UJUMBE: 65-1126 Kazi Ni Imani Katika Matendo
- 25-0622 Kazi Ni Imani Katika Matendo
- 21-1126 Kazi Ni Imani Katika Matendo
- 19-1201 Kazi Ni Imani Katika Matendo
- 17-1203 Kazi Ni Imani Katika Matendo – Preliminari
Mpendwa Neno Lililofanyika Mwili,
Haleluya! Udongo wa kuzalia wa mioyo yetu umetayarishwa kwa kulisikia Neno na imefunuliwa kwetu, SISI NDIYE Bibi-arusi mwadilifu wa Kristo; mwana wa Mungu wa thamani, mwadilifu, asiye na dhambi, akisimama pamoja na Bibi-arusi Neno msafi, asiyeghoshiwa, aliyeoshwa kwa Maji ya Damu Yake Mwenyewe.
Sisi tumekuwa Neno lililodhihirishwa lililofanyika mwili, ili Yesu apate kutuchukua sisi, ambao Yeye alitangulia kuwachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, katika kifua cha Baba.
Ulimwengu unaweza kuona kule kudhihirishwa kwa Imani yetu kulingana na jinsi tulivyokuwa tukitenda, na kudhihirisha ya kwamba tunao Ufunuo wa kweli kutoka kwa Mungu wa Neno Lake lililothibitishwa, nasi hatuogopi. Hatujali kile ulimwengu mzima unachosema ama unachoamini…SISI HATUOGOPI. Kubonyeza Play ndiyo njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi wa Yesu Kristo.
Kuna wengi wanaosema wanauamini Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, wanaamini kwamba Mungu alimtuma nabii, wanaamini William Marrion Branham alikuwa malaika-mjumbe wa saba, wanaamini kwamba alinena Bwana Asema Hivi, lakini wao HAWAAMINI kwamba Sauti ndiyo sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia. Wao hawaamini kuwa yeye alinena Maneno ya kutokosea. Hawaamini kuzicheza kanda katika makanisa yao.
Hiyo inamaanisha nini? INAMAANISHA HILO HALIJAFUNULIWA KWAO!
Ni ufunuo. Yeye amekufunulia jambo fulani kwa neema Yake. Hakuna kitu ulichofanya. Hukujitahidi upate imani. Kama ukiwahi kuwa na imani, umepewa hiyo kwa neema ya Mungu. Na Mungu anakufunulia, kwa hiyo imani ni ufunuo. Na Kanisa lote la Mungu limejengwa juu ya ufunuo.
Kwa IMANI imefunuliwa kwetu ya kwamba Ujumbe huu ndiyo Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ambayo imerekodiwa, na kuhifadhiwa, ili kumlisha na kumkamilisha Bibi-arusi wa Yesu Kristo.
Ni IMANI ya kweli, isiyoghoshiwa katika yale Mungu aliyosema kwamba ni Kweli. Nayo imetia nanga ndani ya moyo na nafsi yetu na hakuna kitu kitakachoitikisa. Itakaa papo hapo mpaka nabii Wake atakapotutambulisha kwa Bwana wetu.
Hatuwezi kufanya vinginevyo. Yeye alitutayarisha sisi kulipokea na kuliamini Hilo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Yeye alijua sisi tungeipokea Sauti Yake katika wakati huu. Alitangulia kutujua tangu zamani na akatuchagua tangu asili kuipokea.
Basi, kazi ambazo Roho Mtakatifu anazifanya siku hizi, kwa maono haya yasiyoshindwa, ahadi zisizoshindwa, ishara zote za kimitume zilizoahidiwa katika Biblia, za Malaki 4, na, loo, Ufunuo 10:7, yote hayo yanatimia; na kuthibitishwa kisayansi, kwa njia yoyote ile. Na kama sijawaambia Kweli, mambo haya hayangetendeka. Lakini kama nimewaambia Kweli, yanashuhudia ya kwamba nimewaambia Kweli. Angali ni yeye yule jana, leo, na hata milele, na madhihirisho ya Roho Wake yanamnyakua Bibi-arusi. Hebu imani hiyo (ufunuo) iangukie ndani ya moyo wako, ya kwamba “Hii ndiyo ile saa.”
Hii ndiyo ile saa yenyewe. Huu ndio Ujumbe wenyewe. Hii ndiyo Sauti ya Mungu inayomwita Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Loo, Ewe Kanisa, Bwana na auandae udongo wa kuzalia wa moyo wako upate kuwa na Imani na akufunulie ya kwamba kuisikiliza Sauti hii, kwenye kanda, ndiko kutamkamilisha na kumuunganisha Bibi-arusi wa Yesu Kristo.
Ninawaalika kwa mara nyingine tena mje kuungana nasi Jumapili saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) kuipeleka IMANI yako ifike mahali pa juu, na kuketi pamoja nasi katika ulimwengu wa roho tunapoisikia Sauti ya Mungu ikitutayarisha kwa ajili ya ujio Wake wa hivi karibuni.
Ndugu. Joseph Branham
Tafadhali iweni katika maombi kwa ajili yetu wiki ijayo tunapoianza Kambi yetu ya kwanza ya Still Waters.
Ujumbe: Kazi Ni Imani Katika Matendo 65-1126 (Matendo Ni Imani Iliyodhihirishwa)
Maandiko ya kusoma:
Mwanzo 15:5-6, 22:1-12
Matendo 2:17
Warumi 4:1-8, 8:28-34
Waefeso 1:1-5
Yakobo 2:21-23
Yohana Mtakatifu 1:26, 6:44-46