21-0418 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi_arusi aliyekatwa atoke,

Mungu alitambua kwamba kulikuwa na watu duniani ambao aliowakusudia Uzima. Alitambua kuwa huu ndio wakati wa kutuma Ujumbe Wake kupitia mjumbe Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Amefanya hivyo. Sasa Bibi-arusi Wake ametambua siku yetu na Ujumbe Wake, na ametambua sisi ni nani, kuzaliwa asili kwa Neno.

Sisi ni yule Bibi-arusi ambaye aliyekuja katika onyesho la Awali mbele ya nabii. Bibi-arusi aliyefanana sana na yule aliyepita mwanzoni. Alipotuona, moyo wake uliruka kwa furaha, kwa kujua kwamba kuna Bibi-arusi ambaye atayekaa na Neno. Alipotuona, tulifanywa kwa kitu kimoja, na kuvikwa kwa kitu kimoja kama yule aliyekuwako mwanzo: Alfa na Omega. Sisi ni yule Bibi-arusi Neno kamilifu.

Mungu amembangua Bibi-arusi Wake atoke, amemkatatilia mbali na makanisa mengine yote kupitia nabii Wake, kwa Neno. Sasa, baada ya miaka elfu mbili, na kulingana na Neno Lake lililoahidiwa kwamba angefanya katika siku za mwisho, Ameizuru kambi tena. Ameizuru kambi kudhihirisha Neno Lake kwa ajili ya leo hii, kama vile alivyofanya katika siku za Musa. Kama ilivyokuwa wakati huo, ndivyo ilivyo sasa. Huyo hakuwa Musa aliyetenda hayo; Musa alikuwa mwanadamu. Ilikuwa ni Kristo.

Ilifanyaje? Iliwasumbua makuhani, kuona hao watu wakiondoka makanisani na kwenda zao. Akasema, “kama ye yote wenu akihudhuria mikutano yake, mtatengwa na ushirika. Tutawafukuza moja kwa moja kutoka katika dhehebu. “
Angalia, “Kama vile Yane na Yambre pia walivyompinga Musa,” atakuja moja kwa moja, baadhi yao. Sio, sasa, yeye hazungumzi kuhusu Mmethodisti, Mbaptisti, hapa; wao wako nje ya picha. Unaona?

Lakini ni kitu gani kinachotukia kwa Bibi-arusi? Tunakusanyika pamoja kutoka kote ulimwenguni. Tumeundwa kutoka kote nchini; kutoka New York, kutoka Massachusetts, Maine, Tennessee, Georgia, Alabama, na kote nchini na ulimwenguni kote. Sisi ni Tai tunakusanyika pamoja. “Kutakuwa na Nuru yapata wakati wa jioni.”

Kama kijana mdogo siku zote nilijiuliza, “Bwana, utaletaje Kanisa lako pamoja kama ulivyofanya Kanisa Lako la kwanza?” “Ninasoma katika Neno lako, Wewe kila wakati uliwaleta pamoja wakati ulipotaka kuwaunganisha.” “Je! Utamleta kila mmoja huko Jeffersonville?” “Utafanyaje jambo hilo?” “Je! Sote tutahitaji kukusanywa mahali pamoja?”

Sasa imefunuliwa kwangu, Sio katika makao ya kimwili ambapo Bibi-arusi Wake wanakusanyika pamoja , sio Mlima Mtakatifu, mahali Patakatifu, BIBI-ARUSI ANAKUSANYIKA KWENYE NENO LAKE, kwa kuwa hapo ndipo MAHALI PEKEE ambapo Bibi-arusi anaweza kuungana.

Mungu ameusimamisha ulimwengu ili alitimize Neno lake. Shetani anajaribu kulizuia; kujaribu kulifanyia mzaha. Anajaribu kuwafanya watu waogope kwamba ikiwa watazisikiliza Kanda, watatengwa na Ushirika, watapotea. Lakini hawezi kuzuia kile kinachotokea.

“Ondoka njiani! Nina Ujumbe wa Mfalme. ” Amina. “Mimi ni Mjumbe wa Mfalme,” Neno lililothibitishwa. Nikawazia, “Shetani, ondoka njiani! Nina Ujumbe wa Mfalme. Sina budi kwenda.”
Ni Ujumbe wa Mfalme. Hebu na tuutambue, wapendwa, kwa kuwa tumeitwa kukusanyika pamoja kwa ajili ya kupigwa kwa Baragumu. “Kwa maana Baragumu ya Bwana italia, ndipo hakutakuwa na wakati baada ya hayo.”

Hakuna furaha kubwa, hakuna upako mkubwa zaidi, kuliko kukaa pamoja katika makao ya kimbinguni na Bibi-arusi kote ulimwenguni, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikinena kupitia mjumbe wake aliyethibitishwa na kunena Neno la Uzima wa Milele.

Kumbuka katika ono langu? Nilisema, “Ikiwa watu wa Paulo wataingia, na wangu pia wataingia, kwa sababu nimefanya vile hasa alivyofanya.” Ninadumu kabisa nalo. Hao mamilioni walitupa mikono yao, wakisema, “Tunategemea jambo hilo!”

Tai watakusanyika tena Jumapili hii saa 8:00 mchana, saa ya Jeffersonville,(Ni saa 3:00 usiku ya TZ), kumsikia Kristo mwenyewe akizungumza nasi kupitia mjumbe wake aliyethibitishwa. Neno tunalotegemea. Njoo uungane nasi tunapomsikia akiuonya ulimwengu kwamba lazima wawe : Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Hosea 6
Malaki 4:5-6
2 Timotheo 3