UJUMBE: 61-0806 Lile Juma La Sabini La Danieli
Wapendwa Wanaokesha na Kungoja,
Kuna msisimko mkubwa miongoni mwa Bibi-arusi zaidi ya hapo kabla. Tuko chini ya matarajio makubwa; mwaka wetu wa yubile unakaribia kutimia. Bibi-arusi amengoja kwa muda mrefu sana siku hii ifike. Mwisho wa kipindi cha Mataifa umefika nao mwanzo wa umilele na Bwana wetu utaanza hivi karibuni.
Tunauelewa wakati tunaoishi kwa kulisikia Neno. Muda umeisha. Wakati wa Kunyakuliwa umekaribia. Tumewasili. Roho Mtakatifu amekuja na kumfunulia Bibi-arusi Wake mambo yote makuu, ya siri, yenye kilindi.
Tuko katika hali ya kudhikika, tukimtafuta Mungu; tukijiweka tayari. Tumetupilia mbali mambo yote ya ulimwengu huu. Masumbuko ya maisha haya hayamaanishi kitu kwetu. Imani yetu imefikia viwango vikuu kuliko hapo awali. Roho Mtakatifu anampa Bibi mteule Wake Imani ya kunyakuliwa, ili aweze kuja na kumchukua.
“Haya majuma sitini na tisa yametimia kikamilifu; kule kuondoka kwa Wayahudi kulitimia kikamilifu; wakati wa kanisa ulitimia kikamilifu. Tuko katika wakati wa mwisho, wakati wa kanisa la Laodikia, mwisho wake. Wale wajumbe nyota wote wamehubiri ujumbe wao. Umetangazwa. Tuko tu karibu na ukingoni.”_
Ni wakati wa kitendawili jinsi gani tunaoishi. Ni nyakati ngumu kuliko kwani adui anamshambulia kila mmoja kuliko hapo awali. Anatutupia yote aliyo nayo. Yuko katika hali ya kudhikika, kwa maana anajua wakati wake umefika mwisho.
Lakini wakati huo huo, hatukuwahi kuwa wenye furaha maishani mwetu.
- ° Hatukuwahi kuwa karibu zaidi na Bwana.
- ° Roho Mtakatifu anajaza kila kiungo cha mwili wetu.
- ° Upendo wetu kwa Neno Lake haujawahi kuwa mkuu zaidi.
- ° Ufunuo wetu wa Neno Lake hujaza nafsi zetu.
- ° Tunamshinda kila adui kwa Neno.
NA, hatukuwahi kuwa na hakika ya kuwa sisi ni nani:
- ° ALIYECHAGULIWA TANGU ZAMANI
- ° MTEULE
- ° ALIYECHAGULIWA
- ° UZAO WA KIFALME
- ° KIPENZI,
- WA MILELE, ALIYEVIKWA MAVAZI MEUPE, BI. JÉZU, MSIKILIZA KANDA, ALIYEANGAZWA, BIKIRA SAFI, ALIYEJAZWA NA ROHO, ASIYESHINDWA, MWANA MWENYE MAMLAKA, ASIYEGHOSHIWA, BIBI-ARUSI NENO BIKIRA.
Kitu gani kinachofuata? Lile Jiwe linakuja. Tunakesha, tukingoja na kuomba kila dakika ya kila siku. Hakuna kitu kingine kilicho muhimu ila sisi kujitayarisha kwa ajili ya kuja Kwake.
Sio, “Tunatumai hivyo”, TUNAJUA. Hakuna mashaka tena. Katika dakika moja, katika kufumba na kufumbua jicho itakwisha, nasi tutakuwa ng’ambo ya pili pamoja na wapendwa wetu wote na YEYE kwenye Karamu yetu ya Arusi.
NA HUO NI MWANZO TU…NA HAKUNA MWISHO!!
Njoo ujitayarishe kwa ajili ya Karamu hiyo ya Arusi pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) wakati Mungu anaponena kupitia malaika Wake mwenye nguvu, yule aliyemtuma kumwongoza Bibi-arusi Wake, wakati aelezapo, na kufunua, siri zote za Mungu.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 61-0806 – Lile Juma La Sabini La Danieli