25-0209 Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli

UJUMBE: 61-0730E Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi anayefurahi,

Tumeelekeza nyuso zetu Mbinguni katika maombi na kusihi ili kupata siku na saa hasa tunayoishi.

Zaidi ya hapo awali, tumeketi pamoja katika ulimwengu wa roho, kutoka ulimwenguni kote, tukimsikiliza Mungu akinena na kulifunua Neno Lake kwetu kupitia malaika-mjumbe Wake mwenye nguvu. Malaika-mjumbe wa duniani ambaye Baba alimtuma kwa Bibi-arusi Wake katika siku hii ya mwisho kulifunua Neno Lake.

Gabrieli ndiye malaika kwa watu waliochaguliwa na Mungu, Wayahudi. Lakini kwa Bibi-arusi Wake Mmataifa, Melkizedeki Mwenyewe alikuja na kunena kupitia mwili wa mwanadamu katika malaika wa duniani aitwaye William Marrion Branham, ili apate kunena na kulifunua Neno Lake LOTE kwa Bibi-arusi Wake kipenzi wa moyoni.

Alilifanya lirekodiwe, lihifadhiwe, na litunzwe, ili Bibi-arusi apate Chakula Chake cha kiroho, Mana iliyofichwa, kwenye ncha ya vidole vyao kila dakika ya kila siku mpaka mwisho wa wakati.

Utu wetu wa ndani umejawa na upako kama nini wakati tunaiposikia Sauti ya Mungu ikilifunua Neno Lake kwetu. Jinsi gani Yeye anavyolifunua Neno Lake ili tuweze kuona waziwazi na kuelewa maana Yake. Linafunua saa yenyewe hasa tunayoishi, linatuambia sisi ni nani na ni nini kinachoenda kutukia hivi karibuni; Unyakuo wetu unaokuja hivi karibuni.

Yeye hata anamfunulia Bibi-arusi Wake kile kitakachokuwa kikitendeka hapa duniani wakati tuwapo pamoja Naye kwenye Karamu ya Arusi. Jinsi ambavyo Yeye atakavyoyafungua macho yaliyopofushwa ya wateule Wake; wale aliowapofusha kwa ajili ya Bibi-arusi Wake Mmataifa.

Enyi marafiki, najua jinsi tulivyochoshwa na ulimwengu huu na tukitamani kuja kwake kutuchukua, lakini pia hebu na tufurahi na kushukuru kwa yale yanayotukia hivi sasa mbele ya yaya haya macho yetu.

Hebu na tuinue mikono yetu, mioyo yetu, sauti zetu, na kufurahi. Sio tu kwamba tunatazamia yale ambayo anayoenda kututendea hivi karibuni, lakini hebu na tufurahi juu ya yale anayotufunulia na kututendea hivi SASA.

Yeye anatuambia sisi ni Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa tangu asili tukiungana pamoja Naye na Neno Lake. Anatuhakikishia tena na tena, tuko katika Mapenzi Yake makamilifu kwa sisi kukaa na Sauti Yake, Neno Lake, malaika Wake. Ametupa IMANI ya kujua na kujitambua sisi ni nani:
NENO LAKE LIISHILO KATIKA MWILI.

Hatuna cha kuogopa; Hakuna cha kuhofia, hakuna cha kujihuzunisha nacho; Ninalijuaje hilo? MUNGU ALISEMA HIVYO! KWA HIYO HEBU NA TUSHANGILIE, TUFURAHI, TUWE NA SHUKRANI; NENO LILILO HAI LINAISHI NA KUKAA NDANI YETU. SISI NDIO UZAO WAKE MKUU WA KIFALME.

Ninaamini kweli Bwana lazima atakuwa pia amechangamshwa sana kujua kwamba wakati umefika nasi tumejiweka wenyewe tayari kwa kudumu wa kweli na waaminifu kwa Neno Lake.

Kama yule mvulana mdogo aliyejitazama kwenye kioo kwa mara yake ya kwanza, tunatazama katika Neno Lake, tukiona sisi NI NANI. Bwana…NI MIMI. Mimi ndiye Bibi-arusi Neno lililo hai Wako. Mimi ndiye uliyemchagua WEWE. Mimi niko ndani Yako, Wewe U ndani yangu, sisi ni Mmoja.

Tunawezaje kutosherehekea na kuwa watu wenye furaha kuliko wote waliowahi kuishi kwenye uso wa dunia? Watakatifu na manabii wote waliotutangulia walitaka kuishi katika siku hii na kuziona ahadi hizi zikishika kasi. Lakini kwa NEEMA ya Mungu,Yeye alituweka SISI hapa.

Tunasubiri kwa hamu:

Brrrr! Loo, jamani! Whiu! Kwa maneno mengine, wakati adui atakapokuwa ameondolewa, mwisho wa dhambi umekuja, kuletwa kwa haki ya milele kumekuja, Shetani amefungiwa kuzimuni, na maarifa ya Bwana yataijaza dunia kama maji yaifunikavyo bahari. Amina! Mungu atukuzwe! Linakuja, ndugu, linakuja!

Ni upako wa namna gani utakaotendeka Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) tunapokusanyika pamoja kutoka ulimwenguni kote kumsikia malaika wa Mungu, Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi, akituletea Ujumbe: Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli 61-0730E.

Ndugu. Joseph Branham