All posts by admin5

Pasaka 2024

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo,

Kalvari inapaswa kukumbukwa kila siku. Tumesikia mengi sana kuihusu. Tumesoma mengi sana juu yake. Wahubiri wameihubiri tangu mwanzo wa wakati. Waimbaji wameimba juu yake katika nyakati zote. Manabii walitabiri miaka elfu nne kabla haijatukia, na manabii wa siku hizi wanatuonyesha kule nyuma ilipotendeka. Ni siku muhimu sana.

Ni moja ya siku zilizo muhimu sana ambazo Mungu amepata kuzishusha duniani.

Ni kukusanyika kwa kipekee kulikoje kutoka ulimwenguni kote ambako Bibi-arusi atakuwanako wikendi hii ya Pasaka. Tutafunga milango yetu na kuuzima ulimwengu wa nje. Tutazima vifaa vyetu vyote ili tusizubaishwe, na tuongee Naye kabisa kabisa kila siku. Tutainua sauti zetu kwake kwa upatano, kwa nia moja na moyo mmoja, kumsifu, kumwabudu, kumwambia jinsi gani tunavyompenda.

Tutasikia Sauti Yake ikizungumza na mioyo yetu tunapoyaweka upya maisha yetu Kwake. Hakuna kitakachokuwa muhimu zaidi kwetu wakati tunapojitayarisha kwa ajili ya Ujio Wake wa hivi karibuni. Bibi-arusi anajiweka mwenyewe tayari zaidi ya hapo awali.

Ningependa sote tuungane kwenye ratiba ifuatayo:

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu alikula Karamu ya Mwisho na wanafunzi wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Ni fursa iliyoje tuliyo nayo ya kuzungumza na Bwana katika nyumba zetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba atusamehe dhambi zetu, na kutupa sisi sote yale tunayohitaji katika safari yetu.

Lijalie, Bwana. Waponye walio wagonjwa. Wafariji walio wachovu. Wape furaha wanaodhulumiwa. Wape amani walio wachovu, Chakula kwa wenye njaa, Maji kwa wenye kiu, furaha kwa wenye huzuni, uwezo kwa kanisa. Bwana, mlete Yesu miongoni mwetu usiku wa leo, tukiwa tunajitayarisha kushiriki ushirika unaowakilisha mwili Wake uliovunjwa-vunjwa. Tunaomba, Bwana, kwamba Yeye atatuzuru kwa njia ya ajabu sana…

Wabariki wengine, Bwana, kila mahali ulimwenguni, ambao wanangojea kwa furaha kuja kwa Bwana, taa zimetengenezwa, na dohani zimesuguliwa kabisa, na Nuru ya Injili ikiangaza katika sehemu zenye giza.

Hebu sote tuanze saa 12:00 KUMI NA MBILI JIONI. Masaa ya maeneo mnayoishi ili kusikia  Ushirika 62-0204, na kisha nabii atatupeleka katika Ibada yetu maalum ya Ushirika na Kutawadhana Miguu, ambayo itakuwa ikicheza kwenye app ya Lifeline (kwa Kiingereza), au unaweza kupakua ibada hii kwa Kiingereza ama lugha nyinginezo kwa kubofya anuani iliyo hapa chini.

Kufuatana na Ujumbe, tutakusanyika pamoja na familia zetu katika nyumba zetu na kula Meza ya Bwana.

IJUMAA

Hebu tuende katika maombi pamoja na familia zetu saa 3:00 TATU ASUBUHI,( ni saa 10:00 Kumi jioni ya Afrika Mashariki ) na kisha tena saa 6:00 SITA MCHANA,( ni saa 1:00 Moja jioni ya Afrika Mashariki ) tukimualika Bwana awe pamoja nasi na azijaze nyumba zetu na Roho Mtakatifu wakati tujiweka wakfu Kwake.

Hebu mawazo yetu na yarudi nyuma hadi siku ile pale Kalvari, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani, na kisha tujitoe vivyo hivyo kufanya daima yale yanayompendeza Baba:

Iwapo siku hii ni muhimu sana, moja ya siku zilizo kuu sana, hebu na tuangalie mambo matatu ambayo siku hiyo ilimaanisha kwetu. Tungechukua mamia. Bali asubuhi ya leo nimechagua tu mambo matatu tofauti yaliyo muhimu sana ambayo tunataka kuyachunguza katika muda mfupi ujao; ambayo Kalvari ilimaanisha kwetu. Nami naomba ya kwamba itamhukumu kila mwenye dhambi aliyeko, ya kwamba itamfanya kila mtakatifu kupiga magoti yake, ya kwamba itamfanya kila mgonjwa ainue imani yake kwa Mungu na aondoke ameponywa, kila mwenye dhambi aokolewe, kila aliyerudi nyuma arudi na ajionee aibu, na kila mtakatifu afurahi na apate tumaini jipya na tumaini jipya.

