UJUMBE: 65-1127E Nimesikia, Bali Sasa Ninaona
- 25-0706 Nimesikia Bali Sasa Ninaona
- 21-1127e Nimesikia, Bali Sasa Ninaona
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 19-1222 Nimesikia Bali Sasa Ninaona
- 17-1210 Nimesikia Bali Sasa Ninaona – Preliminari
- 15-1231 Nimesikia Bali Sasa Ninaona
Mpendwa Bibi-arusi aliyeunganishwa kwa simu,
Leo, Maneno haya Mungu aliyoyanena kupitia Malaika-Mjumbe Wake wa Saba yangali yanatimia kupitia SISI, BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
Kama mimi siamini kwenda kanisani, basi kwa nini niwe na makanisa? Tulikuwa nayo kila mahali nchini, yameunganishwa kwa simu hivi majuzi usiku, kila maili mia mbili mraba kulikuwapo na kanisa langu.
Walikuwa katika makanisa, majumbani, majengo madogo, na hata kituo cha mafuta; wakiwa wametawanyika kote Marekani, wakisikiliza, wote kwa wakati mmoja Neno lilikuwa likitoka.
Na leo hii, sisi tungali ni MOJA YA MAKANISA YAKE. Yeye ANGALI NI MCHUNGAJI WETU. Neno Lake LINGALI HALIHITAJI FASIRI YOYOTE, nasi TUNGALI tumekusanyika ulimwenguni kote, TUMEUNGANISHWA KWA SIMU, tukiisikiliza SAUTI ya Mungu ikimkamilisha Bibi-arusi wa Yesu Kristo.
Leo, Neno hili lingali linatimia.
Kwa nini wao walifanya hivyo wakati huo? Kwa nini wachungaji waliyafunga makanisa yao ili kuusikia Ujumbe moja kwa moja? Wao wangeweza kusubiri tu wazipate kanda, kisha wakahubiri Ujumbe wao wenyewe kwa watu wao baadaye; nami nina hakika wengi wasio na Ufunuo walifanya hivyo.
Au labda wengine waliyaambia makusanyiko yao, “Sasa sikilizeni, sisi tunaamini Ndugu Branham ni nabii wa Mungu, lakini yeye hakusema tunatakiwa kumsikiliza yeye katika makanisa yetu. Mimi ninahubiri Jumapili hii, na kila Jumapili; ninyi zichukueni tu kanda na mzisikilize huko majumbani mwenu.”
Bibi-arusi wakati ule, ni kama tu Bibi-arusi sasa hivi, walikuwa na Ufunuo, nao walitaka kuisikia Sauti ya Mungu moja kwa moja wao wenyewe. Walitaka kuungana na Bibi-arusi kote nchini waisikie Sauti ya Mungu ilipokuwa ikitoka. Wao walitaka kutambulishwa kama moja ya makanisa yake, majumba, ama po pote walipokuwa, na Ujumbe, Sauti, na sasa, kanda.
Leo, Neno hili lingali linatimia.
Kwa nini wao/sisi Tunaliona na wengine hawalioni? Kwa kujua tangu zamani, sisi tulichaguliwa kuliona Hili. Lakini ninyi ambao hamkuchaguliwa, kamwe hamtaliona. Ngano inaliona nayo imeanza kuondoka.
Haimaanishi kwamba unapaswa kuacha kwenda kwenye kanisa lako. Wala haimaanishi mchungaji wako aache kuhudumu. Inamaanisha tu kwamba wahudumu wengi na wachungaji wengi wamesahau JAMBO KUU, nao hawawaambii watu wao SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI mnayopaswa kuisikia ni SAUTI ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Kwenda kanisani kila siku ya kila wiki hakukufanyi wewe kuwa Bibi-arusi; hayo si matakwa ya Mungu. Mafarisayo na Masadukayo walikuwa na mafundisho hayo. Walijua kila herufi ya kila Neno, bali Neno lililo Hai lilikuwa limesimama PAPO HAPO katika mwili wa mwanadamu, lakini wao walifanya nini? Jambo lile lile wafanyalo wengi leo.
Wao watasema, “hayo yalikuwa ni madhehebu aliyokuwa akizungumzia. Ambao hawangemruhusu Ndugu Branham kuhubiri makanisani mwao, bali sisi tunalihubiri Neno na tunasema vile tu yeye alivyosema.”
Hilo ni zuri. Bwana asifiwe. Hivyo ndivyo unavyopaswa kufanya. Lakini kisha useme, leo ni tofauti, ni makosa kuzicheza kanda za Ndugu Branham katika kanisa lako. Wewe hauna tofauti na Mafarisayo na Masadukayo, au madhehebu.
Wewe ni mnafiki.
Kama ilivyokuwa wakati huo, ni Yesu, akisimama mlangoni akibisha, akijaribu kuingia ndani anene moja kwa moja na Kanisa Lake, nao hawataifungua milango yao, nao hawatazicheza kanda katika makanisa yao. “Yeye haji katika kanisa letu ahubiri”.
Adui atageuza hilo na kulizungusha katika pande nyingi sana kwani ANACHUKIA kufichuliwa, lakini hata hivyo, linadhihirishwa mbele ya macho yetu na wengi wanajiondokea.
“Hapo mwanzo kulikuwako” [kusanyiko linasema, “Neno!”—Mh.] “Naye Neno alikuwako kwa” [Kusanyiko linasema “Mungu!”—Mh.] “Naye Neno alikuwa” [Kusanyiko linasema “Mungu!”—Mh.]. “Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu.” Hiyo ni kweli? Sasa tunaona Neno lile lile lililoahidiwa, la Luka, la Malaki, ahadi hizi nyingine zote za siku ya leo, zikifanyika mwili, zikikaa kati yetu, ambazo tulisikia kwa masikio yetu; sasa tunamwona Yeye (kwa macho yetu) akifasiri Neno Lake Mwenyewe, hatuhitaji fasiri yo yote ya mwanadamu. Ee kanisa la Mungu Aliye Hai! mlio hapa na kwenye simu! amkeni upesi, kabla hamjachelewa sana!
Ifungueni mioyo yenu na msikie yale ambayo Mungu ametoka kuwaambieni, makanisa yake yote. Sasa tunamwona YEYE, kwa macho yetu, AKILIFASIRI NENO LAKE MWENYEWE. Hatuhitaji fasiri yoyote ya mwanadamu!! AMKENI KABLA HAMJACHELEWA!!
Tumeyasikia mambo haya maisha yetu yote yale yaliyokuwa yanaenda kutukia katika wakati wa mwisho. Sasa tunaliona kwa macho yetu hilo likitukia.
Yeye Alituambia, KUNA NJIA MOJA PEKE YAKE, AMBAYO NDIYO NJIA YA MUNGU ILIYOANDALIWA ALIYOIFANYA KWA AJILI YA BIBI-ARUSI WAKE. LAZIMA UKAE NA SAUTI YA MUNGU ILIYO KWENYE KANDA.
Ninaualika ulimwengu mzima uje kuungana nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) na kuisikia Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii. Kisha wewe pia unaweza kusema, “Nimesikia habari Zako, bali sasa Ninakuona”.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 65-1127E Nimesikia Bali Sasa Ninaona
Maandiko
Mwanzo 17
Kutoka 14:13-16
Ayubu sura ya 14 na 42:1-5
Amosi 3:7
Marko 11:22-26 na 14:3-9
Luka 17:28-30