UJUMBE: 61-0730M Maagizo Ya Gabrieli Kwa Danieli
Wapendwa Walengwa,
Ni Majira ya baridi ya ajabu vipi tumekuwa nayo tulipojifunza Nyakati Saba za Kanisa, na kisha Mungu akitufunulia hata na zaidi katika Kitabu cha Ufunuo wa Yesu Kristo. Jinsi zile sura tatu za kwanza za Ufunuo zilivyokuwa Nyakati za Kanisa, halafu jinsi ambavyo Yohana alivyotwaliwa juu katika mlango wa 4 na wa 5 kutuonyesha mambo ambayo yangekuja.
Katika sura ya 6, Yeye alifunua jinsi Yohana alivyoshushwa duniani tena ili kuyaona mambo yakitukia ambayo yatakayoanzia sura ya 6 hadi sura ya 19 ya Ufunuo.
Jinsi gani Bibi-arusi atakavyobarikiwa Jumapili tunapoisikia Sauti ya Mungu ikinena kupitia malaika Wake wa saba mwenye nguvu na kutuambia kile kinachoenda kufunuliwa.
Ninayo furaha sana kutangaza kwamba sasa tutaanza lile somo kuu la Yale Majuma Sabini Ya Danieli. Nabii alisema ya kwamba itaunganisha ile sehemu nyingine ya Ujumbe kabla hatujaingia kwenye ile Mihuri Saba; Baragumu Saba; Ole Tatu; yule mwanamke katika jua; kutupwa nje kwa yule pepo mwekundu; wale mia na arobaini na nne elfu waliotiwa muhuri; yote yanatukia katikati ya wakati huu.
Kitabu cha Danieli ndicho kalenda halisi kwa ajili ya kizazi na wakati tunaoishi, na haijalishi linaweza kuonekana gumu kiasi gani, Mungu atalivunja-vunja na kulifanya rahisi kwa ajili yetu.
Na Mungu anajua hayo ndiyo ninayotafuta sasa, nipate kuwafariji watu Wake na kuwaambia mambo yaliyo karibu kutimia, hapa asubuhi ya leo, na pia huko nje katika nchi ambako kanda hizi zitakwenda, kila mahali ulimwenguni, ya kwamba tuko katika wakati wa mwisho.
Sisi ndio wateule wa Mungu ambao tunaotamani na kuomba kwa ajili ya siku hiyo na saa hiyo. Na macho yetu yameelekezwa Mbinguni, nasi tunakutazamia Kuja Kwake.
Hebu sote tuwe kama Danieli na tuzielekeze nyuso zetu Mbinguni, katika maombi na kusihi, kama tujuavyo kwa kusoma Neno na kuisikia Sauti Yake, kuja kwa Bwana kunakaribia upesi; tuko mwisho.
Tusaidie Baba kuweka kando kila mzigo, kila dhambi, kila kutokuamini kudogo ambako kungetuzinga kwa upesi. Hebu sasa na tukaze mwendo kuelekea mede ya wito mkuu, tukijua ya kwamba wakati wetu ni mdogo.
Ujumbe umetoka. Kila kitu kiko tayari sasa; tunangojea na kupumzika. Kanisa limetiwa muhuri. Walio waovu wanazidi kutenda maovu. Makanisa yanazidi kuwa baridi, lakini watakatifu Wako wanakukaribia Wewe zaidi.
Tunayo Sauti inayolia kutoka nyikani, ikiwaita watu waurudie Ujumbe wa asili; wayarudie mambo ya Mungu. Tunafahamu kwa Ufunuo mambo haya yanatukia.
Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) Wakati Mungu anapotufunulia Neno Lake, tunapolianza somo letu kuu la Kitabu cha Danieli.
Ndugu. Joseph Branham
61-0730M – Maagizo ya Gabrieli Kwa Danieli