Kisha saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA,( Ni saa 1:30 Moja na Nusu jioni ya Afrika Mashariki ) tuungane pamoja katika nyumba zetu ili kusikia,  Siku Hiyo Pale Kalvari 60-0925.

Kisha tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA ALASIRI.( ni saa 4:00 Nne Usiku ya Afrika Mashariki ) katika ukumbusho wa kusulubishwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu sote kwa mara nyingine tena tuungane katika maombi saa 3:00 TATU ASUBUHI.( ni saa 10:00 Kumi jioni ya Afrika Mashariki ) na  saa 6:00 SITA MCHANA,( ni saa 1:00 Moja Jioni ya Afrika Mashariki ) na kuitayarisha mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu Atakayotutendea sisi katikati yetu.

Ninaweza kumsikia akisema, “Shetani, njoo hapa!” Yeye ni Bosi sasa. Ananyosha mkono, anaunyakua ule ufunguo wa mauti na kuzimu kutoka ubavuni mwake, akauning’iniza ubavuni Mwake Mwenyewe. “Ninataka kukupa notisi. Umekuwa laghai muda mrefu kutosha. Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai niliyezaliwa na bikira. Damu Yangu ingali imelowa msalabani, na deni kamili limelipwa! Huna haki tena. Umenyang’anywa zote. Nipe funguo hizo!”

Kisha saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, ( ni 1:30 moja na Nusu jioni ya Afrika Mashariki ) sote tutakusanyika ili kusikia NENO:  Kuzikwa 57-0420.

Hii itakuwa SIKU-KUU iliyoje kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

Kisha tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA ALASIRI ( Ni saa 4:00 Nne Usiku ya Afrika Mashariki ).

JUMAPILI

Hebu kwanza tuamke mapema kama Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, robin, alipomwamsha saa 11:00 KUMI NA MOJA ASUBUHI. Hebu tumshukuru tu Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, rafiki yangu mdogo mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa 3:00 TATU ASUBUHI. ( Ni saa 10:00 Kumi jioni ya Afrika Mashariki ) na saa 6:00 SITA MCHANA,( ni saa 1:00 Moja jioni ya Afrika Mashariki ) hebu tuungane kwa mara nyingine tena katika mnyororo wetu wa maombi, kuombeana mmoja kwa mwingine na kujitayarisha wenyewe kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, ( Ni saa 1:30 Moja na Nusu jioni ya Afrika Mashariki ) tutakusanyika pamoja ili kuusikia Ujumbe wetu wa Pasaka:  Muhuri wa Kweli wa Pasaka 61-0402.

Saa 9:00 TISA ALASIRI, ( ni saa 4:00 Nne usiku ya Afrika Mashariki ) tuungane tena katika maombi, tukimshukuru Yeye kwa WIKENDI YA AJABU ALIYOTUPA PAMOJA NAYE NA PAMOJA NA BIBI-ARUSI WAKE ULIMWENGUNI KOTE.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama mwaka jana, ningependa kuwaalika kuungana nasi kwa masaa ya Jeffersonville, kwa masaa yote ya maombi yaliyo kwenye ratiba hii. Ninatambua, hata hivyo, kwamba kuzicheza Kanda ya Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri kwa masaa ya Jeffersonville kungekuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikieni huru kucheza Jumbe hizo kwa masaa yafaayo kwenu. Ningependa, hata hivyo, tuungane pamoja Jumapili saa 6:30 SITA NA NUSU MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:30 MOJA NA NUSU Jioni masaa ya Afrika Mashariki ) ili kuusikia Ujumbe wetu wa Jumapili pamoja.

Ningependa pia kuwaalika ninyi na watoto wenu kuwa sehemu ya vipindi vya Ubunifu, Journaling, na maswali ya majaribio ya YF, ambayo familia yako yote yaweza kufurahia pamoja. Twaamini utayapenda kwa kuwa yote yanahusiana na NENO tutakalosikia wikendi hii.

Kwa ratiba ya wikendi, taarifa ya jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika kwa ajili ya vipindi vya ubunifu, Maswali ya jaribio la Pasaka, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizo hapa chini.

