UJUMBE: 60-0515M Mfalme Aliyekataliwa
- 25-0427 Mfalme Aliyekataliwa
- 21-0613 Mfalme Aliyekataliwa
- 18-0527 Mfalme Aliyekataliwa
- 16-0217 Mfalme Aliyekataliwa – Preliminari
Rafiki Zangu Wapendwa,
Rafiki zangu wapendwa, wapendwa wangu, wapenzi wangu wa Injili, watoto wangu niliomzalia Mungu.
Ni wikendi ya ajabu vipi tuliokuwa nayo pamoja na Bwana wetu. Haikuwa kama kitu kingine chochote, kutumia tu wakati pamoja Naye, kuzungumza Naye, kuisikia Sauti Yake, kumwabudu Yeye, kumshukuru, na kumwambia jinsi gani tunavyompenda.
Ni heshima iliyoje kuishi katika siku hii na kuwa sehemu ya Maandiko yanayotimia. Maneno ya kibinadamu yanawezaje kueleza yote yaliyo moyoni mwetu? Kama vile nabii alivyosema, Si mimi, kuna Kitu Fulani ndani kilindini, kikisukuma na kububujika ndani yangu; kisima kinachofoka maji ya Roho Mtakatifu. Ni Bibi-arusi akijifanya Mwenyewe tayari kwa ajili ya Bwana-arusi.
Jinsi gani bibi-arusi huchangamka kabla ya harusi yake. Moyo wake huanza kudunda kwa kasi sana wakati sekunde chache za mwisho zinapopita….anajua kuwa hatimaye wakati umefika. “Nimejiweka tayari. Anakuja kunichukua. Sasa tutakuwa MMOJA.”
Kwa kweli tunaishi katika nyakati za mwisho za kumalizia za wakati. Bibi-arusi hivi karibuni atanyakuliwa na kuitwa kwenye Karamu yetu ya fungate. Yeye anatupeleka kwenye viwango vipya. Hakuna swali tena; hakuna tena kushangaa; SISI NDIO BIBI-ARUSI.
Na bado Yeye hajamaliza. Bado Yeye anataka kumbariki na kumtia moyo Bibi-arusi Wake kipenzi aliyechaguliwa. Jinsi gani Yeye anavyopenda kumtia moyo na kumwambia jinsi gani Yeye anavyompenda. Jinsi anavyojivunia Yeye.
Yeye bado anao Ufunuo mwingine wa kipekee sana wa kumpa Bibi-arusi. Wakati kuna sauti nyingi sana ulimwenguni zinazokataa kucheza kanda, Yeye anataka tena kumhakikishia Bibi-arusi kwamba wako katika Mapenzi Yake makamilifu na Njia Yake iliyoandaliwa.
Mpango Wake daima umekataliwa. Bibi-arusi Wake daima ameteswa. Watu daima wanataka njia yao wenyewe, mawazo yao. Wanataka kiongozi tofauti awaongoze. Lakini Mungu alimtuma kiongozi MMOJA kumwongoza Bibi-arusi Wake, Yeye Mwenyewe, Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu wa siku hii, kama ilivyo katika SIKU ZINGINE ZOTE, NI NABII WA MUNGU.
Siku zote wao wametaka watu wawaongoze. Katika siku za Samweli, Mungu alisema walikuwa wakimkataa Yeye kwa kutotaka Samweli awaongoze. Ilionekana kuwa jambo la ajabu kwa vile Samweli yeye pia alikuwa mtu, lakini tofauti ilikuwa Samweli alikuwa ndiye mtu ambaye Mungu alimchagua kuwaongoza. Haikuwa Samweli, Ilikuwa ni Mungu akimtumia Samweli. Yeye alikuwa ndiye SAUTI na MTU ambaye Mungu alimchagua KUWAONGOZA, lakini wao walitaka sauti zingine.
Sauli alijua watu walimcha Samweli, hivyo ilimbidi atangaze, “Sauli NA Samweli”. Ilibidi awaogopeshe watu ili wamfuate yeye. Kweli, alikuwa ameitwa. Kweli, alikuwa ametiwa mafuta na Samweli kuwa mfalme wao, lakini Mungu ANGALI alikuwa anayo Njia iliyoandaliwa, na nabii aliyemchagua Yeye kuwaongoza, hata kumwongoza na Sauli. Mungu alinena na nabii Wake na kumwambia Sauli la kufanya. Wakati Sauli alipoamua kuwa amepakwa mafuta yeye pia, na hakutaka kumsikia nabii tu, Mungu aliuondoa ufalme wake.
