21-0718 Kutoka kwa tatu

Ujume: 63-0630m Kutoka kwa tatu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Wana na Mabinti waliyodhihirishwa,

Mtu hajui ni wapi aanzie. Kufikiria, tumekuwa tukikaa pamoja katika hali ya kimbinguni, kutoka kote ulimwenguni, tukinywa kutoka kwenye maji hayo yaliyo hai, kuwa wana na mabinti zake waliodhihirishwa. Ujumbe huu unatupa ufahamu mkamilifu, unatuweka mahali petu, na unatuambia sisi ni NANI katika Kristo Yesu.

Je! Ujumbe huu unafanya nini?

“Kwa maana mimi niliwaposa, nikawachumbia kwa Kristo, kama bikira safi.”

Utukufu, Mungu alimtuma malaika-mjumbe wake wa 7 kutuposa kwake kama bikira safi. Tutahukumiwa kwa kila neno ALILOSEMA. Hiyo inamaanisha ni lazima UBONYEZE PLAY.

Aliandika Biblia yake ya kwanza angani. Kisha akaandika Biblia yake ya pili katika jiwe. Biblia yake ya tatu iliandikwa kwenye karatasi kwa ajili ya ulimwengu mashuhuri, wenye hekima wakiakili ujao. Lakini leo, siku kuu ya ufunuo, tuna Kipeo Chake kitimilifu na kikamilifu, Sauti ya Mungu yenyewe ikimwita Bibi-arusi Wake, Atoke kwa Kanda:

“Nawe UTA tukabidhi kwa Bwana Yesu atakapokuja, kama tunu za huduma YAKO.”

Na sisi sote tunapaaza sauti kwa pamoja,

“Tunajua hilo! Tunastarehe kwa uhakika . ” Kasema, “WEWE utatukabidhi kwake, na ndipo tutarudi duniani tena, tukaishi milele.”
Je! Bibi-arusi wa Kristo alipaza sauti akisema nani atatukabidhi kwa Mungu? Nabii wa Mungu kwa HUDUMA YAKE. Je! Basi Unawezaje kutotaka kucheza kanda hizi kanisani mwako?

Ni Ujumbe huu peke yake, kanda hizi, zinazoweza kulileta Kanisa katika upatano hivi na Mungu, mpaka Dhihirisho la Bwana Arusi limedhihirishwa ndani yetu. Nimejuaje kuwaambieni “kaeni na hizo Kanda,” nilirudi kwenye Ramani ili kuona kile nabii alichosema.

Ninatumaini mtu wa rohoni anaweza kulishika hilo. Nina hakika mnalishika. Lakini sijui, huko nje. Kwa vyovyote vile, huwezi kutembelea kila taifa. Unaweza kutuma kanda huko. Mungu atakuwa na njia fulani ya kumshika mtu huyo huko nje ambako mbegu hiyo inapandwa. Kweli. Na mara Nuru itakapoigusa, imetoka, imepata Uzima. Kama vile yule mwanamke pale kisimani, alisema, “ hilo hapo .” Akaishika.

Kwetu sisi ni asali mwambani, ni furaha isiyotamkika, ni dhamana iliyobarikiwa, ni nanga ya nafsini, ni tumaini na tegemeo letu, ni Mwamba wenye imara, ni kila kitu.

Nia zetu za roho hazijachafuliwa. Tunajua yakini Yeye ni nani. Tunajua yakini Yeye ni nini. Tunajua yakini sisi ni nani. Tunajua Yakini tunakoelekea. Tunajua tunayemwamini na kusadiki ya kwamba yeye aweza kukilinda kile tulichoweka Amana kwake hata siku ile.

Halafu ikiwa Mungu ametufunulia sisi ni mabalozi wake, nguvu zote zilizo Mbinguni, yote Mungu Aliyo, Malaika wake wote na nguvu zake zote zinasimama nyuma ya MANENO YETU. Mungu hana budi kuliheshimu Neno, kwa maana alisema, “Lolote Mtakalofunga duniani, hilo nitalifunga Mbinguni. Chochote Mtakachofungua duniani, hicho nitakifungua Mbinguni. Nami nawapa funguo za Ufalme. ”

Ni wakati wa kwenda Nyumbani. Kule Kutoka kumekaribia. Mungu anatuonyesha nani ni nani. Bibi-arusi wa Yesu Kristo, atatoka, kuingia katika Nchi ile iliyoahidiwa.

Katika kutoka kwake kwa kwanza, Aliwatoa katika nchi ya kawaida, akawapeleka kwenye nchi ya kawaida.
Kutoka kwa pili, Yeye aliwatoa kutoka katika hali ya kiroho, akawaingiza katika ubatizo wa kiroho wa Roho Mtakatifu.
Sasa Yeye anatuleta kutoka kwenye ubatizo wa kiroho wa Roho Mtakatifu, kurudi katika ya Milele, kwa Nguzo ile ile ya Moto, kwa mfumo ule ule uliotiwa mafuta, Mungu yeye yule akifanya mambo yale yale!

Acha upepo uvume vikali. Acha tufani itikise, tuko salama milele. Tunapumzika papo hapo kwa kila Neno.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 8:00 nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni saa 3:00 tatu Usiku ya TZ), na utegemee kila Neno Alilolinena Mungu kwa ajili ya siku yetu. Jiweke Mwenyewe tayari kwa kuja kwake kwa hivi karibuni na usikie: Kutoka kwa Tatu 63-0630M.

Ndugu. Joseph Branham

Kutoka 3: 1-12

Mwanzo Sura ya 37 yote

Mwanzo Sura ya 43 yote