24-0526 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

UJUMBE: 65-0217 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Abiria wa Ninawi,

Baba, palipo Mzoga Wako, ndipo Tai Wako wanakusanyika pamoja. Unatulisha kwa Mana Yako ya Kiungu. Zipe nafsi zetu kile tunachohitaji. Tunakuonea kiu, Ewe Baba. Tuko Mikononi Mwako.

Tumekaa katika uwepo Wako, tukiivishwa, kwa kuisikia Sauti Yako. Bibi-arusi hawana budi waamue niani mwao na kukabiliana nalo. Aidha ni Kweli au ni uongo. Je! kuisikia Sauti Yako iliyothibitishwa ndilo jambo lililo muhimu zaidi ambalo Bibi-arusi Wako analopaswa kufanya au la? Kama ni kweli, hebu na tulifanye. Usingojee zaidi, tafuta uone sasa ukweli ni upi na lililo sahihi, na udumu Nalo. Tunajua ni Kweli, tunajua Ndio Njia Yako iliyoandaliwa ya siku hii.

Ni lazima nipige kelele, “Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Mungu amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?” Tunaliona katika Neno. Uliliahidi Hilo. Ni nani wawezao kunyamaza na kutulia?

Hatutaki wazo linalopendwa na watu wengi. Tunataka Ukweli. Nasi hatuninino, tuna(taka) hatutaki ku—hatutaki kukabili cho chote ila ambacho Mungu amesema ni Kweli.

Wakati umefika ambapo yakubidi uamue ni merikebu gani unayopanda. Je! unajilisha Neno lililonenwa moja kwa moja kutoka kwa Mwana wa Adamu, ama kitu kingine? Je! kuna mtu fulani anayekuambia kwamba yakubidi uzisikie sauti zingine ili uweze kuwa Bibi-arusi Wake? Kwamba kuzicheza kanda katika nyumba zenu au makanisani mwenu silo jambo lililo muhimu zaidi ambalo Bibi-arusi analotakiwa kufanya?

Unasikiliza sauti ya nani? Hiyo sauti inakuambia nini? Ni sauti gani unayoweka kikomo chako cha Milele, na cha familia yako kwake?

Si mimi, haikuwa yule malaika wa saba, loo, la; ilikuwa ni kudhihirishwa kwa Mwana wa Adamu. Haikuwa ni yule malaika, ujumbe wake; ilikuwa ni siri aliyoifunua Mungu. Si mwanadamu; ni Mungu. Yule malaika hakuwa Mwana wa Adamu; yeye alikuwa ni mjumbe kutoka kwa Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu ni Kristo; Yeye Ndiye mnayejilisha. Hamjilishi mwanadamu; mwanadamu, maneno yake yatashindwa. Bali mnakula Mwili-Neno lisiloshindwa la Mwana wa Adamu.

Msisikilize sauti yo yote ambayo haiweki Sauti hiyo, Mwili-Neno lisiloshindwa la Mwana wa Adamu, NAFASI YA KWANZA mbele zenu. Wao wanaweza kuhubiri, kufundisha, au kufanya yote ambayo Mungu amewaitia kufanya, lakini wao SIO ile sauti iliyo muhimu zaidi MNAYOPASWA KUISIKIA.

Kama wangeamini hivyo, basi wangeicheza Sauti hiyo mnapokuwa mmekusanyika pamoja na kuwaambia, “Sauti hii, iliyo kwenye kanda, ndio Sauti iliyo muhimu zaidi ya kusikiliza. Hiyo, na HIYO pekee ndio, BWANA ASEMA HIVI.”

Ni Sauti ipi unayoipenda? Kwa nini Yeye aliifanya Sauti Yake irekodiwe na kuhifadhiwa? Mungu alichagua Sauti ya nani kulinena Neno Lake kwa ajili ya siku yetu?

Kwa nabii Wake aliyemtoa, yule aliyemtuma kushuka kwenda kule na kuutangaza ujumbe huo. Naam, ilionekana kama kwamba Yeye angaliweza kumtuma nabii mwingine, bali Yeye alimchagua Yona; na hata Eliya asingalifaa; Yeremia asingalifaa; Musa asingalifaa. Yona ndiye ilikuwa aende Ninawi. Hakukuwa na lingine. Yeye alimwagiza na kumwambia aondoke aende. Na Yeye anaposema, “Nenda kule, Yona, nenda Ninawi,” hakuna mwingine anayeweza kwenda kufanya jambo hilo ila Yona.

Mungu alituchagua tangu zamani kwa ajili ya maisha haya. Sauti hii inatunenea Maneno ya Uzima wa Milele. Kwetu sisi, hii ndiyo Njia iliyoandaliwa na Mungu. Hii ndio Merikebu yetu. Kama umo kwenye merikebu inayoenda Tarshishi, Toka kabla haijachelewa sana.

Kama umekuwa ukishangaa, au una maswali yoyote moyoni mwako upitie njia gani ama ufanye nini, njoo uungane nasi. Ingia kwenye Merikebu pamoja nasi. Tunaenda Ninawi, kupiga kelele. Tunaiacha hiyo merikebu ya Tarshishi ishuke iende kama wakitaka. Tuna wajibu mbele za Mungu, huo ni Ujumbe ambao tunawajibika kwake.

Sisemi ikiwa unaenda kwenye kanisa lisilocheza kanda kuwa ni merikebu inayoelekea Tarshishi, lakini kama MTU YEYOTE haweki Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda kuwa ndio sauti iliyo muhimu sana ikupasayo kuisikia, afadhali uangalie kuona ni nani anayeiongoza merikebu yako na ni wapi merikebu yako inakoelekea.

Ninakualika uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) wakati Nahodha wa Merikebu yetu anapozungumza na kutuletea Ujumbe:   Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana 65-0217.

Hebu na tuanze ufufuo huu vizuri. Hiyo ni kweli. Mnangojea nini? Tunaamini ya kwamba Kuja kwa Bwana kumekaribia, Naye atakuwa na Bibi-Arusi, na Yuko tayari. Nasi hatutaki merikebu zo zote zinazoelekea Tarshishi ye yote. Tunaenda Ninawi. Tunaenda Utukufuni. Amina. Hiyo ni kweli. Tunaelekea mahali ambapo Mungu atatubariki, na hivyo ndivyo tunavyotaka kufanya.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Yona 1:1-3
Malaki 4
Yohana Mt 14:12
Luka 17:30