21-1010 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

UJUMBE: 65-0801e Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Kundi dogo Bibi-arusi Neno Bikira wa Kristo,

Sisi ni Bibi-arusi Neno wake tukisubiri Bwana harusi Neno wetu na fungate yake ya utawala wa miaka Elfu . Tutasikiliza Sauti moja tu . “Kondoo Wangu wanaijua Sauti Yangu. Mgeni Hawatamfuata. ” Sauti yake ni nini?

Sauti ya mtu ye yote ni neno lake. Nalo ndilo Hili, Biblia, neno moja lisiongezwe Kwake au kuondolewa Kwake. Dumuni waaminifu tu kwa Sauti hiyo. “Mgeni hawatamfuata,” madhehebu.

Sauti hiyo ni Sauti Yake, izungumzayo kwenye Kanda kupitia Mfasiri pekee wa Kiungu wa Neno Lake, nabii Wake, William Marrion Branham. Ni Yesu Kristo akinena kupitia midomo ya mwanadamu. Sisi Hatujali maneno ya mwanadamu, mawazo ya mwanadamu au Fasiri ya mwanadamu, Tunaijali tu Sauti iliyothibitishwa kwa ajili ya wakati wetu. Ni BWANA ASEMA HIVI.

Mungu aliiongoza mikono ya nabii wetu. Mungu aliyaongoza macho yake katika maono. Hakuweza kusema kitu chochote ila kile alichokuwa anaangalia. Asingeweza kunena kitu, Maana Mungu Alitawala kabisa ulimi wake, kidole chake, kila kiungo cha mwili wake kilikuwa katika utawala Mkamilifu wa Mungu. Si ajabu kwamba Biblia ilisema manabii Wake walikuwa miungu; walikuwa ni sehemu ya Mungu! Yeye Alikuwa ndiye Neno la Mungu lililodhihirishwa kwa ajili ya wakati wetu.

Biblia hii inatabiri, kwa unabii, ni siku gani tunayoishi, na wakati gani tunaoishi, na ni matukio ya namna gani yanayopaswa kutukia. Inatabiri jambo hilo kikamilifu kabisa, wala haijakosea hata kizazi kimoja, wakati wote. Hakuna hata wakati mmoja ambapo imekosea, wala haitakosea, kwa kuwa waliochaguliwa tangu zamani kuliona wataliona. Ni Neno Likiungana na Neno

Katika Kila wakati, watu wanamwachilia mtu aweke fasiri yao kwenye Neno hili, na inawafanya watu wasione matukio yaliyotukia. Jambo lile lile limefanyika kwa Mafarisayo na Masadukayo.

Waliwaambia watu, “Sisi tumetiwa mafuta na Mungu. Mnatuhitaji sisi kuwambieni kile Neno linachosema. Mnatuhitaji sisi tuwafasirie ninyi. ”

Kama ilivyokuwa katika siku hiyo ndivyo ilivyo leo hii. Upande wa kudanganya ni kwamba wamepakwa mafuta na Roho Mtakatifu. Wana wito kutoka kwa Mungu kufanya huduma ya Neno. Wapo kuwaambia watu kile nabii alichosema, lakini wengi wao huweka FASIRI YAO KWAKE kwa kufanya huduma yao kuwa muhimu zaidi kuliko Sauti ya Mungu.

Angalia jinsi wanavyotaka kujaribu kukusanya watu pamoja kwenye huduma yao, kwenye fasiri yao ya kile manabii wa Mungu walichosema, lakini hawawezi kufanya jambo hilo.

Wanaficha na kuwatisha watu ili kuhalalisha kutocheza kanda katika makanisa yao kwa kusema, “Hao watu wanaweka mkazo sana kwa mtu huyo na wanamwabudu yeye na sio Yesu Kristo. Ni udhehebu kusikiliza ujumbe sote kwa wakati mmoja kutoka sehemu moja. Ndugu Branham hakuwahi kusema chezeni kanda kanisani ”, hivyo kuepuka hasa sababu Yenyewe, hawataki tu kucheza kanda katika makanisa yao. Huduma yao, ufahamu wao, wito wao, ni muhimu zaidi kuliko kusikiliza kanda kanisani. Hawatathubutu kusema kuwa, HAPANA , lakini vitendo vyao vinawasemea.

Mhudumu yeyote wa kweli, anayedai kuamini huu ni Ujumbe wa kweli wa wakati wa mwisho, ni Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu, hangekuwa kamwe na Udhuru wa kutocheza kanda katika kanisa lao. CHUNGUZA TAMSHI HILO PAMOJA NA BIBI-ARUSI NENO.