Kwa hiyo basi walipofanya jambo hilo, wakati kule kushindwa kukuu kulipokuja, ndipo Sauli alichinja maksai wawili wakubwa na kuwapeleka kwa watu wote. Na laiti mngaliona hapa. Wakati Sauli alipopeleka vipande vya yule maksai kwa Israeli wote na kusema, “Na iwe kwamba mtu ye yote ambaye hatamfuata Samweli na Sauli, na awe (huyu maksai) kama huyu.” Mnaona jinsi alivyojaribu kujiwakilisha kwa hila pamoja na mtu wa Mungu? Jinsi lilivyokuwa si la Kikristo. Uchaji wa watu ulikuwa kwa ajili ya Samweli. Bali Sauli akawafanya wote wamfuate kwa maana watu walimcha Samweli. “Na wamfuate Samweli na Sauli.”
Siku moja Sauli alifadhaika sana. Hakuweza kupata jibu kutoka kwa Mungu. Hakuweza kupata faraja. Alitaka majibu. Alijua ni wapi alipaswa kwenda ili kupata jibu alilotaka; palikuwa na mahali pa moja tu, NABII WA MUNGU, SAMWELI. Alikuwa amekwisha vuka ng’ambo, lakini bado yeye alikuwa angali ni SAUTI YA MUNGU, HATA KATIKA PARADISO.
Baba alitaka Bibi-arusi Wake ajue Yeye Alimchagua nani kumwongoza Bibi-arusi Wake katika siku hii ya mwisho, kwa hivyo Yeye Akamchukua malaika Wake mwenye nguvu kule ng’ambo ya pazia la wakati ili kwa mara nyingine tena atuambie, atufariji, na kututia moyo kwamba tuko katika Mapenzi Yake makamilifu na yaliyoandaliwa.
Yasikilize kwa makini sana YOTE anayosema nabii.
Sasa, nisingewataka ninyi mrudie jambo hili. Hili ni mbele ya kanisa langu, ama kondoo wangu ninaowachunga.
Kabla yeye hajatuambia lo lote, kwanza anatutaka tujue hili ni kwa ajili YETU PEKE YAKE, KANISA LAKE, KONDOO WAKE, WALE ANAOWACHUNGA. Kwa hivyo, kama huwezi kusema, “Ndugu Branham ni mchungaji WANGU,” nimesema jambo hilo hapo awali, lakini hakuna tu haja ya kulisoma zaidi, hili si kwa ajili yako, pamoja na kwamba yeye hakututaka hata tulirudie kwa ye yote yule ila kwa wale wanaoamini na kusema, “Ndugu Branham ni mchungaji wangu”.
Hilo papo hapo jibu letu kwa swali tunalopata shutuma nyingi sana kwa sisi kusema: “Ndugu Bramham ndiye mchungaji wetu.” (Hao ni wale watu wa kanda.) Wako sahihi, yeye yuko hivyo, nasi tuko hivyo.
Tafadhali msinikasirikie, mimi sisemi mambo haya ili kumkasirisha mtu ye yote, hilo lingekuwa kosa, bali ni yale Yeye anayomwambia Bibi-arusi. Mimi siweki fasiri yangu kwake, Yeye analisema wazi…Neno la Mungu halihitaji fasiri yo yote.
Ama ilikuwa kwamba nilikuwa katika mwili ama nje yake, ama ilikuwa kuhamishwa, Haikuwa kama ono lo lote nililopata kuona.
Sasa yeye anatuambia hili halikuwa kama ono lo lote alilopata kuona. Alikwenda mahali ambapo hajawahi kufika. Lilikuwa KUBWA kuliko ono lolote alilowahi kuona. Hakuwa akiota, aliuona mwili wake kitandani; ALIKUWEPO KULE.
Bibi-arusi wa Yesu Kristo, hebu hilo na lizame vizuri sana. Walikuwa ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo kule ng’ambo ya pili, wa wakati uliopo, waliyokuja wakimkimbilia, wakipiga kelele na kumshika, wakimkumbatia na kusema, “Loo, ndugu yetu wathamani!”
Yeye alikuwa kule; aliweza kulihisi; aliweza kuwasikia. Walikuwa wakizungumza naye. Alisimama, na kutazama, alikuwa kijana. Akaangalia nyuma kwenye mwili wake mzee uliokuwa umelala pale mikono yake ikiwa nyuma ya kichwa chake.
Sasa tumethibitisha YEYE ALIKUWEPO KULE, na Ilikuwa ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo aliyekuwa akimwona. Sasa hebu na tusikie kile ile sauti kutoka juu ilichokuwa ikimwambia.