Hebu na tuzifunge simu zetu kwa ajili ya wikendi ya Pasaka isipokuwa kupiga picha, kusikia Nukuu ya Siku, na kucheza kanda kwenye app ya the Table, app ya Lifeline, au anuani za kupakua.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kukusanyika pamoja na Bibi-arusi ulimwenguni kote katika wikendi iliyojaa KUABUDU, SIFA NA UPONYAJI. Ninaamini kweli hakika ni wikendi ambayo itayabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham

24-0324 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapenzi Watu Wathamani na Wapendwa,

Inapendeza sana jinsi gani kujua sisi ndio Bibi-arusi Wake mpendwa na Wathamani. Tumefanyizwa kutoka ulimwenguni kote, tukikusanyika pamoja kulizunguka Neno Lake, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikizilisha nafsi zetu.

Tumelikubali katika ukamilifu wake, na katika nguvu ya kuthibitishwa kwake na ufunuo wake. Tumekuwa sehemu Yake. Ni kitu ambacho kiko ndani yetu. Ni zaidi ya uhai kwetu.

Tumetambua: Malaika-Mjumbe Wake wa Saba.
Tumetambua: Ujumbe wa Nuru ya Jioni.
Tumetambua: Sisi ni Nani.

Mungu amechukua Neno la nabii Wake na kutubangua. Ametukata kwa Malaki 4, kama alivyoahidi angefanya. Tunaamini kila Neno kwa mioyo yetu yote.

Kuna uamsho mkubwa unaoendelea miongoni mwa watu. Wao pia wanatambua umuhimu wa kuisikia Sauti hiyo. Wanataka kurudi na kuzicheza kanda katika makanisa yao.

Wamejulishwa na Roho Mtakatifu, kwamba hii ndiyo Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Wanatambua kuwa hii ndio Sauti wanayohitaji kuisikia. Ndicho Chakula cha Mungu kilichohifadhiwa kwa ajili ya kumkamilisha Bibi-arusi Wake.

Neno liliahidi jambo Hilo. Kanda zinalitangaza. Wao wanaliamini.

Ilifanyaje? Iliwasumbua makuhani, kuona hao watu wakiondoka makanisani na kwenda zao. Akasema, “Kama yeyote wenu akihudhuria mikutano Yake, mtatengwa na ushirika. Tutawafukuza moja kwa moja kutoka katika dhehebu.”

Haliaminiki, lakini hilo limekuwa ni jambo lile lile leo hii. Watakufukuza katika makanisa yao ukisema, “Tafadhali, chezeni kanda.” Je! Hivi tumewahi kamwe kuwazia huenda hiki ndicho kinachowatenganisha watu? Kuicheza Sauti ya Mungu katika makanisa yetu?

Kanisa limesahau manabii wao. Wao “hawawahitaji tena,” ndivyo wanavyodai. Bali Mungu anajua hana budi kuwa nao; Yeye huwakata watu Wake kwa Neno Lake. Lakini kwao Hilo limepitwa na wakati sana katika siku hii.

Tutakaa na nabii wetu. Tunaamini kuwa ndio Sauti inayomwita Bibi-arusi Wake. Kwetu sisi, hakuna kitu chochote kilicho muhimu zaidi ya KUBONYEZA PLAY.

Loo, enyi kondoo za Mungu, sikilizeni Sauti ya Mungu! “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.”

Njoo uisikie na uitambue Sauti hiyo pamoja nasi, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia,  Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M.

Ndugu. Joseph Branham

24-0317 Kuenda Nje Ya Kambi

UJUMBE: 64-0719E Kuenda Nje Ya Kambi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Askari Wakristo,

Wazieni jambo hilo! Ni mwisho wa wakati, Haleluya! Tumewasili. Ile Siku kuu ya Kuja kwa Bwana kumchukua Bibi-arusi Wake imekaribia. Tunakusanyika wenyewe pamoja kutoka ulimwenguni kote, tukikamilishwa kwa kusikiliza Sauti ya Mungu. Tunatazamia na kungojea wapendwa wetu watokee… ni siku yoyote sasa.

Kitu pekee ambacho tumeagizwa kufanya ni “Dumuni na Neno”. Yote tuyaonayo ni Yesu, na Yeye ni Neno lililofanyika mwili. Huo ndio Ufunuo wa siku yetu. Hiyo ndio Kambi ya Mungu kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Ujumbe huu, Sauti hii, kanda hizi, ndicho kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya Unyakuo. Hatuhitaji kitu kingine chochote. Tumeitwa tutoke, tumetengwa na kila kitu kingine isipokuwa ile Sauti. Tumeshawishika kuwa Sauti hiyo ndiyo Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.