Sijawahi kusema ni lazima kila Mtu asikilize saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville, la sivyo wewe si Bibi-arusi, KAMWE. Sijawahi kumwabudu mtu . Ni Yesu Kristo ndiye anayepokea utukufu wote. Ninamwabudu Mungu aliye ndani ya huyo Mtu kama vile NENO lilivyotuambia tufanye. Jinsi gani walivyo wadanganyifu na vipofu . Soma tu Maandiko ndugu yangu, liko papo hapo.

Ibilisi ANAJUA kwamba mhudumu yeyote, au kundi la wahudumu, HAWAWEZI KAMWE kumuunganisha Bibi-arusi; Hata hawakubaliani wao kwa wao. Kama tu vile Wamethodisti, Wabaptisti, Wapresbyteri na Wapentekoste, anawezaje yeyote mmoja wao au mchanganyiko wao kumuunganisha Bibi-arusi… HAWAWEZI kabisa.

KITU PEKEE KINACHOWEZA KUMUUNGANISHA BIBI-ARUSI NI SAUTI YA MUNGU KWENYE KANDA .. ​​NA INAFANYA HIVYO !

Adui analichukia jambo hilo, kwa hivyo anajaribu kuliangamiza, lakini haitawezekana kufanya hivyo ….UTUKUFU!

Kama kawaida, wao daima, katika mwisho wa wakati, wameingia katika mchafuko kama huo kwa wanatheolojia wao na makasisi mpaka daima_ ni mchafuko. Daima fasiri yao ni mbaya, hakuna hata wakati mmoja imeshindwa kuwa mbaya. Wala hakuna hata wakati mmoja Neno la Mungu limeshindwa kuwa kweli. Hiyo ndiyo tofauti.

Kuna njia moja rahisi tu ya kuwa na hakika, Dumu na Neno, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Soma Biblia yako, itakuambia ni matukio gani yatakayotokea katika siku hii. Itakuambia juu ya malaika Wake mwenye nguvu ambaye atakuja katika siku hii. Itakuambia kudumu na Sauti Hiyo, Kudumu na mjumbe Wake Aliyemchagua.

Ikiwa Shetani anachukia Kitabu chochote cha Biblia, ni kitabu cha Ufunuo. Kiliandikwa na Kristo mwenyewe. Halafu kulingana na roho hiyo, Kristo mwenyewe lazima aweke msisitizo mwingi kuhusu malaika wake wa 7.

Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye Mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

Kristo Mwenyewe alisema dunia nzima iliangazwa kwa UTUKUFU WAKE. Yeye Hakusema iliangazwa kwa “Utukufu Wangu”. Halafu kulingana na uelewa wako, unamshtaki Kristo mwenyewe kwa yeye kuweka msisisitizo mwingi juu ya Mjumbe wake malaika wa 7.

Mjumbe huyo wa duniani alifanana sana na Kristo mwenyewe, Yohana alijaribu kumwabudu, MARA MBILI, lakini akasema, “HAPANA!, Mwabudu Mungu.” Hilo ndilo hasa tunalofanya, kumwabudu Mungu. Hatuwekei mkazo sana juu ya mtu huyo, tunasema tu kile KRISTO NENO ALICHOSEMA…. “Nchi ikaangazwa kwa utukufu wake”. Hilo Linatupa Changamko Kwa Ufunuo.

Mungu hujichagulia Mwenyewe, kwa kuchagua tangu zamani, akawachagua manabii kwa ajili ya kila wakati. Angalia jambo hilo. Yeye huweka tabia ya huyo nabii ipate kulingana na wakati huo. Mnaona, Yeye huweka mtindo wake, cho chote afanyacho. Yeye humweka kama ana elimu ama hana elimu. Yeye humwekea vipawa, namna atakavyohubiri, karama atakazokuwa nazo. Na Ujumbe wa wakati huo fulani, Mungu alichagua tangu zamani kitu hicho maalum kitendeke wala hakuna kitu kingine kinachoweza kuchukua mahali pake .

Cheza kanda, kanda yoyote , Jumapili, hakuna kinachoweza kuchukua mahali pake. Ikiwa unataka kuungana na Maskani ya Branham tunaposikiliza kanda, unakaribishwa na umealikwa kuungana nasi Jumapili saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) tunaposikia: Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii 65-0801E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko:

Mwanzo: 22: 17-18

Zaburi: 16:10 / Sura 22 yote/ 35:11 / 41: 9

Zekaria 11:12 / 13: 7

Isaya: 9: 6/40: 3-5 / 50: 6/53: 7-12

Malaki: 3: 1/sura ya 4 yote

Yohana Mtakatifu 15:26

Luka Mtakatifu : 17:30 / 24: 12-35

Warumi: 8: 5-13

Waebrania: 1: 1/13: 8

Ufunuo: 1: 1-3 / Sura ya 10 yote