Ndipo sauti hiyo iliyokuwa ikinena nami kutoka juu yangu, ikasema, “Unajua imeandikwa katika Biblia ya kwamba manabii walikusanywa pamoja na watu wao.”
Mungu hakuwa tu akimwonyesha na kumtia moyo nabii Wake, bali kulikuwa na mengi zaidi Kwenye jambo Hilo. Yeye angerudi na kutuambia sio tu wapi tunakoelekea na jinsi gani kungekuwa, bali kutuambia sisi tuko katika Mapenzi Yake makamilifu kwa Kubonyeza Play na hivyo ndivyo unavyofika mahali alipo Bibi-arusi.
Ndugu Branham alisema yeye alitaka kumwona Yesu vibaya sana. Lakini wakamwambia:
“Naam, Yuko juu kidogo tu, moja kwa moja upande ule.” Kasema, “Siku moja Yeye atakuja kwako.”
Wakaendelea kumwambia yeye ALIKUWA NANI.
“Wewe ulitumwa kuwa kiongozi na Mungu atakuja, na atakapokuja, Yeye atakuhukumu kulingana na yale uliyowafundisha, kwanza; kama wataingia ama hawataingia. Tutaingia kulingana na mafundisho yako.”
Ni nani aliyetumwa kama kiongozi? Tunaenda kuhukumiwa kulingana na yale nani aliyotufundisha? Tutaingia Mbinguni kulingana na mafundisho ya nani?
Mtu mmoja anaweza kusema, ninawafundisha watu wangu yale tu Ndugu Branham aliyosema…amina, unapaswa nami naamini baadhi wanafanya hivyo, lakini usilifanye “Ndugu Branham na Mimi”
Hebu tuendelee kusoma kwani Yeye anataka KUHAKIKISHA kwamba tunaelewa kwa uwazi zaidi.
Ndipo hao watu wakapiga kelele wakasema, “Tunajua jambo hilo, nasi tunajua tunarudi pamoja nawe siku moja duniani.” Kasema, “Yesu atakuja, nawe utahukumiwa kulingana na Neno ulilotuhubiria sisi.
Tutahukumiwa kwa Neno YEYE alilotuhubiria. Hivyo, hukumu inakuja kutokana na kile Sauti ya Mungu ilichosema kwenye kanda. Mtu yeyote anawezaje kusema ati hiyo Sauti iliyo kwenye kanda sio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI mnayopaswa kuisikia?
“Halafu, kama ukikubalika wakati huo, ambapo utakubalika”
Je! Mko tayari. Hili litapigilia msumari kuhusu Mapenzi makamilifu ya Bwana ni yapi kwa Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Bibi-arusi anamwambia nabii kile YEYE ATAKACHOFANYA. Si mtu mwingine. Sio kundi. Si mchungaji mwingine, nabii wa Mungu, WILLIAM MARRION BRANHAM.
“basi wewe utatukabidhi Kwake kama tunu yako ya huduma yako.”
Je! Ni nani atakayetukabidhi kwa Bwana Yesu?
Je! Siku za kumsikiliza tu nabii zimekwisha?
Je! Ndugu Branham hakuwahi kamwe kusema tucheze kanda?
Bibi-arusi anapiga kelele na kusema kama unataka kuwa Bibi-arusi ni bora Ubonyeze Play.
Bado haujashawishika? Vema, kuna hata na zaidi.
Kasema, “Utatuongoza Kwake na sote pamoja tutarudi duniani tukaishi milele.”
Ni nani wa kutuongoza Kwake? Ni nani anayemwongoza Bibi-arusi? Bibi-arusi anamwambia yeye kwamba YEYE ATAWAONGOZA BIBI-ARUSI KWAKE, kisha tutarudi duniani tukaishi milele.
Ikiwa kuna Ufunuo WOWOTE ndani yako hata kidogo. Ikiwa unadai unauamini Ujumbe Huu, ninaomba ya kwamba Mungu akufunulie ya kwamba ni LAZIMA uiweke Sauti Yake, kanda, kuwa ya KWANZA.
Enyi Wachungaji, mrudisheni nabii kwenye mimbara zenu. Kanda ndio Sauti iliyo muhimu sana mnayopaswa kuisikia kwani mtaenda kuhukumiwa kwa SAUTI HIYO.
Kulingana na Neno, tuko katika Mapenzi Yake makamilifu na yaliyoandaliwa kwa ajili ya siku yetu kwa kusikiliza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Ikiwa Mungu ameyafungua macho yako kwenye Ufunuo wa kweli wa Neno Lake, ninakualika uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tusikiapo 60-0515M Mfalme Aliyekataliwa.
Ndugu. Joseph Branham