Wazieni jambo hilo, Yeye ametupatia nabii mkuu wa nyakati zote. Yule ambaye Nguzo ya Moto Mwenyewe alipiga picha naye ili aweze kuuambia ulimwengu, “Huyu ni malaika wangu mwenye nguvu. Yeye ni Sauti Yangu kwenu. Yale Anenayo duniani Mimi nitarudisha mwangwi mbinguni. Hakuna aliye kama yeye”.

“Nimemkabidhi yeye, na yeye peke yake, siri Zangu zote nilizozificha tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Yeye ndiye niliyemchagua tangu awali kuwaita NINYI mtoke katika ulimwengu huu mje Kwangu. Yeye ndiye niliyemchagua kuwatangulia, kuwaongoza, na kuwaelekeza. Nawatangazieni, msikieni Yeye, kwa maana si yeye anenaye, NI MIMI, YULE MIMI NIKO ALIYE MKUU.

Nimewaweka wakfu watu wakuu na kuwaita kuutangazia ulimwengu na kuuambia , “Leo maandiko ya Malaki 4, Ufunuo 10:7 na Luka 17:30 yametimia mbele ya macho yenu. Yule Malaika wake mwenye nguvu amewasili, kama jinsi Maandiko yalivyotangaza. Mungu yuko hapa miongoni mwetu, akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kama alivyosema angefanya.”

Ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele. Tumeitwa kuwaelekeza ninyi kwake yeye, malaika wa Mungu. Yeye ndiye ambaye Roho Mtakatifu alimchagua kuongoza na kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Msihojiane, msibishane, msigombane na kushindana ni nani atakayekuwa kuhani mkuu; nani anayetakiwa kuwa hili, lile, ama linginelo. DUMUNI NA SAUTI HIYO. Kwa maana kuna SAUTI YA MUNGU moja tu iliyothibitishwa na jina lake ni William Marrion Branham.

Yatupasa kuwa waangalifu sana kudumu na hiyo Sauti, kwa kuwa kuna wengi wanaotaka kuwaongoza kwingineko. Mapokeo yao yanaiweka Sauti hiyo ya kweli mbali na watu. Yeye amekuwa mgeni kwa wengi wao. Sauti yao imepachukua mahali pa Sauti hiyo, hata wakati Mungu, kwa njia ya kanda, anapowazuru, Yeye ni mgeni.

Ule uwepo mkuu wa Agosti u pamoja nasi. Mtu yeyote mwepesi wa kuhisi Roho anaweza kujua Sauti hiyo ni Sauti ya Mungu. Ndio ile Kambi ya Mungu kwa ajili ya siku hii.

Kila mtu anayedai kuwa Bibi-arusi wa Kristo lazima aamue ni Kambi gani aliyomo. Ni lazima wajiulize swali hili rahisi: Hivi ni Sauti gani ambayo Bibi-arusi wote wanaweza kusema “AMINA” kwayo?

Kama kweli wewe ni Bibi-arusi wa Kristo, mwenye Ufunuo wa kweli wa Neno la siku hii, kuna jibu moja tu: Sauti ya Mungu iliyo kwenye Kanda. Bila shaka Shetani anajaribu kuliendesha hilo kwa njia nyingi tofauti, lakini hakuna jibu lingine kwa Bibi-arusi. Ni rahisi jinsi hiyo.

Sote tunajua kwamba Shetani anatumia jibu hilo ili kutugawanya. Lakini Neno linatuambia Bibi-arusi hana budi KUUNGANA… TUMEUNGANA, kwa SAUTI PEKEE INAYOTUUNGANISHA.

Njoo uungane nasi, kwa maana ile saa imechelewa sana.

“Nataka kwenda nje ya kambi. Haidhuru itanigharimu nini, nitautwaa msalaba wangu na kuubeba kila siku. Nitatoka nje ya kambi. Hata watu waseme nini juu yangu, nataka kumfuata nje ya kambi. Niko tayari kwenda.”

Ikiwa unataka kuwa katika ile Kambi ya Mungu ya siku hii, LAZIMA UAMINI Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio Sauti iliyo muhimu sana unayopaswa kuisikia.

Njoo uungane na sehemu ya Bibi-arusi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunapoisikia ile Sauti ambayo Mungu aliyoichagua kumwongoza Bibi-arusi Wake, anapotuletea Ujumbe, Kuenda Nje ya Kambi 64-0719E.

Sio “kambi fulani”; ni “ILE KAMBI”.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ibada :

Waebrania 13:10-14
Mathayo 17:4-8

24-0310 Sikukuu Ya Baragumu

UJUMBE: 64-0719M Sikukuu Ya Baragumu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watoto wa Nuru,

Tunayo shukurani jinsi gani kuwa tunatembea katika Nuru Yake. Kuwa sehemu ya Nuru hiyo, kutambulishwa na Nuru Yake. Kuitwa na kuchaguliwa Na Yeye. Sisi ni Bibi-arusi wa Kristo, tumetambulishwa pamoja Naye. Hao wawili sasa ni Mmoja.

Nisingeweza kuliandika mara nyingi sana. Hatuwezi kulisema vya kutosha. Ujumbe huu unamaanisha KILA KITU kwetu. Kujua kuwa tunao Ufunuo wa kweli wa Neno Lake ni zaidi ya chochote tungeweza kuweka kwa maneno.

Kuishi katika siku hii na kuwa sehemu ya kile kinachotendeka, ndio heshima iliyo kuu ambayo Mungu angeweza kutupa. Jinsi lilivyokuwa jambo kuu kuketi katika mikutano katika Maskani ya Branham, kuona na kumsikia malaika wa Mungu akizileta Jumbe hizi, ni KUU hata na zaidi kule kuishi katika siku hii, na wakati huu, na kuwa ule utimilifu wa Neno hilo.

Mungu, katika Mpango Wake mkuu, ameandaa Njia ambayo tungeweza kukusanyika kutoka ulimwenguni kote, kuisikiliza Sauti ya Mungu sote kwa wakati mmoja, ili kukamilishwa na Neno Lake. Kusubiri kusikia katika sekunde yoyote malaika-mjumbe wetu wa saba aseme;

“Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”

Hakujawahi kuwa na kitu chochote kama Hicho tangu mwanzo wa wakati. Kule Kumalizika kwa Mpango mkuu wa Mungu kunatukia, SASA HIVI, na sisi tu sehemu Yake. Ile Siku kuu ya Bwana imekaribia.

Siri zote zimefunuliwa kwa Bibi-arusi na malaika-mjumbe wa Mungu. Ile Mihuri, zile Nyakati, Ngurumo, Imani ya Kunyakuliwa, Mvuto wa Tatu…KILA KITU kimekwishanenwa na kiko kwenye kanda ili Bibi-arusi aweze kuzisikia tena na tena, nayo INATUKAMILISHA.

Roho Mtakatifu amerudi Kanisani tena; Kristo, Mwenyewe, akifunuliwa katika mwili wakibinadamu, wakati wa jioni kama alivyoahidi.

Sikiliza kwa makini sasa ewe Bibi-arusi, likamate.

Tumeitwa na Neno; Kristo mwenyewe ametuita. Amejiweka mwenyewe dhahiri kwetu; Waebrania 13:8, Luka 17:30, Malaki 4, Waebrania 4:12, Maandiko haya yote aliyoahidi.

Ni Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye amejifunua kwetu kwa Maandiko haya ambayo yaliyochaguliwa tangu zamani kwa ajili ya siku hii, YAISHI TENA.

Na, kuamini Hilo, ndio dhihirisho la Roho Mtakatifu.

Mungu alimtuma nabii Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Neno linatuambia nabii ni Neno lililo hai la Mungu, lililodhihirishwa. Ndio ishara ya mwisho ambayo ulimwengu utakayopata; Yehova akinena katika umbo la mwanadamu.

Mtu katika mwili wa kibinadamu, kama nabii, hata hivyo ilikuwa ni Elohimu akilitambua wazo lililokuwa katika moyo wa Sara, nyuma Yake. Naye Yesu alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika ukamilifu wa dahari, wakati Mwana wa Adamu,” si Mwana wa Mungu, “wakati Mwana wa Adamu atakapokuwa akifunua.”

Bibi-arusi anajua isipokuwa uwe daima katika Neno, hutajua Yeye ni nani. Wao wanajua umuhimu wa kuiweka Sauti hiyo mbele zao kila siku kwa Kubonyeza Play.

Sasa Bibi-arusi hana budi kuondoka jukwaani, na kwenda juu, ili wale manabii wawili wa Mungu katika Ufunuo waweze kutokea jukwaani ili kupiga Baragumu ya Saba. Kuwajulisha Kristo.

Njoo uwe sehemu ya unabii uliotimia Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) wakati nabii wa Mungu anapoleta Ujumbe, Sikukuu ya Baragumu 64-0719M, na kuzungumza na Baba na kusema,

Yawezekana kuwe na baadhi huko nje katika mataifa, ulimwenguni kote, ambao hata kanda hii ingewakuta manyumbani mwao au makanisani mwao. Tungeomba, Bwana, kwamba wakati ibada inaendelea, pale—pale…au kanda inachezwa, au nafasi yo yote tunayoweza kuwamo, au—au hali, yule Mungu mkuu wa Mbinguni na aheshimu huu unyofu wa mioyo yetu asubuhi hii, na kuponya wahitaji.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Walawi 16 yote
Walawi 23:23-27
Isaya 18:1-3
Isaya 27:12-13
Ufunuo 10:1-7
Ufunuo 9:13-14
Ufunuo 17:8

24-0303 Kile Kipeo

UJUMBE: 64-0705 Kile Kipeo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Familia Iliyo Kipeo,

Jinsi gani Jumbe hizi za mwisho zimekuwa Kamilifu kabisa kwa Bibi-arusi wa Kristo. Mungu, akijifunua Mwenyewe mbele zetu, akijifunua Mwenyewe waziwazi. Ulimwengu hauwezi kuliona Hilo, lakini kwetu sisi, Bibi-arusi Wake, Hilo ndilo tuonalo.

Tumelipenya pazia na kumwona Yeye waziwazi kabisa. Mungu, nyuma ya ngozi ya mwanadamu. Neno limefanyika mwili, kama vile hasa Yeye alivyoahidi katika Luka 17 na Malaki 4. Amejificha Mwenyewe katika pazia la mwanadamu, katika nabii Wake na katika Kanisa Lake.

Sisi ndio watu wenye furaha kuliko wote ulimwenguni wakati tunapomsikia Mungu akinena kupitia malaika-mjumbe Wake na kutuambia,

Ninashukuru sana kwa ajili yenu. Nina furaha sana kushirikiana pamoja nanyi. Nina furaha sana kuwa mmoja wenu. Mungu awe nanyi.Atakuwa nanyi. Yeye hatawaacha kamwe. Hatawapungukia. Yeye hatawaacha. Tayari mmekwisha pita katika ile pazia.

Tumekuwa watu wa kipekee kwa kila mtu, hata katika nyadhifa zetu wenyewe, lakini tunajivunia, na kushukuru sana, kwa Ufunuo Ambao Yeye ametupa wa Neno Lake wa siku hii. Kuwa wapumbavu kwa ajili ya Kristo na Neno Lake lililodhihirishwa.

Tumeweka imani yetu pamoja na imani ya nabii Wake, nasi tumeungana pamoja, tukifanya UMOJA mkuu wa Mungu. Yeye Hawezi kitu bila sisi; sisi hatuwezi kufanya lolote bila nabii huyo; wala hatuwezi kufanya lolote bila Mungu. kwa hiyo sote pamoja, TUNAFANYA KITU KIMOJA, Ule Muungano; Mungu, nabii Wake, Bibi-arusi Wake. Tumekuwa Kipeo Chake.

Ilimchukua Yeye miaka elfu nne kutengeneza Kipeo Chake cha kwanza. Sasa, imemchukua Yeye miaka elfu mbili kutengeneza Kipeo Chake kingine, SISI, Bibi-arusi Wake, familia Yake kuu iliyo Kipeo, Adamu wa Pili na Hawa wa Pili. Sasa tuko tayari kwa ajili ya ile bustani, ule Utawala wa Miaka Elfu. Ametufinyanga tena na sasa tuko tayari.

Sisi ndiye Bibi-arusi Wake Neno Kamilifu, sehemu ya ule Uumbaji Wake ASILI. Ubua, kishada, na ganda, sasa vinakusanyika katika ile Mbegu, tayari kwa ufufuo, na tayari kwa mavuno. Alfa imekuwa Omega. Ile Mbegu iliyoingia ndani, imepitia hatua fulani na imekuwa Mbegu tena.

Ile mbegu iliyoanguka katika bustani ya Edeni kisha ikafa kule, ilirudi. kutoka kwa ile mbegu isiyo kamilifu iliyokufia kule, ikarudi ikawa Mbegu kamilifu, Adamu wa Pili.

Sisi sasa tumekuwa Adamu wa Pili, Bibi-arusi wa kweli, ile Mbegu, amerudi na Neno la asili tena. Na lazima tuwe na Neno lote kusudi tupate kuwa ile Mbegu. Hatupaswi kuwa na nusu ya Mbegu; hatuwezi kukua, lazima tuwe Mbegu nzima.

Kuna jambo moja tu lililosalia, mavuno yamefika. Tumeiva kabisa. Tuko tayari kwa kule Kuja. Ni wakati wa mavuno. Ile Mbegu imeirudia hali yake ya asili. Ile Familia ilio Kipeo imekuja tena, Kristo na Bibi-arusi Wake.

Ili kumtia moyo nabii Wake na Bibi-arusi Wake, Bwana alimpa malaika wake ono kuu. Alimpa kuonekana kimbele kwetu SISI, Bibi-arusi Wake. Tulipopita karibu naye, alisema, tulikuwa wanawake wadogo walio wazuri mno. Alisema sote tulikuwa tukimtazama, tulipokuwa tukipita.

Mwishoni, wengine walikuwa wametoka kwenye mstari, nao walikuwa wakijaribu wawezavyo kurudi mstarini. Kisha aliona kitu fulani muhimu sana, walikuwa wakiangalia mahali pengine, Hawakuwa wakimtazama Yeye. Walikuwa wakiliangalia hilo kanisa lililoingia katika machafuko. Jinsi gani ninavyojivunia na ninavyoshukuru kusema, sio SISI, Hao waliokuwa mbele, sisi hatukutoka nje ya hatua ama kuyaondoa macho yetu Kwake Yeye.

Kwa hiyo kile Kipeo na Mwana wa Mungu—Kipeo na Bibi-arusi, Naye ni sehemu Yake, ambayo ni lazima iwe kutimizwa kwa Neno. Neno limekwishatimizwa, nasi tuko tayari kwa kule Kuja kwa Bwana.

Tunayoshukrani jinsi gani kujua, sisi ndio ile Familia iliyo Vipeo Vyake, Bibi-arusi Wake wa kweli. Neno limekwishatimizwa, nasi tuko tayari kwa kule Kuja kwa Bwana.

Ninawaalika mje muungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) ili kusikia Neno pamoja nasi, na kuwa sehemu ya ile Familia iliyo Kipeo cha Mungu, tunapomsikia nabii akituletea Ujumbe: Kile Kipeo 64-0705.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Isaya 53:1-12
Malaki 3:6
Mathayo 24:24
Marko 9:7
Yohana Mtakatifu 12:24 / 14:19

24-0225 Wa Kipekee

UJUMBE: 64-0614E Wa Kipekee

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Marafiki Wapendwa,

Ni saa 6:00 SITA MCHANA huko Jeffersonville, saa 1:00 MOJA JIONI huko Afrika, saa 4:00 NNE ASUBUHI huko Arizona; Bibi-arusi wamekusanyika pamoja kutoka ulimwenguni kote. Tumesubiri wiki nzima kuufikia wakati huu. Tuko chini ya matarajio makubwa, tukimngojea Mungu aseme nasi kupitia midomo ya mwanadamu kwa njia ya malaika-mjumbe Wake wa saba mwenye nguvu. Tunaomba, “Bwana nitayarishe, unitie mafuta, na unipe Ufunuo zaidi wa Neno Lako.”

Tumeridhika, kwa maana tunajua hakika, ya kwamba nabii, na nabii peke yake, ndiye aliye na Maneno ya Uzima ya saa hii. Huenda tusiweze Kulieleza lote, lakini tunajua tunaamini kila Neno na tunalitegemea Hilo.

Tunajua, kama vile Bwana alivyofanya na Musa, Mungu Anajiandaa kumtukuza nabii wake mbele zetu. Wakati huo, Yeye aliitikisa tu milima. Wakati huu, Yeye Anazitikisa mbingu na nchi.

Ule wakati umefika. Mioyo yetu inaenda mbio ndani yetu. Tunausikia wimbo wetu wa Taifa umeanza kucheza. Kwa moyo mmoja, Bibi-arusi kutoka ulimwenguni kote wainuka kwa miguu yao na kuanza kuimba, AMINI TU , yote yawezekana, Amini Tu. Mungu anajiandaa kuzungumza nasi.

Tunasikia: “Habari za asubuhi marafiki.”

Mioyo yetu inafurahi kusikia tu maneno haya 3 rahisi. Nabii ametoka kuniita mimi rafiki yake. Kisha anatuambia,

Ninawakosa ninyi nyote. Si—sijali ninapokwenda, ni—ni…si, si ninyi. Nina marafiki, kila mahali ulimwenguni, bali si—si ninyi nyote. Kuna kitu fulani kuhusu kundi hili dogo ambalo lina ninino tu…Sijui. Mimi huwafikiria…Sina ku—kundi fulani ulimwenguni, nilijualo, linaloshikamana nami kama kundi hili. Mungu na—na ajalie tuwe wasioweza kutengana sana, hata, katika Ufalme ujao, naomba kwamba tuwe huko pamoja; ombi langu.

Ni Ufunuo mkuu jinsi gani ambao Mungu atatufunulia leo? Tunaenda kusikia kitu gani? Labda tumelisikia mara nyingi, nyingi sana hapo kabla, lakini leo itakuwa tofauti, ni kama vile haijawahi siku yoyote hapo kabla.

