UJUMBE: 65-1212 Ushirika
Mpendwa Bibi-arusi Wa Neno Lililothibitishwa Peke Yake,
Jinsi gani tunavyomshukuru Roho Mtakatifu kwa Ufunuo wa kweli wa Neno Lake lililothibitishwa la wakati huu. Wengi wanakiri kwamba wanaamini Ndugu Branham ndiye nabii wa Mungu anayetimiza Maandiko yaliyoahidiwa kumhusu yeye, lakini Ufunuo wa kweli wa Neno na mpango wa Mungu umefichwa kwao.
Kwa kila Ujumbe wa Barua ya mahaba ambao Bibi-arusi anaousikia, Mungu anatuthibitishia kwamba tuko katika Mapenzi Yake makamilifu kwa kuisikiliza Njia Yake iliyoandaliwa kwa ajili ya wakati huu, Sauti ya Mungu iliyo kwenye Kanda.
Nasi hatuna budi kumfuata, ndiyo njia pekee ya kupata Uzima wa Milele. Kwa hivyo uongozi wa Mungu ni: fuata Neno lililothibitishwa la wakati huu na Roho Mtakatifu.
NJIA PEKEE ya uzima wa Milele ni: Roho Mtakatifu kukuongoza kulifuata Neno lililothibitishwa. Ni nani aliye na Neno lililothibitishwa la wakati huu? Mungu alimchagua nani kulifasiri Neno Lake? Ni nani ambaye Mungu alimsema ndiye Sauti Yake ya wakati huu? Ni nani ambaye Mungu Mwenyewe alimsema alikuwa ndiye kiongozi aliyethibitishwa kumwongoza Bibi-arusi Wake leo? Je, Ni wahudumu?
Kama tu nilivyosema, maskini yule tai mdogo aliposikia Sauti ya Bwana Arusi, alienda Kwake, Neno la Mungu lililotiwa mafuta, lililothibitishwa kwa ajili ya siku hizi za mwisho.
Nuhu alikuwa ndiye Neno lililothibitishwa la wakati wake.
Musa alikuwa ndiye Neno lililothibitishwa la wakati wake.
Yohana alikuwa ni Neno lililothibitishwa
Wanaweza kulipindisha au kuliwekea fasiri yoyote Kwake watakayo, Bali:
WILLIAM MARRION BRANHAM NDIYE NENO LA MUNGU LILILOTHIBITISHWA LA WAKATI HUU!!
Kwa hivyo uongozi wa Mungu ni: fuata Neno lililothibitishwa la wakati huu na Roho Mtakatifu.
Na Je, kuicheza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa katika kanisa lako silo jambo lililo muhimu kuliko ambalo Bibi-arusi analopaswa kufanya? Je, ni muhimu zaidi kuisikiliza sauti tofauti?
Je! ni kundi la watu na huduma yao ndiyo itakayomuunganisha na kumwongoza Bibi-arusi? Je, Bibi-arusi ataunganishwa na yale wasemayo wahudumu? Wote wanasema mambo tofauti, kwa hivyo tumfuate nani?
Je! Ni fasiri yao ya Ujumbe huu ndiyo tutakayohukumiwa kwayo? Je! wao wanayo Nguzo ya Moto inayoithibitisha huduma yao? Je! fasiri yao ya Neno ndiyo Yakini yako?
Nabii alisema Bibi-arusi ANGEUNGANA. Jiulize mwenyewe, ni kitu gani kitakachoufanya unabii huu utimie ili Bwana aje na kumnyakua Bibi-arusi Wake?
Ndiposa, watu wa Mungu waanzapo kukusanyika pamoja, kuna umoja, kuna nguvu. Ona? Na wakati wo wote watu wa Mungu watakapoungana pamoja kabisa, naamini ufufuo utatokea wakati huo. Kutakuwako na wakati wa kunyakuliwa Roho Mtakatifu aanzapo kuwakusanya. Wao—itakuwa katika uchache, bila shaka, lakini kutakuwepo na kukutanika kukuu.
