UJUMBE: 61-0108 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
- 25-0112 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
- 21-0103 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 16-0417 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
Wapendwa Wa Milele,
Ni wakati wa sisi kuvua kofia yetu ya vita na mvae mawazo yenu ya kiroho, maana Mungu anajitayarisha kumpa Bibi-arusi Wake Ufunuo zaidi wa Neno Lake.
Yeye atakuwa akitufunulia siri zote za wakati uliopita. Atatuambia yale yatakayotukia wakati ujao. Yale ambayo wengine wote katika Biblia waliyoyaona au kusikia, Yeye atafunua kila jambo dogo la Neno Lake na maana Yake kwetu.
Tutasikia na kuelewa maana ya alama za Biblia: Viumbe Hai, Bahari ya Kioo, Simba, Ndama, Mwanadamu, Tai, Kiti cha Rehema, Walinzi, Wazee, Sauti, Therion, Zoon.
Tutasikia na kuelewa yote kuhusu walinzi wa Agano la Kale. Yuda: Mlinzi wa Mashariki; Efraimu: Mlinzi wa Magharibi; Rubeni: Mlinzi wa Kusini; na Dani: Mlinzi wa Kaskazini.
Hakuna kitu kingaliweza kuja popote karibu na hicho kiti cha rehema pasipo kuyapitia makabila hayo. Simba, akili ya mwanadamu; Maksai: farasi mtenda-kazi; Tai: Wepesi wake.
Jinsi Mbingu, nchi, katikati, na kote kote huku, walikuwa ni walinzi. Na juu yake ilikuwa ile Nguzo ya Moto. Hakuna kitu kilichogusa kiti hicho cha rehema pasipo kuyapitia makabila hayo.
Sasa kuna walinzi wa Agano Jipya: Mathayo, Marko, Luka na Yohana, wakienda mbele moja kwa moja. Lango la mashariki limelindwa na simba, lango la kaskazini limelindwa na tai arukaye, Yohana, yule mwinjilisti. Halafu tabibu upande huu, Luka, mwanadamu.
Zile Injili nne zinalinda Baraka za Kipentekoste pamoja na kila Andiko kuunga mkono yale hasa waliyosema. Na sasa Matendo ya mitume yanathibitisha leo hii pamoja na zile Injili nne ya kwamba Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo, na hata milele.
Wakati mpakwa mafuta wa kweli wa Mungu anaponena, ni Sauti ya Mungu! Tunataka tu kupaza sauti, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu kwa Bwana!”
Hakuna njia ya kumwacha Huyo. Kwa kweli, Hatuwezi kumwacha, kwa kuwa Yeye hatatuacha. Tumetiwa muhuri hata Siku ya ukombozi wetu. Hakuna cha usoni, hakuna cha wakati uliopo, hatari, njaa, kiu, mauti, wala CHOCHOTE KILE, kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo.
Kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu majina yetu yaliwekwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo ili kuiona Nuru HII, kuipokea Sauti Hii, kuuamini Ujumbe Huu, kumpokea Roho Mtakatifu wa wakati wetu na kutembea ndani Yake. Wakati Mwana-Kondoo alipochinjwa, MAJINA YETU yaliwekwa kwenye Kitabu wakati ule ule Jina la Mwana-Kondoo lilipowekwa mle. UTUKUFU!!
Hivyo, hakuna kinachoweza kututenganisha na Ujumbe huu. Hakuna kinachoweza kututenganisha na Sauti hiyo. Hakuna kinachoweza kuuondoa Ufunuo wa Neno Hili kutoka kwetu. Ni wetu. Mungu alituita na akatuchagua na kutuchagua tangu awali. Kila kitu ni chetu, ni yetu.
Kuna njia moja tu ya kuyapata haya yote. Ni lazima uoshwe kwa maji ya Neno. Huna budi kulisikia Neno kabla hujaingia Mle. Na kuna njia moja tu unayoweza kumkaribia Mungu, hiyo ni kwa Imani. Na Imani huja kwa kusikia, kusikia Neno la Mungu, ambalo linaakisiwa kutoka Patakatifu pa Patakatifu ndani ya mjumbe wa wakati.
Kwa hiyo, hapa, malaika wa wakati wa kanisa anaakisi kuingia kwenye maji hayo kwamba Jamaa huyu ni nani hapa, akiakisi rehema Zake, Maneno Yake, hukumu Yake, Jina Lake. Yote yanaakisiwa humu ndani ambako unatenganishwa kwa kuliamini. Unalipata?
Usiache kuzisikiliza kanda, wewe dumu nalo tu. Lichunguze kwa Neno na uone kama ni kweli. Ni Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii.
Njoo uungane nasi Majira haya ya baridi wakati tunapoungana pamoja kutoka kote ulimwenguni na kuisikia Sauti ya Mungu ikilifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake kuliko hapo awali. Hakuna upako mkuu kuliko kubonyeza play na kusikiliza Sauti Yake.
Kutoka katika kilindi cha moyo wangu, Naweza kusema: Nina furaha sana naweza kusema Mimi ni Mmoja Wao pamoja na kila mmoja wenu.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 61-0108 – “Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu ya III”
Muda: saa 6:00 SITA MCHANA Saa za Jeffersonville ( ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki )