PASAKA 2026 – Ibada Maalum ya Ushirika na Kutawadhana MIGUU

Wapendwa Raia Wenza Wa Ufalme,

Pasaka hii inaahidi kuwa Pasaka iliyo kuu kuliko ambayo Bibi-arusi amewahi kuwa nayo. Tumekuwa tukiketi katika Uwepo wa Mwana, tukiivishwa, tukijitambua sisi ni nani. Ule utimilifu wa Yesu Kristo unadhihirishwa ndani ya kila mmoja wetu huku Neno Lake, Sauti Yake, ikipiga kelele, Tai kwa tai, ikituita kutoka kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi.

Kila mwaka wakati huu Bibi-arusi anaisubiri kwa hamu kubwa wikendi ijayo ya Pasaka. Wakati ambapo Yeye atatuunganisha kutoka kote ulimwenguni kwa siku nne mfululizo, tukimwabudu Yeye, tukimshukuru Yeye, tukimsifu Yeye; kwa maana Yeye amefufuka na anaishi ndani ya kila mmoja wetu. Bwana Arusi na Bibi-arusi wanakuwa MMOJA.

Yeye anatupa sisi wakati huu maalum wa kufungia nje vitu vyote vya kilimwengu vinavyotuzunguka na kuutumia tu muda pamoja Naye. Hakuna vizubaishi vya kilimwengu huu, huku tunapouumba ulimwengu wetu wenyewe pamoja Naye. Tufunge milango yetu, tuvizime vifaa vyetu vyote vya kielektroniki na chochote kinachotukengeusha kutoka Kwake.

Haja iliyo kuu ambayo kila mmoja wetu aliyonayo ni kuwa karibu Naye. Tunataka kuishi maisha yaliyowekwa wakfu zaidi kwa ajili Yake; kuwa daima katika mapenzi Yake makamilifu. Kuwa tayari kwa ajili ya Kuja Kwake. Hakuna chochote katika ulimwengu huu, au katika maisha yetu, kilicho muhimu zaidi kuliko hili.

Yeye ametupa sisi fursa hii maalum ya kuutumia tu muda pamoja Naye, kuzungumza na kumtafakari Yeye. Kuingia katika uwepo Wake na kuifungua mioyo yetu Kwake. ITAKUWA IBADILISHAYO MAISHA KWA BIBI-ARUSI WAKE!

Yeye anajua yaweza kuwa vigumu kwa baadhi yenu wenye watoto, familia, na majukumu mengine tuliyo nayo, lakini tukiitumia kila sekunde huru tuliyonayo kuzungumza Naye, kumkaribia Yeye, kumfungulia Yeye mioyo yetu, kutakuwako na badiliko kubwa katika kutembea kwetu pamoja Naye, hata hatutakuwa vile tulivyokuwa.

Kama vile Yeye alivyofanya katika ile siku ya Musa alipowaleta watoto Wake majumbani mwao, damu ilikuwa imepakwa nao walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kule Kutoka kwao; itakuwa vivyo hivyo na wikendi hii maalum ya Pasaka ambayo Yeye ameiandaa kwa kila mmoja wetu.

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu aliila Karamu ya Mwisho pamoja na wanafunzi Wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Tunayo fursa iliyoje ya kufanya ushirika na Bwana majumbani mwetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba Yeye atusamehe dhambi zetu, na atupe yote tunayohitaji katika safari yetu.

Baba wa Mbinguni, tunashukuru kwa ajili ya jambo hili, wakati mwingine wa kukusanyika pamoja, upande huu wa Umilele. Na tunatarajia asubuhi ya leo kuhuishwa upya kwa nguvu kuja kutoka Kwako, zipate kututia moyo kwa ajili ya safari iliyoko mbele. Tumekusanyika kama wana wa Kiebrania walivyofanya asubuhi na mapema, kuokota mana iliyokuwa imetolewa kwa ajili yao usiku kucha, kuwapa nguvu kwa ajili ya siku ijayo. Tunakusanyika kwa ajili ya Mana ya kiroho, asubuhi ya leo, ipate kutupa nguvu kwa ajili ya safari.

Hebu sote tuanze saa 12:00 KUMI NA MBILI JIONI. masaa ya eneo unaloishi ili kusikiliza Ushirika 62-0204, na kisha nabii atatupeleka kwenye ibada yetu maalum ya Ushirika na Kutawadhana Miguu baada ya kanda kukamilika, ambayo itachezwa kwenye app ya Lifeline (kwa Kiingereza), au unaweza kuipakua ibada hiyo kwa Kiingereza au lugha zingine kwa kubofya anuani iliyo hapa chini.

IJUMAA

Hebu na twende katika maombi pamoja na familia zetu saa 3:00 TATU ASUBUHI,(Ni saa 10:00 KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na kisha tena saa 06:00 SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki), tukimwalika Bwana awe pamoja nasi na kuzijaza nyumba zetu kwa Roho Mtakatifu tunapojiweka wakfu Kwake.

