UJUMBE: 62-1007 Ufunguo Wa Mlango
Wapendwa Wenye Ufunguo wa Imani,
“Mimi ndiye Mlango wa zizi la kondoo. Mimi ndimi Njia, Njia pekee, Kweli, na Uzima, na mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi. Mimi ndimi Mlango wa vitu vyote, na imani ndiyo ufunguo unaofungua mlango ili uweze kuingia.”
Kuna mkono mmoja tu unaoweza kuushikilia ufunguo huu, na huo ni mkono wa IMANI. IMANI ndiyo ufunguo pekee unaofungua ahadi zote za Mungu. IMANI katika kazi yake iliyokwisha kumalizika inaufungua kila mlango kwa kila hazina iliyo ndani ya Ufalme wa Mungu. IMANI ni Ufunguo malaya mkuu wa Mungu ambao unaufungua KILA MLANGO KWA BIBI-ARUSI WAKE nasi tunaushikilia huo Ufunguo katika MKONO wetu wa IMANI.
Ufunguo huo wa imani uko mioyoni mwetu, nasi tunasema, “Ni Neno la Mungu; Ni ahadi za Mungu kwa ajili yetu, nasi tunaushikilia ufunguo.” Na kisha, kwa kila sehemu ya imani tuliyo nayo, bila kutilia shaka hata chembe moja, tunaufungua kila mlango unaosimama kati yetu na baraka ambazo Mungu alizonazo kwa ajili yetu. Inazima jeuri ya moto. Inaufungua uponyaji kwa wagonjwa. Inaufungua wokovu wetu. Tumefika kwenye Mlango na lolote tunalofanya kwa neno au kwa tendo, tunayafanya yote katika Jina Lake, tukijua kwamba tunao ufunguo wa imani; nao ni ufunguo uliotengenezwa kwa Maandiko.
Sisi hatujali kile mtu yeyote anachowazia, kuna jambo moja la hakika: Mungu alituita SISI, alituchagua SISI tangu awali, alitufunulia SISI Neno Lake, alituambia sisi ni nani, nasi tumeyakinia kulifuata Neno Lake, kwa sababu Yeye ametuita sisi tuwe Bibi-arusi Wake.
Baba alizishikilia nyota Zake saba, wajumbe Wake saba, kwa zile nyakati saba mkononi Mwake. Amewashika mkononi Mwake, hivyo wanahusishwa na nguvu Zake. Hicho ndicho mkono unachomaanisha. Unamaanisha nguvu za Mungu! Na mamlaka ya Mungu.
Tumelishika Neno lake katika mikono yetu ya Imani, ikimaanisha uweza na mamlaka ya Mungu vipo MIKONONI MWETU naye ametupa UFUNGUO wa kuufungua kila mlango kwa kila jambo tunalohitaji. Ni Ufunguo Maalum ambao utaufungua KILA MLANGO.
Sasa ninajua kwa nini Mungu alitupa vidole 5 katika kila mkono; sio 4, sio 6, lakini 5, kwa hivyo kila wakati tunapoitazama mikono yetu tutakumbuka, tunayo ILE IMANI ya kuufungua kila mlango.
Ni ishara ya milele kwa jamii ya binadamu kwa hivyo sisi hatutasahau kamwe; daima tutakumbuka na kujipa moyo, kwamba tunaishikilia IMANI hiyo mikononi mwetu. Naye ataiinua imani yetu ya mbegu ya haradali na kutupa ILE IMANI YAKE KUU KATIKA NENO LAKE LISILOWEZA KUSHINDWA KAMWE, LA MILELE LISILOSHINDWA KAMWE!!!
Tunaweza kuinua mikono yetu Mbinguni, kuvinyoosha vidole vyetu 5 kwa kila mkono na kumwambia, “Baba, tunaamini na tunayo IMANI katika kila Neno ulilonena. Ni Ahadi Yako, Neno Lako, nawe Utatupatia Ile IMANI TUNAYOHITAJI ikiwa tu tutaamini….nasi TUNAAMINI.”
Kwa vile tutakuwa na ibada yetu ya Ushirika hadi ifikapo Jumapili jioni, ningependa kuwahimiza mchague Ujumbe wa kusikiliza pamoja na Kanisa lako, familia, au mtu binafsi, Jumapili asubuhi, kwa wakati unaofaa kwako. Hakika hakuna njia bora ya kuitathmini Imani yetu kuliko kusikia Neno; kwa maana IMANI huja kwa kusikia, kulisikia Neno, nalo Neno huja kwa nabii.
Hebu Basi tuungane wote kwa pamoja saa 11:00 kumi na moja JIONI. (kwa masaa ya nchi yako) ili kusikiliza Ujumbe, 62-1007 Ufunguo wa Mlango. Kama ilivyotangazwa, ningependa kuifanya hii kuwa Ibada Maalum ya Ushirika, ambayo itakuwa ikicheza kwenye Redio ya Sauti (Voice Radio) saa 11:00 kumi na moja JIONI. (Masaa ya Jeffersonville). Mnaweza kupakua na kucheza ibada kwa Kiingereza au lugha zingine kwa kubofya hapa: BOFYA HAPA.
Sawa na ibada zingine za Ushirika wa Nyumbani katika wakati uliyopita, mwishoni mwa kanda Ndugu Branham ataombea mkate na divai. Kutakuwa na muziki wa piano kwa dakika kadhaa ili mkamilishe sehemu ya ibada ya Ushirika. Kisha, Ndugu Branham atasoma Maandiko yanayohusu kutawadhana miguu, na Nyimbo za Injili zitafuata usomaji wake kwa dakika kadhaa, ili muweze kukamilisha sehemu ya ibada ya kutawadhana miguu.
Ni fursa iliyoje tuliyo nayo kumwalika Bwana wetu Yesu kula pamoja na kila mmoja wetu katika nyumba zetu, makanisani, au popote ulipo. Niombeeni wakati mnapozungumza Naye, kama ilivyo hakika nitakuwa nikiwaombea.
Mungu awabariki,
Ndugu Joseph Branham