Je! Kutakuwepo na kukutanika kukuu kwenye huduma ya mtu fulani, mbali na nabii wa Mungu aliyethibitishwa? Je! litakuwa ni KUNDI la wahudumu kwa sababu baadhi ya wahudumu wa huduma tano wanasema Hupaswi KAMWE kuicheza Sauti ya Mungu kanisani mwako, ni makosa. Je! wao watamwongoza Bibi-arusi basi?
TAFADHALI NISAIDIE! NI MHUDUMU GANI NINAYEPASWA KUMFUATA, KWANI NATAKA KUUNGANA KATIKA KULE KUKUTANIKA KUKUU.
Wengine husema ati wahudumu wa huduma tano wa Ngurumo Saba ndiyo watakaomkamilisha Bibi-arusi. Baadhi ya wahudumu wa huduma tano wanasema siku za huduma ya Mtu Mmoja zimekwisha. Baadhi ya wahudumu wa huduma tano wanasema yatubidi turudi kwenye Pentekoste. Wengine husema Ujumbe SIO Yakini. Wengine wanasema ukizicheza kanda wewe ni mwamini mungu-mtu. Wote wanasema kitu fulani tofauti, na WOTE wana fasiri tofauti, mawazo tofauti, lakini kila mmoja anasema WAO wanaongozwa na Roho Mtakatifu.
NI MHUDUMU GANI WA HUDUMA TANO NIMFUATE? Maadamu ninamfuata mchungaji “WANGU” wa huduma tano, nitakuwa Bibi-arusi? Kuna “Vikundi” vingi tofauti vya wahudumu wa huduma tano. Hawa wahudumu 20 wanakusanyika na kufanya mikutano yao, lakini wao hawakubaliani kabisa na wahudumu hao wengine 20 walio na mikutano tofauti…niende kwenye mikutano gani ili nikamilishwe na kuungana…baadhi ya hiyo…yote?
Nao watu wanaamini ati MCHAFUKO HUU UTAMUUNGANISHA NA KUMKAMILISHA BIBI-ARUSI? Wote wanasema wao ni WATUMISHI WA KWELI WA HUDUMA TANO ALIYEITWA NA MUNGU. Lakini wao hawawaongozi ninyi kwenye UONGOZI WA KWELI WA ROHO MTAKATIFU, WAO WANAWAONGOZA NINYI KWAO WENYEWE NA KWENYE HUDUMA YAO.
Kwangu mimi, hata huhitaji ufunuo kujua kwamba hilo haliwezi kamwe KUMUUNGANISHA au KUMUONGOZA Bibi-arusi wote. Ni NENO PEKE YAKE litakalomuunganisha Bibi-arusi, kwa SAUTI YA MUNGU MWENYEWE ILIYO KWENYE KANDA.
Ndugu na dada, afadhali muamke ikiwa mnamfuata mchungaji ambaye anahubiri tu na kunukuu Neno, ambalo ni zuri na NDILO HASA analopaswa kuwa akifanya, lakini yeye hawaambii, na muhimu zaidi, HAFANYI HIVYO, kuicheza SAUTI YA MUNGU ILIYO KWENYE KANDA KANISANI MWENU.
Ndugu Branham alituambia:
Naam, tuna tu maagizo matatu ya Kiungu tuliyoachiwa: mojawapo ni—ni ushirika; kutawadhana miguu; ubatizo wa maji. Hayo ndiyo tu mambo matatu. Huo ndio ukamilifu, wa utatu, mnaona.
Ningependa tuwe na Ibada ya Ushirika na Kutawadhana Miguu Jumapili hii, Bwana akipenda. Kama tulivyofanya wakati uliopita, ningewahimiza muanze saa 11:00 JIONI. kwa masaa ya eneo mnaloishi. Ingawa Ndugu Branham alisema mitume walikuwa na Ushirika kila wakati walipokutana pamoja, alipendelea kuufanya wakati wa jioni, naye akautaja kama Meza ya Bwana.
Ujumbe na Ibada ya Ushirika utakuwa kwenye Redio ya Sauti, na pia kutakuwa na anuani ya faili lakupakuliwa, kwa wale ambao hawawezi kuifanikisha Redio ya Sauti Jumapili jioni.
Ndugu Joseph Branham