Ni kitu gani? Chakula cha Mwaminio. Mkate wa Wonyesho kutoka Mbinguni tutakaousheherekea. Mkate wa Wonyesho ulio kwa ajili yetu tu, Bibi-arusi Wake. Ni Utukufu wa Shekina juu ya Mkate huo wa Wonyesho unaotufanya tusiharibike.

Hao walio nje hututazama na kuuliza, “Ninyi watu mnafanya nini? Mnasikiliza tu kanda? Ninyi ni Wa Kipekee kweli kweli.”

Utukufu!! Tunayo furaha sana, na tunamshukuru sana Bwana sisi kuwa Wa Kipekee; wapumbavu kwa ajili Yake na Neno Lake lililothibitishwa. Tunafurahi kuuambia ulimwengu, “NDIYO, NINAAMINI HUDUMA YA KANDA. NINAAMINI KUBONYEZA PLAY. NINAAMINI NDIO SAUTI ILIYO MUHIMU SANA UNAYOPASWA KUISIKIA. NDIYO, NINAAMINI KUZIRUDISHA KANDA MIBARANI.”

Wakati utaji wa mapokeo umeondolewa, unaweza kuona ya kwamba Mungu angali ni Mungu wa Neno Lake. Yeye angali anadumisha Neno Lake. Yeye ni ninii—Yeye ndiye Mungu, Mwandishi wa Neno Lake.

Haijalishi yale mtu yeyote afanyayo, ama asemayo, tunaliamini Hilo, na kisha tunalitendea Hilo kazi. Kama wewe hulifanyi Hilo, basi huliamini. Hauko nyuma ya pazia. Pazia hilo ni la mtu mmoja. Ujumbe huo ni mmoja.

Nami ninatumaini na kuamini ya kwamba—ya kwamba mmekuwa na ufahamu wa kiroho juu ya yale Mungu amekuwa akijaribu kuliambia Kanisa bila ya kulisema moja kwa moja. Unaona? Ni jambo, wakati mwingine, inatubidi kusema mambo kwa njia fulani kwamba iweze kupunguza, iweze kuwafanya wengine kutoka nje, wengine kuondoka, na wengine ku—ku—kutafakari. Lakini hilo linafanywa makusudi. Lazima lifanywe hivyo.

Neno lilifunuliwa kwa nabii wa Mungu. Hakuna cha kundi, Mafarisayo, ama Masadukayo, ama dhehebu fulani ama ukoo. Ni NABII! Mungu alimpata mtu mmoja. Hakupata mawazo mawili au matatu tofauti. Yeye alimchukua mtu mmoja. Ndiye aliye na Neno, na yeye peke yake.

Ndipo huenda ikawa kwamba wengine wangesema, “Unamaanisha Mungu angefanya jambo kama hilo makusudi?” Hakika alifanya. Angali anafanya.

Kama vile walivyosema mamia ya miaka iliyopita, tunasikia jambo lile lile leo hii: “Lakini kuna watu wengine hapa ambao Mungu amewaita.” Hiyo ni kweli. Na maadamu tu wanafuata na kwenda pamoja, ni Amina, bali wakati mtu anapojaribu kupiga hatua na kuchukua nafasi ya Mungu ambayo Mungu aliyompa nabii wetu, ambayo Yeye alichaguliwa tangu zamani na kuwekwa kwa ajili ya kazi hiyo, inatubidi kukaa na Neno lililothibitishwa, ile Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu.

Angalia, kifo, kukaa mbali Nalo sasa. Huna budi kuingia ndani Yake kupitia kwenye pazia hili, la sivyo hutaingia. Jinsi ambavyo Mungu angeweza kuwarehemu, bali kumbukeni vile ilivyokuwa, ya kwamba Mungu anadhihirisha kile kilichokuwa nyuma ya lile pazia. Angalieni kile kilichokuwa nyuma ya pazia, hilo Neno! Lilifunika nini? Neno! Ilikuwa ni kitu gani? Liko kwenye sanduku. Lilikuwa ni lile Neno ambalo lile pazia lililificha. Mnaona? Naye Yesu alikuwa ndiye Neno hilo, Naye Ndiye hilo Neno, nalo pazia la mwili Wake lililificha.

Kwetu sisi, ni udhihirisho! Sio neno tena, ni uhalisia! Amina!

Tunajua kwa wengine sisi ni Wa Kipekee, na linaweza likasikika kama nati kwa ulimwengu, lakini linawavuta watu wote Kwake.

Njoo uingizwe kwenye Neno pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapomsikia nabii akiuambia ulimwengu jinsi sisi tulivyo Wa Kipekee 64-0614E. Tunajivunia na tunashukuru sana kusema ndivyo sisi tulivyo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

I Wakorintho 1:18-25
2 Wakorintho 12:11