Hebu akili zetu na zirudi huko nyuma hadi kwenye siku ile pale Kalvari, yapata miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani. Na tukumbuke ile gharama kuu Yeye aliyoilipa kwa ajili yetu. Yeye alikuwa Mwana wa Mungu asiye na dhambi, lakini ilibidi ateseke kuliko mtu mwingine angeweza kuteseka, kwa sababu dhambi zetu sisi ziliwekwa juu Yake.

Ilibidi amtume Yeye kuzimu akiwa amehukumiwa (Unaona?), kwa sababu Yeye alizichukua dhambi zetu. Naye Kristo alikufa, si mwenye haki; Kristo alikufa mwenye dhambi. Unaona? Kristo mwenyewe hakutenda dhambi, bali alizichukua dhambi zetu juu Yake.

Kisha saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA,(Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) na tuungane pamoja majumbani mwetu kusikia: 57-0419 Ukamilifu.

Kisha na tuungane tena katika maombi mara tu baada ya ibada, katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu na tuungane tena sote katika maombi saa 3:00 ASUBUHI (Ni saa KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na saa 06:00 SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na tuiandae mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu Yeye atakayotutendea sisi miongoni mwetu.

Ninaweza kumsikia akisema, “Shetani, njoo hapa!” Yeye ni Bosi sasa. Ananyosha mkono, anaunyakua ule ufunguo wa mauti na kuzimu kutoka ubavuni mwake, akauning’iniza ubavuni Mwake Mwenyewe. “Ninataka kukupa notisi. Umekuwa laghai muda mrefu kutosha. Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai niliyezaliwa na bikira. Damu Yangu ingali imelowa msalabani, na deni kamili limelipwa! Huna haki tena. Umenyang’anywa zote. Nipe funguo hizo!”

Kisha saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA,(Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) sote tutakusanyika pamoja kulisikiliza NENO: 57-0420 Kuzikwa.

Hii itakuwa SIKU ILIYO MAALUM vipi kwa Bibi-arusi Wake kote ulimwenguni.

Kisha hebu na tuungane tena pamoja katika maombi mara tu baada ya ibada.

JUMAPILI

Hebu kwanza na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, robini, alipomwamsha saa 11:00 Alfajiri. Natumshukuru tu Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, maskini rafiki yangu mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa 3:00 TATU ASUBUHI, (Ni saa KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) tuungane tena katika mnyororo wetu wa maombi, tukiombeana na kujiandaa kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 3:30 TATU NA NUSU ASUBUHI, (Ni saa KUMI NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) tutakusanyika pamoja kuusikiliza Ujumbe wetu wa Pasaka: 65-0418M Ni Kuchomoza kwa Jua.

Saa 06:00 SITA MCHANA. (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tutaziinua sauti zetu Kwake tukimshukuru kwa ajili ya Nguvu za Kuhuisha.

Saa 9:00 TISA ALASIRI.(Ni saa 4:00 NNE USIKU ya Afrika Mashariki), Hebu na tuungane tena katika maombi, tukimshukuru Yeye kwa ajili ya WIKENDI YA KUPENDEZA ALIYOTUPA SISI PAMOJA NAYE NA BIBI-ARUSI WAKE KOTE ULIMWENGUNI.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama vile mwaka jana, ningependa kuwaalika muungane nasi katika masaa ya Jeffersonville, kwa masaa yote ya maombi katika ratiba hii. Hata hivyo, ninatambua kwamba kuzicheza Kanda Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri kwa masaa ya Jeffersonville itakuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikieni huru kuzicheza Jumbe hizo kwa masaa yafaayo kwenu. Hata hivyo, ningependa sote tuungane pamoja Jumapili saa 3:30 TATU NA NUSU ASUBUHI masaa ya Jeffersonville (Ni saa 10:30 KUMI NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki), kuusikia Ujumbe wetu wa Jumapili pamoja.

Pia ningependa kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya vipindi vya Creations, Journaling na mapishi, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunafikiri mtayapenda kwani yote yanalenga NENO tutakalolisikia wikendi hii.

Kwa ajili ya ratiba ya wikendi, taarifa kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika Kwa ajili ya vipindi vya Creations, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizo hapa chini.

Hebu tuzifunge simu zetu kwa ajili ya wikendi ya Pasaka isipokuwa kupiga picha, kusikiliza Nukuu ya Siku, na kucheza kanda kutoka kwenye app ya The Table, app ya Lifeline, au kwenye anuani ya kupakulia.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kuja pamoja na Bibi-arusi ulimwenguni kote katika wikendi iliyojaa KUABUDU, KUSIFU NA UPONYAJI. Ninaamini kweli hii ni wikendi ambayo itayabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham