25-0713 Mahali Pekee Palipowekwa Na Mungu Pa Kuabudia

UJUMBE: 65-1128M Mahali Pekee Palipowekwa Na Mungu Pa Kuabudia

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Familia ya Yesu Kristo,

Jambo fulani linatendeka zaidi ya hapo nyuma kwa Bibi-arusi wa Kristo kote ulimwenguni. Mambo ambayo tumeyasikia na kutamani kuyaona sasa yanadhihirika mbele ya macho yetu.

Roho Mtakatifu anamuunganisha Bibi-arusi Wake kama alivyosema angefanya, kwa njia Yake PEKEE aliyoiandaa kwa ajili ya siku hii, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.

Yeye analifunua na kulithibitisha Neno Lake zaidi ya hapo awali. Kama Kisima kinachofoka maji, Ufunuo unabubujika ndani yetu.

Huo muungano wa kiroho wa Kristo na Kanisa Lake sasa, wakati mwili unapofanyika Neno, nalo Neno linafanyika mwili, linadhihirishwa, linathibitishwa. Vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku. Mbona, inalundikana upesi sana huko nje, katika yale majangwa, na mambo yanayotendeka, hata nisingeweza kufuatilia jambo hilo.

Kila siku Ufunuo zaidi na zaidi unafunuliwa na kudhihirishwa kwetu. Kama vile nabii, mambo yanatokea na yanatendeka haraka sana, hatuwezi hata kuyafuatilia…UTUKUFU!!!

Wakati wetu umefika. Maandiko yanatimia. Mwili unafanyika Neno, nalo Neno linafanyika mwili. Vile vile nabii alivyosema yangetukia sasa yanatendeka.

Kwa nini sisi?

Hakuna chachu, hakuna sauti isiyojulikana, hakuna fasiri ya mwanadamu inayohitajika miongoni mwetu. Tunalisikiliza tu Neno Safi Kamilifu kutoka kwenye kinywa cha Mungu kwa anavyozungumza nasi mdomo kwa sikio.

Sasa tunaona Neno lile lile lililoahidiwa, la Luka, la Malaki, ahadi hizi nyingine zote za siku ya leo, zikifanyika mwili, zikikaa kati yetu, ambazo tulisikia kwa masikio yetu; sasa tunamwona Yeye (kwa macho yetu) akifasiri Neno Lake Mwenyewe, hatuhitaji fasiri yo yote ya mwanadamu.

Ewe Bibi-arusi, hilo haliwezi kuwa wazi zaidi ya hapo. Ni Mungu, akisimama mbele ya Bibi-arusi Wake katika mwili wa mwanadamu, ambaye tunaweza kumwona kwa macho yetu wenyewe, akizungumza na kulifasiri Neno Lake Mwenyewe, na kuliweka kwenye kanda. Neno Kamilifu lililonenwa na kurekodiwa na Mungu Mwenyewe, hivyo halihitaji fasiri yoyote ya mwanadamu.

  • • Mungu anazungumza moja kwa moja na Bibi-arusi Wake, kwenye kanda.
  • • Mungu hulifasiri Neno Lake Mwenyewe, kwenye kanda.
  • • Mungu anajifunua Mwenyewe, kwenye kanda.
  • • Mungu akimwambia Bibi-arusi Wake, huhitaji fasiri yoyote ya mwanadamu, Neno Langu lililo kwenye kanda ndiyo yote BIBI-ARUSI WANGU ANALOHITAJI.

Kumbukeni, mtakapoondoka hapa, anzeni kutoka kwenye kapi sasa; mnaingia kwenye punje, bali kaeni katika Uwepo wa Mwana. Msiongeze, yale nimesema; msiondoe, yale nimesema. Kwa sababu, ninazungumza Ukweli kadiri niujuavyo, kama vile Baba alivyonipa. Mnaona?

Mungu ameitengeneza NJIA KAMILIFU PEKEE kwa Bibi-arusi kufanya vile hasa Yeye alivyotuamuru kufanya. Hilo halikuwezekana, hadi leo hii. Hakuna kubahatisha, hakuna kushangaa, hakuna swali ikiwa humo kuna kitu chochote kilichoongezwa, kuondolewa, au kufasiriwa. Bibi-arusi amepewa ule Ufunuo wa kweli: KUZICHEZA KANDA NDIYO NJIA KAMILIFU YA MUNGU.

Ikiwezekana, hebu niliseme hilo tena. Ufunuo wangu ni kwamba Bibi-arusi wa Yesu Kristo, si wengine, BIBI-ARUSI, hahitaji KITU KINGINE ila Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.

Lakini mara huyo Roho Mtakatifu kweli…Neno halisi linapoingia ndani yako (Neno, Yesu), basi, ndugu, Ujumbe si siri kwako basi; unaujua, ndugu, wote umeangaziwa mbele yako.

Ujumbe si siri kwangu. Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. Mbingu na nchi zote zinaitwa Yesu. Yesu ni Neno.

Nalo hilo Jina limo katika Neno kwa kuwa Yeye ni Neno. Amina! Yeye ni nini basi? Neno lililofasiriwa ni dhihirisho la Jina la Mungu.

Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake na Sauti Yake, ambayo alikuwa ameirekodi na kuihifadhi kwa ajili ya siku hii, ili kwamba aweze kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja kama Jamii Moja. Bibi-arusi yeye ataliona na kulitambua Hilo kuwa NJIA PEKEE Yeye anayoweza kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja.

Yeye alilifanya hilo zaidi ya miaka 60 iliyopita ili kutuonyesha sisi jinsi gani ambavyo Yeye angelifanya hilo leo. Sisi ni “moja ya makanisa yake kwenye muunganisho wa simu”

Kama mimi siamini kwenda kanisani, basi kwa nini niwe na makanisa? Tulikuwa nayo kila mahali nchini, yameunganishwa hivi majuzi usiku, kila maili mia mbili mraba kulikuwapo na kanisa langu.

Wahudumu wengi huyaambia makanisa yao kuwa kwenye “muunganisho wa simu” au “kusikiliza hewani”, “kuusikiliza Ujumbe mmoja kwa wakati mmoja”, ati sio kwenda kanisani. YEYE AMETOKA KUSEMA HUKO NI KWENDA! Wao ni kwamba tu aidha hawalijui Neno ama hawawezi kuisoma barua ya mahaba kama vile Bibi-arusi awezavyo.

Kanisa ni nini? Hebu na tuone kile Ndugu Branham alichosema kanisa lilicho.

Makusanyiko mengi, mengi yamepata makao haya kama mlivyokuwa nayo hapa kutoka maskani. Pia imeunganishwa huko Phoenix, ya kwamba kila mahali ibada zilipo, inaingia moja kwa moja kwenye…Na wanakusanyika makanisani na majumbani, na mambo kama hayo, kupitia wimbi zuri sana.

Ndugu Branham anasema waziwazi kwamba watu wakiwa “majumbani” mwao na “mambo kama hayo” walikuwa ni moja ya makanisa yake kwenye muunganisho wa Simu. Kwa hivyo majumba, vituo vya mafuta, majengo, familia zilizokusanyika pamoja kwenye muunganisho wake wa simu hilo liliwafanya kuwa kanisa.

Hebu na tuisome kidogo zaidi BARUA YA MAHABA.

Tunayaombea makanisa yote na makusanyiko ambayo yamekusanyika kuzunguka vile—vile—vile vipaza sauti vidogo nchini kote, kutoka kwenye taifa, kote kote hata kwenye Pwani ya Magharibi, kule juu kwenye milima ya Arizona, chini kwenye mabonde ya Texas, mbali sana hata Pwani ya Mashariki, nchini kote, Bwana, ambako wao wamekutanika. Tuko umbali wa masaa mengi, bali, Bwana, sisi tuko pamoja usiku wa leo kama jamii moja, waamini, tukingojea kuja kwa Masihi.

Kwa hivyo wakiwa kwenye Muunganisho wa Simu, wakimsikiliza Ndugu Branham WOTE KWA WAKATI MMOJA; walikuwa pamoja kama jamii moja, waamini, wakingojea Kuja kwa Masihi.

Lakini ninyi mnasema ukifanya hivyo leo, huko sio kwenda kanisani, ati ni makosa, sio kukusanyika pamoja na zaidi sana tunapoona ile siku ikikaribia, huko sio kwenda kanisani?

Hebu niwaulizeni swali nanyi myajibu makusanyiko yenu. Kama Ndugu Branham angekuwa hapa leo, katika mwili, nanyi mngeweza kusikiliza hewani au kujiunganisha kwa simu ili kumsikiliza yeye kila Jumapili asubuhi, wote kwa wakati mmoja pamoja na Bibi-arusi kote ulimwenguni, enyi wachungaji, Je! mngeweza KUJIUNGANISHA KWA SIMU na kumsikia Ndugu Branham au mngehubiri?

Ndugu Branham anasema waziwazi wajibu wako ni kanisa lako. Kama ungekuwa hapa miaka 60 iliyopita naye Ndugu Branham alikuwa na ibada, lakini kanisa lako halingehudhuria bali lilikuwa na ibada yao wenyewe (jambo ambalo wahudumu wengi walilifanya wakati huo), Je, wewe ungeweza kwenda kwenye “kanisa lako”, au ungeenda kwenye “Maskani ya Branham” kumsikiliza Ndugu Branham?

Nitawapa jibu langu. Mimi ningekuwa nikisimama mlangoni kwenye mvua, theluji au tufani ya theluji ili niingie Maskanini kumsikiliza nabii wa Mungu. Kama NINGEKUWA nikienda kwenye lile kanisa lingine, ningeyabadilisha makanisa usiku huo.

Lakini mwanamke yule, hakujua kama nguvu zilikuwa katika ile fimbo ama la, bali yeye alijua Mungu alikuwa ndani ya Eliya. Hapo ndipo yule Mungu alipokuwa: ndani ya nabii Wake. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na nafsi yako iishivyo, sitakuacha.

Ninawaalika kuungana nasi na kuwa moja ya makanisa ya Ndugu Branham kwenye muunganisho wa simu siku ya Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikituletea Ujumbe: Mahali Pekee Palipowekwa Na Mungu Pa Kuabudia 65-1128M.

Ndugu. Joseph Branham