimadhehebu wa siku hizo. Kwa kweli hawa walikuwa ni watu waliodai kwamba YEYE ALIKUWA nabii wa Mungu ambaye alichaguliwa na Mungu kuwaongoza.

“Ndiyo, wewe ni nabii. Tunaamini Ujumbe. Mungu anakufunulia wewe Neno Lake, nasi tunalipenda, na isitoshe hatutaki kuukosa, lakini sisi tunamtaka mtu mwingine zaidi YAKO atuongoze; mmoja wetu sisi. Bado tunakusudia kusema tunauamini Ujumbe uliotuletea. Ni Neno. Wewe ni nabii, lakini si wewe tu pekee ama Sauti iliyo muhimu zaidi.”

Wapo watu wazuri ulimwenguni siku hizi, makanisa mazuri. Lakini kuna Bi Yesu Kristo mmoja, na Huyo ni sisi, ndio Wale Yeye anakuja kuwachukua; Bibi-arusi Neno Wake aliye safi ambaye atakayekaa na SAUTI PEKEE YA MUNGU ILIYOTHIBITISHWA NA KUHAKIKISHWA KUWA BWANA ASEMA HIVI.

Ikiwa ungependa kuungana nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)
bado tutakuwa kwenye mawasiliano ya simu ulimwenguni kote tukisikiliza. Hiki ndicho kitakachotendeka.

Njoo juu ya ndugu zangu, dada, rafiki zangu, hapa katika sehemu hii usiku wa leo na huko nje kwenye simu. Majimbo mengi mbalimbali yanasikiliza, mahali pote tokea Pwani ya Mashariki hadi ya Magharibi. Naomba, Mungu Mpenzi, huko chini kuvuka majangwa kule Tucson, huko mbali California, juu huko Nevada na Idaho, kwenda hadi Mashariki na kila mahali, chini huko Texas; wakati mwaliko huu unatolewa, watu wameketi katika—katika makanisa madogo, vituo vya mafuta, majumbani, wakisikiliza. Ee Mungu, jalia mwanamume yule aliyepotea au mwanamke, mvulana au msichana, saa hii, aje Kwako. Lijalie hilo sasa hivi. Tunaomba katika Jina la Yesu, kwamba wataona mahali hapa pa usalama wakati muda ungalipo.

Sasa, Bwana, pambano hili limekwisha kabiliwa, kwamba Shetani, yule laghai mkuu, yeye hana haki ya kumshikilia mtoto wa Mungu. Yeye ni kiumbe kilichoshindwa. Yesu Kristo, mahali pekee pa kuabudia, Jina pekee la kweli, alilomshindia hapo Kalvari. Nasi tunadai Damu Yake sasa hivi, kwamba Yeye alishinda kila maradhi, kila ugonjwa.

Nami namwagiza Shetani kuwaacha wasikizi hawa. Katika Jina la Yesu Kristo, toka katika watu hawa, na wafanywe huru

Kila mtu ambaye anakubali kuponywa kwake juu ya msingi wa Neno lililoandikwa, toa ushuhuda wako kwa kusimama kwa miguu yako na kusema, “Ninakubali sasa kuponywa kwangu katika Jina la Yesu Kristo.” Simama kwa miguu yako.

Mungu asifiwe! Basi. Angalia huku, viwete na kadhalika wakiinuka. Mungu asifiwe. Naam. Aminini tu. Yeye yupo hapa.

Ndugu. Joseph Branham

Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia 65-0220

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 16:1-3
Kutoka 12:3-6
Malaki Sura ya 3 & 4
Luka 17:30
Warumi 8:1
Ufunuo 4:7