24-0602 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

UJUMBE: 65-0218 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Uzao Wa Kifalme Wa Ibrahimu,

Ninatuma salamu ulimwenguni kote, kwa wale waliokusanyika pamoja, wakisikiliza hewani kwa njia ya simu, wakizilisha nafsi zao kwa ile Mana mpya inayoanguka kutoka Mbinguni. Ninyi mmenunuliwa kwa Damu ya Yesu Kristo Mwenyewe.

Bwana Yesu, naomba ya kwamba Wewe utayapa upako maneno haya usiku huu yakasikiwe na kila sikio linaloongozwa na sauti ya Kiungu. Na ikiwa kuna mmoja hapa anayesikiza nchini kote.

Mungu anayapaka mafuta masikio ya kila mmoja wetu, tunaposikiza kutoka kote ulimwenguni na kuisikia sauti ya Kiungu ya Sauti ya Mungu ikisema nasi, Bwana Asema Hivi.

Sisi ndio Kanisa halisi la Mungu lililozaliwa mara ya pili ambalo huamini KILA Neno la Mungu dhidi ya cho chote kile, bila kujali ni kitu gani, kwa maana ni Sauti ya Mungu ya kweli isiyoghoshiwa inayonena.

Mungu anajidhihirisha Mwenyewe ndani yetu, Kanisa Bibi-arusi Wake. Sisi sio wabebaji wa ile Mbegu, SISI NI UZAO WA KIFALME. Uzima Wake wote uliokuwamo ndani Yake umejizaa tena ndani YETU, Kanisa Bibi-arusi halisi na wa kweli akizaa Neno zima la Mungu katika utimilifu Wake na katika nguvu Zake.

Hapawezi kuwepo nyakati zingine za kanisa baada ya huu. Tuko katika wakati wa mwisho, ndugu na dada. Tuko hapa; tumefika. Bwana ashukuriwe!

Tuko mwisho. Tumewasili. Bibi-arusi YEYE ametambua Sisi ni nani. Ni wakati wa Bibi-arusi Mbegu. Makapi yamekufa. Yale makapi tayari yamekwisha kukauka. Sisi ndio Neno la Mungu lililozaliwa kibikira lililodhihirishwa, Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele.

Hatutaguswa. Hakutakuwa na kuguswa-guswa na watu ndani YETU. Sisi NDIKO Kuzaliwa kibikira kwa Bibi-arusi. Tumeamriwa na Mungu kudumu waaminifu kwa Neno bikira. Mbegu haina budi kukaa katika Uwepo wa Mwana, Roho Mtakatifu, Sauti ya Mwana wa Adamu, ili Iweze kuivishwa. Na kwetu sisi, KUNA NJIA MOJA TU PEKEE: KUBONYEZA PLAY NA KUISIKIA SAUTI YA MWANA WA ADAMU MWENYEWE.

Na kama nisemavyo kuna Kanisa lililoteuliwa mahali fulani ulimwenguni lililotoka na kujiweka mbali na mambo hayo. Na madhihirisho ya Mungu yamelivutia macho. Tumo katika siku za mwisho.

Sisi ni Tai wa Mungu. Hakuna kupatana ndani yetu. Tunaweza tu kula Mana mpya. Sisi ni kama ndama zizini. Tunakula tu Chakula kilichohifadhiwa ambacho kimeandaliwa kwa ajili yetu.

Tunawaona Tai wa Mungu kote ulimwenguni wakitaka hiyo Mana mpya. Wataendelea kuitafuta mpaka waipate. Wataruka juu zaidi na zaidi. Iwapo haimo katika bonde hili, ataruka juu zaidi. Wanataka Neno la Mungu jipya kutoka kwenye Sauti ya Mungu. Kikomo chao cha Milele kimetulia juu Yake. Palipo na Mzoga, Tai wanakusanyika.

Roho wake amekuja juu yetu kufanya mambo yale aliyofanya. Ni kujizaa tena kwa ile Punje. Sisi ndio ule Uzao wa Kifalme wa Imani ya Ibrahimu ambao tunachukua lolote lilio kinyume cha Neno la Mungu na kukiita kana kwamba Sivyo kilivyo. Hatuwezi kutilia shaka ama kuliweka mahala pasipo pake Neno hata moja la Mungu, kwa maana tunaamini ni BWANA ASEMA HIVI. Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele.

Mungu mpendwa, hebu na tusiyape kisogo kwa ajili ya upuzi wa ulimwengu, bali hebu na tumpokee Yeye usiku wa leo kwa mioyo yetu yote._Nawe Bwana, kaumbe ndani yangu roho zuri, Roho ya Uzima, nipate kuamini maneno Yako yote na kumkubali Yesu, aliye Neno, yeye yule jana, leo, na hata milele, na nikaamini leo ile sehemu ambayo imekusudiwa kwa wakati huu. Tujalie, Bwana. Naomba katika Jina la Yesu.
   
Ningependa kuwaalika kuja kuisikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ya wakati wa mwisho anapotupa Chakula cha Tai; ahadi ya Mungu. Inahitaji imani isiyoghoshiwa katika Neno hili la Mungu ili kuwa Bibi-arusi Wake.

Ndugu. Joseph Branham
    

Muda:

saa 6:00 SITA MCHANA Saa za Jeffersonville (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)

Ujumbe:

Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi 65-0218

Maandiko:

Mathayo 24:24
Luka Mt 17:30
Yohana Mt 5:24 / 14:12
Warumi 8:1
Wagalatia 4:27-31
Waebrania 13:8
1 Yohana 5:7
Ufunuo 10
Malaki 4

Bali unapofikia kusema, “Mimi na Baba Yangu ni Mmoja,” na mambo haya mengine, ndipo kapi linajiondoa kwake. Bali Kanisa Bibi-Arusi halisi atazaa Neno nzima la Mungu katika utimilifu Wake na nguvu Zake, kwa maana ni yeye yule jana, leo, na hata milele.

65-0218 -  Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi
Rev. William Marrion Branham 

Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele.
Roho yuaja juu ya Bibi-Arusi kufanya mambo yale aliyofanya. Mnaona, ni kujizaa tena kwa ile punje.

65-0218 – Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi
Rev. William Marrion Branham